Kamishna msaidizi idara ya uendelezaji wa sekta ya fedha wizara ya fedha na mipango ,Janeth Hiza akizungumza katika siku hiyo ya wahasibu duniani.
Naibu Mkuu wa chuo taaluma utafiti na ushauri wa kitaalamu chuo cha uhasibu Arusha ,Profesa Epaphra Manamba akizungumza katika siku ya wahasibu duniani chuoni hapo

Wanafunzi wanaosomea kozi ya uhasibu katika chuo cha uhasibu Arusha wakisikiliza mada mbalimbali chuoni hapo leo.
*********************
Julieth Laizer,Arusha.
Arusha.Wataalamu wa maswala ya Fedha na Mahesabu nchini wameaswa kuwa waadilifu wanapotekeleza majukumu yao na kuwa washauri wazuri kwa jamii katika kufafanua dira ya maendeleo ya uchumi nchini .
Hayo yamesemwa leo novemba 11 jijini Arusha na Kamishna msaidizi idara ya uendelezaji wa sekta ya fedha wizara ya Fedha na Mipango,Janeth Hiza wakati akizungumza katika siku ya wahasibu duniani iliyofanyika katika chuo cha uhasibu Arusha .
Hiza amesema kuwa,wataalamu hao wanapaswa kuwa waadilifu na kutanguliza weledi katika utendaji kazi wao kwani idara hiyo ni muhimu sana kwa malachi ya nchi kwa ujumla.
Aidha amewataka wahasibu kuhakikisha wanajifunza udhibiti wa fedha haramu,pamoja na kuhakikisha wanajiunga na bima mbalimbali kwa ajili ya maendeleo yao .
“Nawaombeni sana mkajifunze kupata huduma jumuishi za fedha na mkatumie elimu zenu kufundisha jamii kuhusu elimu juu ya matumizi ya fedha na nidhamu ya fedha kwa ujumla kwani nyie ndio mnaotegemea katika jamii nzima inayowazunguka .”amesema .
Kwa upande wake Naibu Mkuu wa chuo taaluma utafiti na ushauri wa kitaalamu chuo cha uhasibu Arusha ,Profesa Epaphra Manamba amewataka wahasibu hao kuhakikisha wanafanya kazi kulingana na sheria na taratibu zilizopo huku wakifuata maadili na matumizi sahihi ya fedha.
Profesa Manamba amewataka wanafunzi kufanya kazi kulingana na elimu na maadili waliyopata chuoni hapo ili wakawe mfano wa kuigwa katika jamii.
“maadhimisho ya siku ya wahasibu itafanyika jijini Mwanza yakiwa na dhumuni la kuboresha uchumi na kuondoa umaskini ili kukuza ufanisi wa matumizi ya fedha na kutoa elimu juu ya masomo ya fedha .”amesema Profesa.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa idara ya fedha na uhasibu chuo cha IAA ,Dennis Hyera amesema kuwa,Sikh ya wahasibu duniani kwa mara ya kwanza iliadhimishwa mwaka 1972 na wanajumuiya ya CPA wa San Diego Chapter katika taasisi ya Management Accountants .
Hyera amesema kuwa, siku ya wahasibu duniani imeanzishwa kwa ajili ya kuwahamasisha vijana walioko kwenye tasnia nzima ya uhasibu mnamo mwaka 1976 taasisi mbalimbali zilialikwa rasmi kusherehekea siku ya wahasibu duniani na ikarasimishwa kusherehekewa mahali popote na nchi yoyote kila ifikapo novemba 10 kila mwaka .
Amesema kuwa, siku ya wahasibu duniani imekuwa siku yenye manufaa makubwa kwa kujenga mtandao na kufungua fursa mbalimbali kwa wahasibu nchini hivyo chuo kitaendelea kuiadhimisha siku hiyo ,huku akihimiza wahasibu kuendelea kudumisha kanuni na taratibu za kiuhasibu na kufuata viwango vyote vilivyoanzishwa na bodi ya wahasibu Tanzania ili waendelee kuwa wahasibu bora wenye kuleta chachu ya maendeleo kwa Taifa zima na kuleta maendeleo katika sekta ya fedha na uhasibu.
Makamu wa Rais serikali ya wanafunzi (IAASO),Shazma Edward amesema kuwa,kupitia siku ya wahasibu duniani wamejifunza mambo mengi ikiwemo kutanguliza maadili na uzalendo katika utendaji kazi wao wa kila siku ili taaluma hiyo iendelee kuboreka zaidi.
