Mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego akiongea na wakulima waliofika ofisi kwake kwa ajili ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha sekta ya Kilimo.
Baadhi ya wakulima waliofika ofisi kwa mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego kwa ajili ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha sekta ya KilimoBaadhi ya wakulima waliofika ofisi kwa mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego kwa ajili ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha sekta ya Kilimo.
Na Fredy Mgunda, Iringa.
WAKULIMA mkoa wa Iringa wamefanya matembezi ya kumpongeza Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuwapunguzia bei ya mbolea.
Wakizungumza Mbele ya Mkuu wa mkoa wa Iringa,wakulima hao wamesema kuwa walikuwa wakinunua mbolea kwa shilingi 150,000 lakini sasa wananunua kwa shilingi 60,000 hadi 70000
“Tunampongeza na kumshukuru sana rais samia kwa kutuona sisi wakulima kwa sababu mwanzo tulikuwa tukinunua mbolea kwa laki moja elfu thelathini lakini saizi tunapata kwa elfu 60000 hadi sabini ni hatua nzuri tunampongeza mama na sasa tunaamini kila mwananchi wetu atalima”walisema
Akisoma risala Mbele ya Mkuu wa mkoa wa Iringa Abeid Kiponza alisema kuwa wana kila sababu ya kumpongeza Rais Samia kutokana na kupunguza gharama za pembejeo za kilimo hususani upande wa mbolea
“sisi wakulima wa mkoa wa Iringa tumefanya matembezi maalumu ya kumshukuru na kumpongeza mheshimiwa rais kutokana na upendo wake kwetu kutokana na mambop makubwa anayoendelea kutufanyia kwenye kilimo tanzania nzima inajua wakulima wa nyanda za juu kusini tumekuwa tukizalisha viazi,mahindi,ngano,alizeti na mazao mengine ya chakula na hatuwezi zalisha mazo vizuri bila kuungwa mkono na serikali na tumwambie usiwasikilize wanasiasa ambao wamekuwa kama wasemaji wetu wakati sio wasemaji wetu usiwasikilize”alisema
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita imeamua kutatua matatizo ya msingi kwa kuwekeza kwenye kilimo na miradi umwagiliaji.
“Sisi wote ni mashuhuda mheshimiwa rasi ameweza kutoa pikip[iki kwa maafisa ugani wote na wanatakiwa wahikikishe wanafika kama kuna maswali muulize wawahudumie nyinyi na zimetoka billion 55 mradi wa pawaga umwagiliaji kwa hiyo tunaposema mama ameupiga mwingi na ametuletea ruzuku ambayo ndio tunategemea sisi wakulima”
Hata hivyo lengo la serikali ya Rais Samia Suluhu awamu ya sita ni kuhakikisha inaboresha sekta ya kilimo na maslahi ya wakulima kwa ujumla.