Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, amekutana na Ujumbe kutoka Wakala wa Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi Zanzibar (ZEEA) ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Bw. Juma Amour Mohamed, katika Ofisi za Benki Kuu jijini Dar es Salaam.
Katika kikao hicho kilichofanyika tarehe 09 Februari 2024, masuala mbalimbali yamejadiliwa ikiwemo ushirikiano kati ya BoT na ZEEA katika kuwawezesha kiuchumi wananchi wa Zanzibar.