Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini akiwasilisha mada kuhusu Dhana ya Mgawanyo wa Madaraka na Namna ya Kudhibiti Muingiliano wa Madaraka ya Mihimili ya Dola katika Semina ya Mafunzo ya kuwajengea uwezo Wajumbe wa Kamati ya Uongozi, Makamu Wenyeviti wa Kamati na Tume ya Utumishi wa Bunge yanayoendelea leo katika ofisi ndogo za Bunge, Tunguu Zanzibar.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Zungu (Mb), akiongoza semina ya mafunzo ya kuwajengea uwezo Wajumbe wa kamati ya uongozi, Makamu Wenyeviti wa kamati na Tume ya Utumishi wa Bunge yanayoendelea leo katika ofisi Ndogo za Bunge, Tunguu Zanzibar.Semina hiyo imewasilishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, mada kuhusu Dhana ya Mgawanyo wa Madaraka na Namna ya Kudhibiti Muingiliano wa Madaraka ya Mihimili ya Dola.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge na Mbunge wa Jimbo la Tabora Kaskazini, Mhe. Almas Maige na akichangia jambo kuhusu mada ya Dhana ya Mgawanyo wa Madaraka na Namna ya Kudhibiti Muingiliano wa Madaraka ya Mihimili ya Dola iliyowasilishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini leo, katika ofisi ndogo za Bunge, Tunguu Zanzibar.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Dkt Eliazer Feleshi akitoa ufafanuzi wakati wa semian ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa kamati ya uongozi Makamu Wenyeviti wa Kamati na Tume ya Utumishi wa Bunge yanayoendela leo katika ofisi ndogo za Bunge, Tunguu Zanzibar. Semina hiyo imewasilishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, mada kuhusu Dhana ya Mgawanyo wa Madaraka na Namna ya Kudhibiti Muingiliano wa Madaraka ya Mihimili ya Dola.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini akiteta jambo na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Zungu (Mb), baada ya kumaliza Semina ya Mafunzo ya kuwajengea uwezo Wajumbe wa Kamati ya Uongozi, Makamu Wenyeviti wa Kamati na Tume ya Utumishi wa Bunge yanayoendelea leo katika ofisi ndogo za Bunge, Tunguu Zanzibar.