Kamanda wa polisi mkoani Arusha, Justine Masejo akizungumzia ajali hiyo jijiji Arusha (Happy Lazaro)
****************************
Happy Lazaro,Arusha.
Arusha.Watu sita wamefariki kwa ajili na wengine wanne wamejeruhiwa ajali baada gari ya abiria Toyota Noah kugongana na lori aina ya Scania katika eneo la Alkatani Kata ya Sepeko wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha .
Ajali hiyo imetokea saa nne usiku wa kuamkia leo April 20,2022, katika barabara ya Arusha Babati.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuyataja magari hayo yaliyopata ajali kuwa ni Toyota Noah yenye namba za usajili T.189 DFY likitokea Arusha mjini kwenda Karatu na lori lenye namba za usajili T.250 CAA ambapo lori hilo lilikuwa linatokea Makuyuni kwenda Arusha mjini.
Kamanda Masejo amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Lori ambaye alishindwa kulimudu gari hilo na kuhamia upande mwingine wa Barabara na kusabisha kugonga gari Noah hiyo.
Kamanda Masejo amesema kuwa Jeshi hilo linamshikilia dereva wa Lori aliyesababisha ajali hiyo.
Kamanda Masejo amesema kuwa bado wanaendelea kufanya uchunguzi kufahamu majina halisi ya abiria waliofariki katika ajali hiyo na amewaomba wananchi kufika katika hosptali ya rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru kutambua miili ya marehemu.
Masejo ametoa wito kwa watumiaji wa vyombo vya moto kuwa waangalifu wakati wamatumizi ya vyombo hivyo ilikupunguza ajali ambazo zinagharimu maisha ya watu.