Baadhi ya wananchi wa waliojitokeza mbele ya Kamati ya Kusikiliza Migogoro ya Ardhi ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakisikiliza maelekezo ya wataalamu wa Wizara hiyo jana walipofika Ofisi za Kata ya Mkonze Jijini Dodoma kusikiliza na kutatuliwa migogoro yao.
Sehemu ya wataalamu wa Kamati ya Kusikiliza Migogoro ya Ardhi ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakisikiliza mwananchi ambaye alifika mbele ya wataalamu hao walioweka kambi Ofisi za Kata ya Mkonze Jijini Dodoma kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi ya wananchi wa kata hiyo mapema jana Jijini Dodoma.
Sehemu ya wataalamu wa Kamati ya Kusikiliza Migogoro ya Ardhi ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakisikiliza mwananchi ambaye alifika mbele ya wataalamu hao walioweka kambi Ofisi za Kata ya Mkonze Jijini Dodoma kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi ya wananchi wa kata hiyo mapema jana Jijini Dodoma.
Kamishna wa Ardhi Nchini Nathaniel Methew akifuatilia kwa makini suala la Mwananchi wa Kata ya Mkonze Jijini Dodoma aliyefika Mbele ya Kamati ya Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi ya Wizara ya Ardhi kuwasilisha malalamiko yake ili yaweze kupatiwa ufumbuzi jana Jijini Dodoma.
………………………………………
na Anthony Ishengoma-Dodoma.
Wakazi takribani 150 wa Kata ya Mkonze Jijini Dodoma wamejitokeza mbele ya Kamati iliyoundwa na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Allan Kijazi iliyo jikita Jijini Dodoma kuhakikisha inamaliza kero zote za ardhi ndani ya Jiji la Dodoma.
Wakazi hao wamejitokeza kwa makundi tofauti kutoka mitaa ya kata ya Mkonze ambapo zoezi limeanzia ili kuwasilisha malalamiko yao mbele ya kamati hiyo uku madai yao yakitofautiana kulingana na aina ya migogoro ambayo kila mwananchi anakabiliana nayo.
Akifafanua kuhusu aina ya malalamiko ambayo Kamati imeyabaini baada ya kukutana na Wananchi wa Kata hiyo Kamishna wa Ardhi wa Ardhi Nchini Nathaniel Methew alisema mpaka sasa Kamati imebaini kuwa kuna migogoro muda mrefu ambayo ilianza tangu enzi za Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma CDA hivyo kutoa taswira tofauti ya namna migogoro hiyo uilivyojitokeza.
Kamishna Methew aliongeza kuwa pia timu yake imebaini pia migogoro hiyo umechangiwa na baadhi ya taratibu za urasimishaji viwanja ambao haukuzingatia uwiano wa asilimia 30/70 hivyo baadhi ya wananchi kushindwa kupata asilimia zinazotakiwa jambo ambalo pia limezua mamalalamiko hivyo timu hiyo itaangazia namna bora ya kutatua kero hiyo.
Aidha Kamishna ametaja chanzo kingine cha migogoro hiyo Kata ya Mkonze kuwepo kwa kundi kubwa la wananchi wanaolalamikia eneo la ukanda wa kijani uliopo eneo la Biawana na kusema kuwa Wizara itaweka utaratibu wa kuona namna bora ya kushughulikia mgogoro huo kwa wananchi wa wa eneo hilo.
Akiangazia zaidi kuhusu malalamiko hayo Kamishna Methew alitaja uwepo wa changamoto ya umilishikaji viwanja mala mbili au kumilikiwanja kimoja kwa zaidi ya mtu mmoja jambo ambalo timu ya wataalam inalifanyia kazi ili kutoa haki kwa wakazi hao.
Mzee John Samwel Mlonganile mkazi wa Kata ya Mkonze aliviambia vyombo vya habari kuwa anaiomba serikali kuingilia kati na kumaliza mgogoro wa Shamba lake ambalo anadai limemegwa na Shirika la Umeme TANESCO bila kumpa fidia akidai swala lake na wenzake 47 wamejaribu kuwasilisha mamalamiko yao katika ngazi mbalimbali bila mafanikio.
Mzee Mlonganile amesema amemiliki shamba hilo toka Mwaka 1945 na tangu wakati huo ameishi hapo akifanya shughuli za kilimo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya maji hivyo kuitaka Serikali kuingilia kati kumaliza mgogoro wao dhidi ya TANESCO.
Naye Diwani wa Kata ya Mkonze Bw. David Boshera ameyataja madhara ya Migogoro ya Ardhi isiyokwisha ni kwa baadhi ya Wananchi kukosa imani na Serikali lakini pia akaonya upendeleo wa kwa watu wenye nguvu kifedha kupewa upendeleo katika umilikaji ardhi na hivyo kuleta chuki isiyokwisha miongoni wa wanajamii.
Naye Bi. Christina Elias Mtipa alikunuliwa na vyombo vya habari akisema yeye ni mjane na hana pakwenda wakati akipinga sheria inayosema ardhi ni mali ya serikali uku akioji kama Mwenyezi Mungu alifanya makosa kumuumba juu ya ardhi ambayo serikali inadai siyo mali yake.
Aidha Bi. Christina anaongeza kuwa kwa uwezo wake haweze kuvamia ardhi ya Taasisi kama TANESCO anachojua yeye aliambiwa na serikali kuwa ardhi yao ilikuwa inatengwa kwa ajili ya Shule na Hospitali kinyume chake Shirika limejenga uzio bila kutoa fidia kwa wananchi.
Zoezi la utatuzi wa Migogoro ya Ardhi ni endelevu na tayari serikali imefanya zoezi kama hilo Jijini Dar es Salaam na linaendelea katika Kata nyingine zinazounda Jiji la Dodoma na litaendelea sehemu nyingine za Tanzania zinzokabiliwa changamoto ya Migogoro ya Ardhi.