Home Mchanganyiko NAIBU KATIBU MKUU WA UN ATUA DODOMA

NAIBU KATIBU MKUU WA UN ATUA DODOMA

0

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Mhe. Amina Mohammed amewasili Nchini kwa ziara ya siku mbili kuwasilisha ujumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe. Antonio Guteres kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Mhe. Amina Mohammed amepokelewa katika uwanja wa ndege wa Dodoma na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb).