Na Dotto Mwaibale, Singida
WAHITIMU wa Kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Mtipa iliyopo
Manispaa ya Singida wameaswa kutojiingiza kucheza kamari (kubet) kwani ni janga kubwa nchini.
Wito huo umetolewa na Mjumbe wa Kamati ya Siasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Iddi Maalim
ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kumi na nne 2022 ya kidato cha nne yaliyofanyika leo Oktoba 22, 2022 katika viwanja vya shule hiyo
na kuhudhuriwa na wazazi na wageni waalikwa kutoka shule jirani.
“Nchi yetu hivi sasa inashuhudia mambo ambayo hayapo hata kwenye dini
vijana wetu wengi leo hii ukipita mijini utakuta wanashughulika na kitu
kinaitwa kubeti au kucheza kamari hakika ili ni tatizo kwenye elimu wanabeti
utafikiri watapata fedha” alisema Maalim.
Maalim alisema tangu ameanza kuwaona wakibeti hajawahi kushuhudia mtu
akinunua nyumba yake zaidi ya kuambulia sH.100,000, SH.20,000 na elfu 10 huku
akivutika na anaendeleakucheza analiwa na kurudi nyumbani akiwa hana kitu.
Alisema mchezo huo umtengenezwa na walioubuni ili kuchota pesa kutoka kwetu
hivyo anapenda kusisitiza kuwa hauna faida na wasidanganyike kwani
inawanufaisha wale walioutengeneza kwa kutumia mahesabu makali.
Akizungumzia masuala ya elimu alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa
kuendelea kutoa elimu bila ya malipo pamoja na kutoa fedha nyingi kuboresha
miundombinu ya shule mbalimbali hasa ujenzi wa vyumba vya madarasa kote nchini
na Shule ya Sekondari ya Mtipa ikiwa ni moja ya shule iliyonufaika kwa
kupata madarasa saba..
Maalim alitumia nafasi hiyo kuwaasa wahitimu hao waangalie mifano iliyopo
ya viongozi au watu mashuhuri waliojituma na kufanya kazi kwa bidii kwenye
elimu na kwenye maisha na akawata wajifunze kutoka kwao.
Aidha Maalim aliwata wahitimu hao kuwaenzi wazazi wao kwa kusoma kwa bidii
huku wakifuata nasaha zao juu ya kujiheshimu, kujitunza na akawaomba wazazi
wasichoke kuwahimiza watoto wao kwenda shuleni ikiwa ni pamoja na kupitia
madaftari yao kuona kile wanachofundishwa.
Mkuu wa shule hiyo Anna Hamphrey Mrisho alisema shule hiyo licha ya kuwa na
changamoto za hapa na pale kama upungufu wa walimu na mambo mengine alitaja
baadhi ya mafanikio kuwa ni pamoja na kupokea fedha kutoka Serikalini kuu
Sh.140,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa uyumba saba vya madarasa.
Alitaja mafanikio mengine ni kuwawezesha wanafunzi kujitambua kuhusu maisha
yao, robo tatu ya wanafunzi kuweza kukaa kambi ya masomo kwa miezi mitatu ili
kuinua taaluma yao, kupata nishati ya umeme kwenye vyumba viwili katika jengo
la utawala, kuborsha ofisi ya mkuu wa shule na kukamilisha vyumba vyote vya
maabara.