*Awahimiza watanzania kuunga mkono jududi za Serikali za kuleta maendeleo
Said Mwishehe,Michuzi TV-Manyara
KATIBU
wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka
ameendelea kuhimiza wananchi wote kuhakikisha wanashirikiana na Serikali
ya Awamu ya Sita chini ya uongozi mahiri wa Rais Samia Suluhu Hassan
katika kuleta maendeleo na uongozi wa Rais umekuwa kinara katika kutenda
haki, demokrasia na utawala bora.
Aidha amesema tangu Rais
Samia ameingia madarakani amekuwa na uthubutu wa kufanya mambo makubwa
kwa ajili ya kuhakikisha wananchi wanakuwa na maendeleo huku akiwataka
wananchi na shaka yoyote kwani Rais atawavusha salama na ataendelea
kuwatumikia kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo mkubwa.
Akizungumza
kwenye mikutano yake aliyofanya mkoani Manyara kwa nyakati tofauti
Shaka amesema uongozi wa Rais Samia pamoja na mambo mengine ya
kimaendeleo umekwenda kufungua uhuru, haki na demokrasia kwa kila mmoja
wetu na lengo ni kuhakikisha wananchi wanashiriki katika shughuli
mbalimbali za ujenzi wa taifa la Tanzania.
“Rais Samia Suluhu
Hassan amekuwa kinara katika kuheshimu misingi yakutenda haki,
demokrasia na utawala bora na tangu alipoingia madarakani ameweka
mazingira mazuri ya kufanya siasa hapa nchini.
Shaka amesema
wananchi hivi sasa ni mashahidi wameshuhudia vyama vya siasa na
wanasiasa wakiwa huru kufanya shughuli zao za kisiasa bila kusumbuliwa
tofauti na huko nyuma.“Rais Samia ametoa uhuru mkubwa kwa wanasiasa na
vyama vya siasa kufanya siasa kiungwana na kuvumiliana” amesema Shaka na
kuongeza
“Rais Samia tangu aingie madarakani ameshakutana mara
mbili na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe lakini pamoja viongozi
wengine wa upinzani.Tunaposema Rais Samia amekuwa kinara wa haki, kinara
wa demokrasia na kinara wa utawala bora tunayo mifano.
“Ndio
maana husikii wanasiasa wakilalamika lakini hata yale mambo ya kusikia
fulani kapotea , haonekani siku hizi hayapo tena.Watu wako huru kufanya
shughuli zao na wala hawasumbuli, Rais Samia nia yake ni njema kwa taifa
hili hivyo ni wajibu wetu kumuunga mkono na kumpa ushirikiano.”amesema
Shaka.
Pamoja na hayo Shaka amewataka wananchi wote ujumla
kujiandaa kwa mambo makubwa zaidi ya kufurahisha ndani ya utawala wa
Rais Samia na kwa uthubutu ambao amekuwa akiuonesha ni imani yake yajayo
yanafurahisha zaidi.
Hata hivyo katika ziara yake kwenye Mkoa
huo shaka ameendelea kuwakumbusha wakuu wa wilaya, mikoa na wakurugenzi
wote nchini kuhakikisha wanaelezea mafanikikio yaliyopatikana kwenye
maeneo yao kotokana na fedha wanazopewa na Serikali badala ya kukaa
kimya wakati kuna mambo makubwa ya maendeleo yamefanyika.
KATIBU
wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Shaka Hamdu
Shaka akizungumza kwenye moja ya mikutano yake ya ndani mjini
Babati,mkoani Manyara akiwa kwenye ziara yake ya kujitambulisha mbele ya
wanachama wa ccm , kama mlezi mpya wa chama hicho akichukua nafasi ya
Waziri mkuu mstaafu Mzee Mizengo Pinda.
Wanachama
wa CCM mjini Babati wakimsikiliza Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Shaka Hamdu Shaka alipokuwa akizungumza nao
kwenye kikao cha ndani
Wanachama
wa CCM mjini Babati wakifurahia jambo baada ya kumsikiliza Katibu wa
Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Shaka Hamdu Shaka
alipokuwa akizungumza nao kwenye kikao cha ndani. PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MMG