Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzaibar Mhe. Rahma Kassim Ali,akiwasili katika Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea Ofisi hizo zilizopo jijini Dodoma.

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzaibar Mhe. Rahma Kassim Ali,akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) zilizopo jijini Dodoma.

Naibu Katibu mkuu Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk. Jim Yonazi,akitoa Salama za Wizara kwa Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzaibar Mhe. Rahma Kassim Ali,alipotembelea Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) jijini Dodoma.

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzaibar Mhe. Rahma Kassim Ali,akizungumza na watendaji wa  Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea Ofisi hizo zilizopo jijini Dodoma.

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzaibar Mhe. Rahma Kassim Ali,akimsikiliza Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew wakati wa ziara yake ya kutembelea Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF)  zilizopo jijini Dodoma.

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzaibar Mhe. Rahma Kassim Ali,akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote(UCSAF), Justina Mashiba,wakati akiwasilisha Utekelezaji wa Miradi mbalimbali inayofanywa na UCSAF Visiwani Zanzibar baada ya Waziri huyo kufanya ziara  ya kutembelea Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF)  zilizopo jijini Dodoma.

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzaibar Mhe. Rahma Kassim Ali,akikabidhiwa Zawadi na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote(UCSAF), Justina Mashiba, baada ya kufanya ziara  ya kutembelea Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF)  zilizopo jijini Dodoma.

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzaibar Mhe. Rahma Kassim Ali,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kuongea na watendaji wa  UCSAF baada ya kufanya ziara  ya kutembelea Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF)  zilizopo jijini Dodoma.

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzaibar Mhe. Rahma Kassim Ali,akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi wa Ujenzi Mhandisi Valentino Chaffu mara baada ya kukagua ujenzi wa Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)  inayojengwa eneo la Njedengwa jijini Dodoma.

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzaibar Mhe. Rahma Kassim Ali,akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote(UCSAF), Justina Mashiba, baada ya kukagua ujenzi wa Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) inayojengwa eneo la Njedengwa jijini Dodoma.

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzaibar Mhe. Rahma Kassim Ali,akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) inayojengwa eneo la Njedengwa jijini Dodoma.

Muonekano wa Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) inayojengwa eneo la Njedengwa jijini Dodoma.

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzaibar Mhe. Rahma Kassim Ali,akiwa katika picha ya pamoja mara  baada ya kukagua ujenzi wa Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) inayojengwa eneo la Njedengwa jijini Dodoma.

………………………………………………………………

Na.Alex Sonna,Dodoma 
WAZIRI wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Rahma Kassim Ali ametoa wito kwa mfuko wa Mawasiliano kwa wote nchini(UCSAF) kuhakikisha  watu wenye ulemavu wanapewa kipaumbele kwenye mafunzo ya Tehama ili waweze kunufaika na huduma hiyo . 
Kauli hiyo ameitoa jijini Dodoma alipofanya ziara ya kutembelea  ofisi za UCSAF Mhe.Rahma Kassim Ali amesema kuwa huduma za mawasiliano hazipaswi kuwaacha nyuma watu wenye ulemavu kwani nao wanahaki ya kunufaika na huduma hizo.
“Tunapoenda mbele zaidi Katika Mawasiliano hatupaswi kuwaacha wenzetu hawa watu wenye Ulemavu kwani wakipatiwa  mafunzo watakuwa na uelewa zaidi”amesema Waziri Rahma.
Hata hivyo ameiongeza UCSAF kwa kuendeleza miradi mbalimbali visiwani Zanzibar huku akiahidi kuwa Serikali chini ya Rais Dkt.Hussein Mwinyi kuwa itaendelea kutoa ushirikiano kwa mfuko huo ili waweze kuwafikishia wananchi huduma iliyo bora.
Aidha Waziri Rahma amesema kuwa Katika  kisiwa cha Pemba wananchi wake bado wana changamoto ya mawasiliano hivyo wanapaswa kutatuliwa kero zao.
“Kwa kweli pamoja na kazi nzuri mnayoifanya ya kuwafikishia huduma wananchi bado wengi wao visiwani Pemba bado mawasiliano hayajawa naamini mtasambaza mawasiliano kwa wote kama inavyosomeka kuwa ni  mfuko wa Mawasiliano”amesema 
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew,amemshukuru Waziri huyo kwa kufanya ziara katika Ofisi za UCSAF hivyo watatoa ushirikiano mkubwa kwa upande wa Zanzibar ili wananchi waweze kupata huduma ya mawasiliano.
Awali Mtendaji mkuu wa Mfuko wa mawasiliano kwa wote UCSAF Bi. Justina Mashiba ameelezea utekelezaji wa Miradi inayotekelezwa visiwani Zanzibar ili wananchi waweze kufikiwa na  huduma ya mawasiliano.
“Sisi kama UCSAF nia yetu ni kuhakikisha huduma ya mawasiliano inapatikana kote,na lengo ni kila  sehemu kuwe na Mawasiliano  katika visiwa vyote vilivyopo Zanzibar” amesema Mashiba.
Katika hatua nyingine Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Rahma Kassim Ali,ameridhwa na ujenzi wa Ofisi ya UCSAF inayojengwa katika eneo la Njedengwa.
”Kabisa nawapongeza UCSAF kwa ujenzi wa ofisi hii na mmeniambia kuwa ujenzi huo unatarajia kukamilika Disemba mwaka huo hivyo nawaomba Wasimamizi wa ujenzi huo mfanye kazi usiku na mchana ili muweze kukamilisha ujenzi huu kwa wakati na katika ubora wa majengo unavyotakiwa na Serikali”
Mradi wa ujenzi wa ofisi mpya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote unagharimu kiasi cha shilingi bilioni  2 ambapo hadi sasa umefikia asilimia 65  ukiwa unatarajiwa kukamilika mwezi Disemba mwaka huu na jumla ya Tsh.milioni 900 zikiwa zimeshatumika .