Kamanda wa Polisi Mkoani Tabora ACP Richard Abwao
……………………………………..
Na Lucas Raphael,Tabora
Kufuatia mvua inayoendelea kunyesha mkoanu Tabora imesababisha watu watatu familia moja kufariki Dunia baada ya kupingwa na Radi ndani ya nyumba yao katika maeneo ya Ikundika kitongoji cha Mkuyuni kijiji cha Limbulasiasa kata ya Uganga wilaya ya Kaliua mkoa Tabora.
Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani Tabota Richard Abwao alisema kwamba tukio hilo,lilitokea Novemba 25 mwaka huu amajara ya saa 9.30 alasiri na kusabisha vifo vya watu hao.
Aliwataja waliokufa kuwa ni mtoto mdogo mwenye umri wa mwaka moja aliyefahamika kwa jina la Raphael John (1),Mbisi Maziku (28) na John Matelemki (40).
Alisema alisema kwamba Radi hiyo ilipopinga iliunguza nyumba ambayo marehemu hao wakiwa ndani .
Kamanda huyo wa polisi alitoa taadhari kwa wananchi wa mkoa wa Tabora hasa kipindi cha mvua za masika kuchukua taadhari ya mvua hizo ambazo kwa sasa zinambatana na Radi na upepo mkali.