Makamu wa Rais ,Philipo Mpango akizungumza katika mahakama hiyo jijini Arusha.
Makamu wa Rais ,Philipo Mpango akiwa katika picha ya pamoja na majaji mbalimbali katika.mahakama hiyo.
**************************
Julieth Laizer ,Arusha 
Arusha. Makamu wa Rais wa Jamuhuri  ya Muungano Dk Philip  Mpango amesema, Serikali ya Tanzania inatambua umuhimu wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binaadamu na Watu(AFCHPR na itaendelea kufanya nayo kazi .
Hata hivyo, amesema kumekuwepo na changamoto kadhaa katika utekelezwaji wa hukumu za mahakama hiyo na akashauri mahakama kuboresha mahusiano na mahakama za ndani ya nchi, ili kuondoa dhana  kuwa  mahakama hiyo kuingilia uhuru wa mahakama za ndani.
Amesema  ni muhimu kuwepo na ushirikiano na mafunzo baina ya watendaji wa mahakama  majaji, Mawakili na mahakimu juu ya masuala ya haki za binaadamu .
Kauli mbiu ya mwaka wa mahakama hiyo mwaka huu ni “kuunganisha mifumo wa sheria za haki za binaadamu za kikanda na kimataifa katika mifumo ya kitaifa” 
Rais wa mahakama hiyo, Jaji Imani  Aboud akizungumza  katika ufunguzi wa mwaka wa mahakama hiyo  jijini Arusha , amesema bado nchi nyingi   hazitekelezi hukumu za Mahakama hiyo.