Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ,George Simbachawene amewasili katika Kijiji cha Mlunduzi, Kata ya Mlunduzi, Jimboni kwake Kibakwe na kupokelewa na Viongozi wa Kata, Viongozi wa Kijiji na Viongozi wa Chama wa ngazi zote wa kata hizo pamoja na walimu na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mlunduzi wa jimbo hilo. Ameanza Ziara ya Kikazi jimboni kwake tarehe 30/11/2021. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri Simbachawene akizungumza na Wananchi wake wa Kijiji cha Chaludewa, Kijiji cha Mlunduzi na Kijiji cha Chinyang’huku vilivvyopo Jimboni kwake alipowatembelea kwenye Ziara ya Kikazi tarehe 30/11/2021. Amewaomba kushirikiana na serikali ya Mtaa na ya Kijiji kuhakikisha kwamba wanaangalia usalama ili kudhibiti uhalifu pamoja na kutunza mazingira yanayowazunguka. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri Simbachawene akikagua Majengo ya Shule ya Msingi Chaludewa iliyopo Kijiji cha Chaludewa, Kata ya Mlunduzi , jimboni kwake ikiwa ni moja ya Ziara yake ya Kikazi jimboni na kuahidi kutoa mifuko mia moja (100) ya cement ili kujenga upya madarasa yaliyo haribiwa na upepo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Baadhi ya wananchi wa jimbo la Kibakwe wakiwa kwenye mkutano na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene alipowatembelewa kwenye Ziara ya Kikazi jimboni kwake Kibakwe, tarehe 29/11/2021. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.