Mkuu wa Sayansi na Mhandisi Dkt.Tabu Kondo akifungua  Mafunzo ya TEHAMA kwa walimu wa Shule za Msingi na Sekondari yaliyoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) wenye  lengo la kufikisha elimu yaliyofanyika  leo oktoba 25, 2021 jijini Dodoma

AFISA na Mratibu Tehama kutoka TAMISEMI,Mwl. Mratibu Abed, akizungumza wakati wa mafunzo ya TEHAMA kwa walimu wa Shule za Msingi na Sekondari  yaliyoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) yenye  lengo la kufikisha elimu kwa walimu wengine yaliyofanyika leo oktoba 25, 2021 jijini Dodoma

Kaimu Mtendaji  Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) John Mkondya,akizungumza wakati wa mafunzo ya TEHAMA kwa walimu wa Shule za Msingi na Sekondari yaliyoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) wenye  lengo la kufikisha elimu uliofanyika  leo oktoba 25, 2021 jijini Dodoma.

Baadhi ya washiri wa Mkutano wakifatilia hotuba mbalimbali wakati wa mafunzo ya TEHAMA kwa walimu wa Shule za Msingi na Sekonadri nchini yaliyoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) wenye  lengo la kufikisha elimu kwa walimu wengine yaliyofanyika  leo oktoba 25, 2021 jijini Dodoma

……………………………………………………….

Na Eric Mungele,Dodoma

AFISA na Mratibu Tehama kutoka TAMISEMI,Mwl. Mratibu Abed, amewataka walimu wa Shule za Msingi na Sekondari wanaopata mafunzo ya Tehama kufanya kwa vitendo na kwa waledi ili waweze kwenda kusaidia wanafunzi mashuleni.

Hayo ameyasema leo oktoba 25, 2021 jijini Dodoma wakati wa Mkutano wa mafunzo ya TEHAMA yaliyoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) kwa lengo la kufikisha elimu kwa walimu wengine kwa Sule za Sekondari na Msingi nchini.

Mwl Abed amewataka walimu kufanya mafunzo kwa umakini wa hali ya juu kwa vitendo ili waweze kufikisha elimu sahihi  kwa wanafunzi ambao wataenda kuwafundisha na kuwa watatoka na kitu.

Aidha amewataka kuwa wavumiliu kwa changamoto zitakazojitokea kwa kipindi chote cha mafunzo pia kwa wale wasio na vifaa vya Tehama watasaidiwa kuweza kupata.

“Mafunzo haya ninyeti inawabidi kufanya mafunzo hayo kwa umakini wa hali ya juu kwa vitendo ili muweze kuelewa na kuwafkishia wanafunzi na walimu ambao mmewawakilisha”amesema Mwl Abed

“lakini pia kwa vikwanzo au changamoto yoyote mtakazo kutana nazo  itawabidi kuwa wavumilivu lakni pia kwa wale ambao bado hawajapata vifaa vya Tehama tutawasaidia kuweza kupata,”amesema

Kwa upande wa walimu kutoka shule ya sekondari ya Wasichana Tabora,Daudi Njele , amesema wanatumani wanatweza kufanya vizuri mafunzo haya nawataweza kufanya kwa vitendo na umakini ili kufikisha elimu dhabiti kwa wanafunzi na walimu walio wawakilisha.

Aidha ameishukuru  UCSAF kwa kuandaa mafunzo hayo kwa wiki nzima maana inaenda kuwasaidia wao pamoja na wanafunzi kutokana na mfumo wa Dunia ya sayansi na teknolojia inavyohitaji

”Tunaishukuru UCSAF kwa kuanda mafunzo haya maana yataenda kutusaidi sisi pamoja na wanafunzi kutokana na mfumo wa Dunia ya sanyansi na teknolohia inavyohitaji,”amesema