Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini na Katibu wa
CCM Kata ya Mandewa Yusuph Kijanga Makera akihutubia mahafali ya 13 ya Shule ya
Sekondari Mandewa iliyopo Manispaa ya Singida kwa niaba ya mbunge jana.
ya wageni mashuhuri waliohudhuria mahafali hayo wakiongozwa na Yusuph Makera
Kijanga (wa tatu kulia) wakijiandaa kukata keki ya mahafali, zoezi lililokwenda
sambamba na harambee fupi iliyolenga kukusanya kiasi cha fedha kwa ajili ya
kufanikisha mahafali hayo.
wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye sherehe hizo.
wakiimba wimbo maalumu.
Wazazi wa wahitimu na wananchi wengine wakifuatilia hotuba
ya Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Ramadhan Sima iliyosomwa na
mwakilishi wake ‘Kijanga.’
wageni walioketi meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye sherehe hizo.
na wahitimu wakifurahi.
zikiendelea.
zikiendelea.
ya walimu wa Shule ya Sekondari Mandewa wakiwa kwenye sherehe hizo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Mandewa, Georgia Maghiya akicheza
na kufurahi wakati wa mahafali hayo.
wakifuatilia burudani mbalimbali kwenye mahafali hayo.
wa miradi ya majengo mbalimbali ya vyumba vya madarasa ambayo baadhi
imekamilika na mingine kuwa katika hatua za mwisho za kupaua ambayo fedha yake
ilitolewa na Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.
wa miradi ya majengo mbalimbali ya vyumba vya madarasa ambayo baadhi
imekamilika na mingine kuwa katika hatua za mwisho za kupaua ambayo fedha yake
ilitolewa na Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.
wa miradi ya majengo mbalimbali ya vyumba vya madarasa ambayo baadhi
imekamilika na mingine kuwa katika hatua za mwisho za kupaua ambayo fedha yake
ilitolewa na Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.
wa miradi ya majengo mbalimbali ya vyumba vya madarasa ambayo baadhi
imekamilika na mingine kuwa katika hatua za mwisho za kupaua ambayo fedha yake
ilitolewa na Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.
Na Godwin Myovela, Singida
MBUNGE wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima ameishukuru
serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa msukumo wa kipekee katika
utekelezaji wa miradi ya miundombinu mbalimbali ya elimu inayolenga kuinua tija
na ustawi kwa ukuaji wa sekta ya elimu ndani ya jimbo lake.
Aidha, Mbunge huyo pamoja na mambo mengine, amekabidhi vifaa
vya Tehama kwa shule ya Sekondari Mandewa ikiwa ni mwendelezo wa jitihada zake
za kuinua taaluma na viwango vya ufaulu ndani ya shule zote zilizopo ndani ya
Jimbo la Singida Mjini kwa minajiri ya kuchagiza kasi ya ufaulu na uwajibikaji.
Akizungumza kwenye Mahafali ya 13 ya Kidato cha Nne ya Shule
ya Sekondari Mandewa iliyopo ndani ya Manispaa ya Singida mkoani hapa jana,
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mandewa Yusuph Kijanga Makera kwa
niaba ya Mbunge huyo alisema muda mfupi ujao miradi hiyo inakwenda kupanua wigo
wa fursa kwa watoto na vijana kujipatia elimu stahiki kwenye nyanja za mazingira
rafiki.
“Tunaendelea kumshukuru Rais na chama chetu kwa mapenzi
makubwa kwa wananchi wa mkoa wa Singida katika jitihada za wazi za utekelezaji
wa maelekezo ya Ilani ya CCM kwa vitendo. Mpaka sasa zaidi ya majengo ya
miundombinu mbalimbali ya kujifunzia takribani 42 ndani ya jimbo hili yapo
kwenye hatua za mwisho za kukamilika,” alisema Makera kwa niaba ya Mbunge.
Akihutubia mamia ya wazazi na wananchi waliohudhuria
mahafali hayo Makera alisema dhamira ya serikali ni kuhakikisha hatua kwa hatua
inakwenda kupunguza changamoto nyingine zote zilizosalia kwenye sekta ya elimu,
afya, maji, nishati, kilimo na nyinginezo, ili kujenga ustawi na tija kwa
uwiano wa matokeo chanya katika muktadha wa kuinua kipato kwa mwananchi mmoja
mmoja na taifa.
Kwa niaba ya Mbunge Sima, aliwasihi wakazi wa Singida Mjini,
hususan wazazi wanaozunguka Kata ya Mandewa kuendelea kuchapa kazi, kuwa
wazalendo, kumuunga mkono Rais Samia kwa majukumu mazito aliyoanza nayo kwa
kasi na mafanikio makubwa ndani ya kipindi kifupi, na zaidi kukiamini Chama Cha
Mapinduzi ambacho ndio taswira na mwelekeo katika mageuzi yaliyopo ya kiuchumi.
Aidha, Makera aliwataka wahitimu wapatao 163 wa shule hiyo
kujikita katika kudumisha nidhamu, maadili, uzalendo na kuwaheshimu wazazi
katika kipindi hiki wanapokuwa nje ya mikono ya walimu wao kama nyenzo ya
kuwawezesha kuvuka salama dhidi ya vishawishi na makundi maovu ya mitaani
vinavyoweza kuhatarisha maono ya ndoto zao katika kufikia mafanikio.
Kwa upande wake, Mkuu wa Shule hiyo Georgia Maghiya, alisema
mpaka sasa tayari serikali imewakabidhi kwa nyakati tofauti jumla ya shilingi
milioni 173-fedha za EP4R na Uviko 19 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na matundu ya choo na baadhi ya miradi hiyo ipo
mbioni kukamilika huku mingine ikiwa tayari imeanza kutoa huduma kwa walengwa.
Hata hivyo pamoja na kushukuru serikali na Mbunge kwa
jitihada zinazoelekezwa kwa shule hiyo-ikiwemo ugawaji wa vifaa hivyo vya
Tehama, Maghiya alimuomba Mbunge kuangalia uwezekano wa kumaliza changamoto ya
ukosefu wa jengo la utawala ambalo huwafanya walimu wa shule ya Mandewa mpaka
sasa kutumia darasa kama ofisi kwa shughuli za uwajibikaji.
“Tuna ukosefu huo wa jengo la utawala, maktaba, upungufu wa
nyumba za walimu, upungufu wa fedha za ujenzi wa bweni kiasi cha shilingi milioni
hamsini, pia hatuna hostel kwani wanafunzi wengi wanatembea umbali mrefu wa
takribani kilometa 10 kutoka maeneo ya Mwaja, Uhamaka, Ititi na maeneo mengine
hadi kufika eneo la shule…hali hii huwalazimu baadhi ya wazazi kuwapangishia vyumba
watoto jambo ambalo linahatarisha maisha hasa kwa watoto wa kike,” alisema
Maghiya.