*************************
Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Ilemela kimepokea vifaa kwaajili ya zoezi la uchaguzi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo hilo Mhe Dkt Angeline Mabula vyenye jumla ya shilingi milioni 12,848,000 ikiwemo Ream 582 zenye thamani ya shilingi 8,148,000, Kalamu boksi 20 zenye thamani ya shilingi 260,000 pamoja na vifaa vyengine kwaajili ya kuimarisha chama kama Luninga mbili Kwa makada wa vijiwe vya Kahawa vya kata ya Kirumba na Mwigulu kata ya Kawekamo vyenye thamani ya shilingi 630,000, Bati 22 kwaajili ya kupaua ofisi ya CCM kata ya Kahama zenye thamani ya shilingi 480,000, Gharama za usafiri kwa wakurugenzi wa uchaguzi wa kata 19, matawi 126 na jumuiya zao jumla ya shilingi 3,330,000
Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula amesema kuwa ameamua kutekeleza zoezi hilo kama sehemu ya wajibu wake kwa Chama Cha Mapinduzi pamoja na kuunga mkono juhudi za Mwenyekiti wa Chama hicho ngazi ya taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan katika kuwarahisishia watendaji wa Chama hicho kutekeleza zoezi la uchaguzi Kwa amani, haki na uhuru
‘.. Ni wajibu wangu kuwezesha vitendea kazi vya uchaguzi kwa matawi, kata na hata wilaya, Tunajua Kuwa si matawi yote au kata zote zenye uwezo wa kugharamia shughuli zote za uchaguzi ..’ Alisema
Aidha Mhe Dkt Mabula amemshukuru Rais Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kipindi cha uongozi wake wa mwaka mmoja ameweza kuipatia wilaya ya Ilemela zaidi ya kiasi cha shilingi Bilioni 29 kwaajili ya Utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo zahanati ya Kayenze, stendi ya kisasa ya mabasi Nyamhongolo, Ujenzi wa madarasa kupitia fedha za UVIKO-19.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ilemela Nelson Meshack amempongeza Mbunge huyo Kwa Jitihada zake za kusaidia Chama huku akiwataka viongozi waliopokea vifaa hivyo kuvitumia kama ilivyokusudiwa
Nae Katibu wa CCM wilaya ya Ilemela Bi Aziza Isimbula amewasisitiza watendaji wa Chama hicho Kwa ngazi ya kata na matawi kuhakikisha wanawasilisha taarifa za zoezi la uchaguzi katika maeneo yao kila siku linapokamilika
Cosmas Lutebeka ni Katibu wa UVCCM Kata ya Kahama amemshukuru Mbunge huyo Kwa kusaidia mabati yatakayotumika kukamilisha ofisi Yao iliyokwama Kwa muda mrefu