Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Wilaya ya Singida, William Nyalandu akizungumza kwenye uzinduzi huo. |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Eliya Digha akizungumza kwenye uzinduzi huo. |
Mratibu wa Miradi wa Taasisi hiyo mkoani hapa Ibrahim Mghama akisoma risala kwenye uzinduzi huo. |
Burudani zikitolewa kwenye uzinduzi huo. |
Na Dotto Mwaibale, Singida
MKUU wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Mulagiri
ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wananchi
waliovamia na kufanya shughuli za kilimo, ufugaji na uchomaji mkaa kwenye
misitu ya Munkhola na Mgori ili kudhibiti uharibifu mkubwa wa mazingira
unaofanyika kwenye misitu hiyo.
Muragili alitoa agizo hilo wakati akizindua zoezi la
upandaji miti iliyotolewa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Trees for the
Future Tanzania katika Kijiji cha Munkhola Kata ya Mgori wilaya humo ambapo
miche ya miti 3000 inatarajiwa kupandwa kwenye maeneo hayo ya misitu.
“Wale wote walioenda kulima kwenye maeneo hayo
wakamatwe kwani tunawajua hatuwezi kulinda misitu yetu lakini watu wachache wanaendelea kuhalibu, najua mnamahitaji makubwa ya chakula lakini hatuwezi kuhalibu mazingira kwa gharama ya chakula ili jambo haliwekani” alisema Muragili.
Muragili alisema kila mtu wilayani humo ana wajibu wa
kuitunza misitu na akatumia nafasi hiyo kuipongeza Taasisi ya Trees for the
Future Tanzania kwa jitihada zake inazozifanya za kuisaidia Serikali katika utunzaji wa mazingira.
Katika hatua nyingine Muragili ameagiza kila kaya katika
wilaya hiyo ihakikishe inalima ekari isiyo pungua moja ya zao la mtama ili kukabiliana na uhaba
wa chakula ambao utaweza kutokea kutokana
na ukosefu wa mvua.
“Ili ni agizo watendaji na viongozi wote wa halmashauri
nitafanya ukaguzi wa kaya hadi kaya na kaya ambayo itakutwa haijalima mtama tuaiadhibu ni lazima
tuwe na zao la tahadhari ikitokea bahati mbaya neema ya Mungu haijatushukia
hatujapata mvua mpaka mwezi wa tano na ikatokea bahati mbaya mazao ya mahindi
tukayakosa basi mtama liwe zao la kutuokoa” alisema Muragili.
Mragili aliwashauri wananchi hao kupanda mazao mengine
yanayotumia maji kidogo jambo litakalosaidia kupata chakula badala ya kusubiria
kulima mazao yanayotumia maji mengi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Heri Rashid alisema
taasisi hiyo inajihusisha na uhamasishaji wa kilimo endelevu kwa kutumia miti huku
wakiamini kuwa miti ndio vyanzo vizuri vya maisha na vipo katika mazingira.
Alisema mazingira yanaharibiwa sana kutokana na shughuli za
kibinadamu kama kukata miti kwa ajili kilimo, kujengea,malisho ya mifugo na shughuli
mbalimbali imepelekea maeneo mengi kuwa wazi na kuharibu uoto wa asili hivyo wanashirikiana na Halmashauri
ya Wilaya ya Singida kama juhudi zao za kuhamasisha wananchi kupanda miti kwa
wingi ili waweze kurudisha uoto wa asili na hali ya hewa kurudi katika hali
yake ya kawaida.
Alisema miaka ya nyuma Singida ilikuwa na mvua za kutosha na
vyanzo vya maji vilikuwa vingilakini sasa hali hiyo haipo tena ndio maana Taasisi hiyo
imekuwa ikifanya kazi ya kuhamasisha upandaji wa miti.
Mratibu wa Miradi wa Taasisi hiyo mkoani hapa Ibrahim Mghama alisema katika kutekeleza
malengo yake ya kupanda miti, inawawezesha kifedha wadau wa
maendeleo mbalimbali wanaojihusisha na shughuli za za upandaji miti na uhifadhi
wa mazingira nchini ikiwemo Magereza Tanzania kupitia Gereza la Uyui-Tabora,
Ilagala-Kigoma, Msalato-Dodoma, Manyoni-Singida na Gereza la Shinyanga.
Aidha alisema taasisi hiyo inasaidia asasi za kiraia
zinazofanyakazi na wakulima ambazo ni ADESE
na WAENDELEE za Mkoa wa Singida, TaDeCaO na Frontie Friends
of Environment za Mkoa wa Tabora, Women Against Poverty ya Mkoa wa Dar es
Salaam, Twitange ya Mkoa wa Iringa, Environment Develepment Group na Life
Securing and Relief Services za Mkoa wa Shinyanga na Friends of Lake Tanganyika
ya Mkoa wa Kigoma na kuwa kwa kipee taasisi hiyo inashirikiana na Clinton
Development Initiative (CDI) iliyoko Mkoa wa Iringa na HELVETAS ya
Singida.
Alisema katika Mkoa wa Singida wanafanya kazi katika
Halmashauri nne ambazo ni Ikungi, Iramba, Mkalama na Singida.
Alisema katika tukio la leo wamepanga kupanda miche ya miti
3,000 katika msitu wa Munkhola na kugawa kwa wananchi wanaouzunguka msitu huo miche ya miti
2,000 na kuwa lengo la mwaka huu nikupanda miti 2,466,300 iliyozalishwa na washirika na
wakulima wa Wilaya ya Singida kwa
ujumla.