Mbunge wa Jimbo la Kibaha mji Silvestry Koka wa kushoto akikabidhi madawati kwa baadhi ya shule hizo zilizopo katika Jimbo lake.
**************************
NA VICTOR MASANGU,KIBAHA.
Mbuge wa Jimbo la Kibaha mji Silvestry Koka katika kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya elimu ameamua kuchangia madawati yapatayo 120 kwa shule za msingi na sekondari.
Koka amekabidhi msaada huo wa madawati na viti kwa shule tatu za sekondari na moja shule ya msingi muungano ambayo ilipatwa na janga la kuungua na Moto hivi karibuni.
Mbunge huyo ambaye katika ziara hiyo ambayo iliweza kugusa zaidi katika sekta ya elimu aliambatana na wajumbe wa mfuko wa Jimbo pamoja na baadhi ya viongozi wa idara za elimu kutoka halmashauri ya mji Kibaha.
Katika ziara hiyo Mbunge huyo Alisema kuwa lengo lakek kubwa kwa Sasa ni kuweka mikakati kabambe kwa ajili ya kuzisaidia shule za msingi na sekondari zilizopo pembozoni ili nazo ziweze kufanya vizuri.
“Kwa upande wangu mm Kama Mbunge wa Jimbo la Kibaha mji kipaumbele changu kikubwa kwa Sasa nitatumia fedha za mfuko wa Jimbo Kama asilimia 70 kwa lengo la kuboresha elimu,”Alisema Koka.
Aidha alifafanua kwamba lengo la serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha inaboresha zaidi mazingira rafik kwa wanafunzi pamoja na walimu ili kuleta mabadiliko zaidi katika kuongeza kiwango Cha elimu.
Pia alisema anatambua bado kuna baadhi ya shule katika Jimbo lake zinakabiliwa na changamoto mbali mbali hivyo atajitahidi kwa Hali na mali kuzisikiliza na kuzitafutia ufumbuzi kwa kushirikiana na serikali na wadau wadau wa maendeleo.
Aliongeza kuwa ana Imani mchango wa madawati hayo pamoja na viti vitawasaidia wanafunzi kwa kiasi kikubwa kusoma katika mazingira mazuri ukilinganisha na siku za hapo nyuma.
Katika hatua nyingine aliwakumbusha wanafunzi kuhakikisha wanasoma kwa bidiiii na kusikiliza Yale yote ambayo yanafundishwa na walimu wao.
Mbunge huyo kupitia ziara hiyo aliwaahidi walimu na wanafunzi kuendelea kutatua changamoto za uhaba wa matundu ya vyoo pamoja na upungufu wa madarasa na nyumba za walimu.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mkuza Fokasi Bundala alimpongeza Mbunge huyo kwa juhudi ambazo anazifanya kwa kuboresha sekta ya elimu kupitia fedha za mfuko wa Jimbo.
Nao baadhi ya wanafunzi na walimu ambao shule zao zimeweza kunufaika na msaada huo wamesema kwamba madawati hayo yatatakuwa no mkombozi mkubwa katika suala zima la kuindokana na kusoma kwa mlundikano mkubwa.
Katika ziara ya jumla ya madawati yapatayo 120 yamekabidhiwa kwa shule ya Sekondari nyumbu,Simbani,Mbwawa pamoja na shule ya msingi Muungano kwa kiasi Cha shilingi milioni 78 fedha kutoka mfuko wa Jimbo.