WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Ummy Mwalimu,aakizungumza na washiriki wakati wa kufunga maonyesho ya akitoka Wiki ya Asasi za Kirai (AZAKI) yaliyomalizika leo Oktoba 28,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Ummy Mwalimu,(hayupo pichani) wakati wa kufunga maonyesho ya akitoka Wiki ya Asasi za Kirai (AZAKI) yaliyomalizika leo Oktoba 28,2021 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Ummy Mwalimu,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunga maonyesho ya akitoka Wiki ya Asasi za Kirai (AZAKI) yaliyomalizika leo Oktoba 28,2021 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Ummy Mwalimu,akitoka mara baada ya kufunga Wiki ya Asasi za Kirai (AZAKI) zilizomaliza leo Oktoba 28,2021 jijini Dodoma.
………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Ummy Mwalimu,amefunga maonyesho ya Wiki ya Asasi za Kirai (AZAKI) jijini Dodoma huku akiwapongeza wadau kwa kuendelea kushirikiana na Serikali.
Akizngumza leo Oktoba 28,2021 jijini Dodoma Waziri Ummy amesema kuwa wataendelea kutoa ushirikiano kwa mshirika hayo na kuyasihi kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi ikiwa ni moja ya mchango mkubwa wa maendeleo ya nchi.
“Kwa kutambua mchango wa Azaki natoa wito kwenu kuendelea kushirikiana na Serikali kuendelea kuihudumia jamii ambayo Asasi hizi mmekuwa mkifanya
kazi nizuri kwa kuifikia jamii hasa wananchi walioko vijijini kwa kushirikiana na Serikali za Vijiji na halmashauri” Amesema Mhe. Ummy
Aidha ametoa wito kwa Sekta Binafsi kuwekeza kwenye
mashirika ya Asasi za Kiraia ili kuchangia ukuaji wa maendeleo ya jamii na
Taifa kwa ujumla na kwamba kwa kufanya hivyo kutaisaidia Sekta Binafsi kutimiza malengo yao ya huduma za jamii kwani
asasi hizo zimekuwa zikifanyakazi na jamii hizo kwenye maeneo yao.
Pia amezitaka Asasi za Kiraia kuongeza nguvu katika suala
zima la kutoa elimu kwa wananchi na kuwajengea uwezo ili wananchi hao waweze
kujisimamia katika shughuli zao za kimaendeleo na kiuchumi huku akiwataka
kuwasaidia madiwani kwenye halmashauri kwa kuwajengea uwezo kwenye masuala mbalimbali
yakiwemo usimamizi wa fedha na miradi ya maendeleo.
“Napenda kuwapongeza sana kwa elimu mnayotoa kwa wananchi
kwa kuwajengea uwezo, lakini naomba muende mbali zaidi kuyafikia mabaraza ya
madiwani kwenye halmauri zetu ili nao wajengewe uwezo wa kusimamia halmashauri
kwenye matumizi ya fedha na ufuatiliaji wa shughuli za maendeleo” Ameongeza Mhe. Ummy.
Awali mratibu wa Wiki ya Azaki
na Mshauri wa Foundation for Civil Society (FCS) Justice Rutenge ameeleza kazi
zilizofanywa katika wiki ya Azaki ikiwa ni pamoja na mijadala mbalimbali
iliyowakutanisha wadau wa Asasi za Kiraia, Wabunge, Makundi Maaalum na wananchi
ambapo kwa pamoja waliweza kushirikiana katika mazungumzo na mijadala
iliyolenga kujadili
masuala yanayohusu ustawi wa nchi na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
“Mheshimiwa Waziri Wiki ya Azaki mwaka huu imeweza
kuzikutanisha Asasi zaidiya 300 ambao kwapamoja waliweza kukutana hapa Dodoma
kuanzia siku ya ufunguzi na baadae kushiriki kwenye mijadala mbalimbali
iliyowawezesha kutoa mawazo yao juu ya masuala mbalimbali ya ustawi wa jamii na
Taifa kwa ujumla” Amesema Justice.
Wiki ya AZAKI ni jukwaa pekee nchini lililowaleta kwa pamoja
wadau wakuu wa maendeleo ikiwemo Serikali, Sekta Binafsi na Asasi za
Kiraia, pamoja na wananchi kwa lengo la kujadili masuala yanayohusu
ustawi wa nchi na maendeleo ya Taifa.