………………………………………………………………
Na Silvia Mchuruza,Kagera.
Kamishina Mkuu wa TRA Mr. Alphayo Kidata amewataka wafanyabiashara pamoja na wananchi wote wa Mkoa wa Kagera kulipa kodi kwa hiari.
Kauli hiyo ameitoa wakatia akizungumza na wafanyabiashara Kagera katika Mkutano wenye lengo la kutatua Kero zinazowakabili.
Hata hivyo ametoa pole kwa wafanyabiashara kwa upande wamifumo kuwa na matatizo kidogo kipindi cha nyuma lakini sasa kila kitu kimerekebishwa.
“Natoa pole zangu kwenu ndugu zangu kwa usumbufu uliokuwepo kipindi cha nyuma lakini sasa kila kitu kimerekebishwa na TRA inachoitaji ni napata ya serikali yakusanywe kwa ufanisi mkubwa”
Pia amewataka wafanyabiashara kutunza kumbukumbu zao ili kuweza kuwasaidia maafisa ukadilia kodi sahihi.
Aidha amewataka wafanyabiashara kuwa na matumizi sahihi ya mashine za EFD maana inaokoa mapato ya serikal.
Sambamba na hayo nao wafanyabiashara Wameiomba TRA kutoa elimu ya kutosha kwa mlipa kodi Ili kuepuka usumbufu unaojitokeza.
Vile vile wafanyabiashara hao Wameiomba mamlaka ya mapato nchini TRA kupunguza VAT kwa upande wao Kwani inawarudisha nyuma katika mapato Yao