Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ndani ya moja ya mabehewa ya Reli ya Kisasa (SGR) ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) ambayo yanatengenezwa katika kiwanda cha kampuni ya Sung Shin Rolling ya Korea. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo ametembelea kiwanda hicho na kujionea maendeleo ya utengengenezaji wa mabehewa hayo, Oktoba 25, 2022. Wengine pichani kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Korea, MheTogolani Idrissa Mvura, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mabarouk, Rais na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sung Shin Roliing, Bw. Gye Shul Park na kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Emmanuel Tutuba.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Bw. Gye Shul Park ambaye ni Rais na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sung Shin Rolling Stock ya Korea (kushoto kwake) kuhusu mabehewa ya Reli ya Kisasa (SGR) ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) wakati alipotembelea karakana ya kutengeneza mabehewa ya treni inayomilikiwa na kampuni hiyo, Oktoba 25, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ndani ya moja ya mabehewa ya Reli ya Kisasa (SGR) ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) ambayo yanatengenezwa katika kiwanda cha kampuni ya Sung Shin Rolling ya Korea. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo ametembelea kiwanda hicho na kujionea maendeleo ya utengengenezaji wa mabehewa hayo, Oktoba 25, 2022. Wengine pichani kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Korea, MheTogolani Idrissa Mvura, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mabarouk, Rais na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni yaSung Shin Roliing, BW. Gye Shul Park na kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Emmanuel Tutuba.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Muonekano wa baadhi ya mabehewa ya Reli ya Kisasa (SGR) ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) ambayo yanatengenezwa katika kiwanda cha kampuni ya Sung Shin Rolling ya Korea. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo ametembelea kiwanda hicho na kujionea maendeleo ya utengenezaji wa mabehewa hayo, Oktoba 25, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
***********************
*Ni yale yanayotengenezwa nchini Korea Kusini kwa ajili ya SGR
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na maendeleo na kasi ya ujenzi wa mabehewa mapya kwa ajili Reli ya Kisasa (SGR) ya Shirika la Reli Tanzania yanayotengenezwa na kampuni ya Sung Shin Rolling Stock (SSRT) iliyoko nchini Korea Kusini.
“Kati ya mabehewa 81 ambayo Tanzania inatengeneza kutoka kwenu, tayari 36 yamekamilika na yameshapelekwa nchini Tanzania na 45 yaliyobaki yanategemewa kukamilika Machi, 2023. Mabehewa haya ni ya daraja la tatu na yatatoa huduma zote muhimu.”
Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo (Oktoba 24, 2022) mara baada ya kutembelea kampuni ya SSRST inayotengeneza mabehewa na injini za treni nchini Korea Kusini.
Kadhalika, Waziri Mkuu amemkaribisha nchini Rais wa Kampuni hiyo Gye Shul Park aje kuwekeza nchini Tanzania kutokana na fursa mbalimbali zilizopo ikiwemo mpango wa Serikali wa kuendelea kuiboresha sekta ya usafiri wa reli
“Mnakiwanda kikubwa, teknolojia ya hali ya juu pamoja na utaalamu na watalaam kwenye eneo hili. Kwa sasa tuna mipango mikubwa ya kuendelea kuiboresha sekta hii ya usafiri wa reli, yapo maeneo tofauti kwenye mpango wa kuunganishwa na reli ya kisasa (SGR), nakukaribisha kuja kuwekeza kitu kama hiki Tanzania.”
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa alitembelea kituo cha Seamul Undong ambacho ni taswira ya maendeleo ya Korea kupitia mpango wa kuviwezesha vijiji ambao unatekeleza mpango huo nchini Tanzania katika mkoa wa Morogoro (Pangawe) na Zanzibar.
Mheshimiwa Majaliwa alimshukuru Rais wa Kituo hicho na kumuomba kuendelea kutoa ushirikiano ili kukuza zaidi mpango huo na kufikia maeneo mengi zaidi.
“Mfumo huu kwasasa umekuwa wa kitaifa, ushirikishwaji wa Wananchi ni mkubwa, sasa tunataka tuikuze zaidi, haya maeneo ya Morogoro na Zanzibar tunataka yawe mifano, kwenye utekelezaji wa eneo hili”
Pia, Mheshimiwa Majaliwa alitembelea kituo cha Ubunifu cha CEIC kilichopo kikichopo katika mji wa Pangyo