Victoris Massawe( wa pili kulia) ambaye ni moja ya wanafunzi waliosoma katika Shule ya Ruvu Sekondari ambaye pia ni mmoja ya Waratibu wa michango ya wanafunzi akikabidhi tofali kwa Waziri MKuu wa Wanafunzi wa Shule hiyo Minael Katamba (kushoto) jana baada ya wanafunzi waliosoma kwenye shule hiyo kuanzia mwaka 1977 mpaka sasa kuamua kuchangia vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa uzio wa Shule hiyo.
Na Mwandishi Wetu, Pwani
wa Shule ya Ruvu Sekondari umesema kiasi cha Sh.milioni 794.9 kinahitajia kwa
ajili ya kufanikisha ujenzi wa uzio shule hiyo kwa lengo la kuimarisha
usalama wa wanafunzi wa kike 850 wanaosoma kwenye shule hiyo.
Akizungumza jana wakati wa tukio la upokeaji wa vifaa vya
ujenzi (matofali na nondo) vilivyotolewa na wanafunzi waliosoma shule hiyo
tangu ilipoanzishwa mwaka 1977 mpaka sasa,
Mkuu wa Shule ya Ruvu Sekondari Juliana Chimanzi alisema
uzio wa shule ni muhimu kwani kuna changamoto ya mifugo kuingia eneo la shule
lakini pia wezi na vibaka.
“Nitoe Serikali, wadau na kwa namna ya kipekee
wanafunzi waliopita hapa kokote waliko watusaidie.Shule yetu ina idadi kubwa
wanafunzi wasichana ambao wanafikia 850 , tunahitaji kuweka ulinzi kwa
kujengewa uzio.Tumefanya tathimini Sh.Sh.milioni 794.9 zinahitajika,”aamesema.
Awali akizungumza baada ya kukabidhi vifaa hivyo vya
ujenzi, Mwenyekiti wa Wanafunzi waliosoma kwenye shule hiyo kwa nyakati tofauti
Veronica Chambuso kuanzia mwaka 1977 amesema wameona wachangishane ili peleka
vifaa vitakavyosaidia kuanza ujenzi wa uzio.
“Tumeleta matofali na nondo , huu ni mwanzo lakini
tunaendelea kuwaomba waliosoma Ruvu Sekondari kuanzia mwaka 1977 mpaka sasa na
miaka inayokuja, wazazi , wafadhili na wale wanaoguswa na ulinzi wa watoto wa
kike tushirikiane kwani ukimlinda mtoto wa kikekwani akapata elimu
itamsaidia na taifa litanufaika,”alisema Chambuso.
Amefafanua kwamba shule hiyo ilijengwa mwaka 1977
baada ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kuomba msaada Serikali ya Cuba,
hivyo wanamshukuru kwa upendo wake na katika kumuenzi wameona kuna uhitaji
mkubwa wa uzio.
Kwa upande wao Waratibu wa Uchangiaji huo ambao nao ni
sehemu ya wanafunzi waliosoma shule hiyo Devota Makililo na Victoris Massawe
wameendelea kuhamasisha wadau kuendelea kuchangia ujenzi huo.
“Tunaomba wadau na Wizara ya Elimu kuona huruma kwa shule
ya wasichana watusaidie kwenye kujenge uzio.Pia kwa unyenyekevu mkubwa
tunamuomba Rais Samia Suluhu Hassan atusaidie kufanikisha ujenzi huu.Watoto
kike wakihitaji kuangaliwa na amekuwa akilisemea hilo mara kwa mara,”ameongeza.
Wakati huo huo Dada Mkuu wa Shule ya Sekondari Ruvu
Jacquline Mgisha anayesoma kidato cha Sita alisema wanashukuru wanafunzi
waliopita shuleni hapo kutambua umuhimu wa jambo hilo.
“Uzio ni muhimu sana kwetu , hivi makazi ya watu yamekuwa
karibu na shule na hivyo kuhatarisha usalama wa wanafunzi.Pia tunamuomba mama
yetu Rais Samia Samia Suluhu kutusaidia na hatimaye tuwe na uzio na sisi tutamlipa
kwa kufanya vizuri kwenye masomo,”amesema.