Na Mwamvua Mwinyi,Miono
WAKAZI wa Kijiji cha Machala Kata ya Miono, Halmashauri ya Chalinze wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wametakiwa kupuuza uzushi unaosambazwa mitandaoni na baadhi ya watu kuhusiana na chanjo ya CORONA, kuwa ina madhara.
Aidha wametakiwa kuungana mkono juhudi za rais Samia Suluhu alizozianzisha kuhusiana na chanjo ya ugonjwa huo hatari, huku rais akiongoza zoezi hilo mpango unaoendelea katika mikoa mbalimbali, huku serikali ikisisitiza kuwa ni zoezi la hiyari.
Hayo yamebainishwa na Mjasiriamali Maarufu wilayani hapa Teddy Davis, alipozungumza kwenye mahafali ya shule ya msingi ya Machala iliyopo kijiji cha Machala, akiwa mgeni rasmi ambapo alisema wayapuuze maneni yanayozungumzwa mitandaoni.
“Nitumie fursa hii kuwakumbusha kwamba hivi sasa dunia inaangaika kupambana na ugonjwa hatari wa CORONA, niwaombe wa-Tanzania wenzangu tuungane na rais wetu Samia Suluhu aliyeonesha kuguswa na janga hilo,” alisema Mlezi huyo.
Katika kupambana na hali hiyo Teddy ameahidi kuwashoneshea barakoa wanafunzi wote pamoja na walimu ikiwa ni kuungana na juhudi za serikali katika mapambano hayo, huku akiahidi kupunguza changamoto zinazoikabili shule ikiwemo uchache wa matundu ya vyoo.
Taarifa ya Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Gao Rodgers imeelezea mafanikio kadhaa pamoja na changamoto ya upungufu wa vyumba vitatu vya madarasa, ofisi ya walimu sanjali na matundu ya vyoo.
Taarifa ya wahitimu hao 13 iliyohudhuliwa na viongozi mbalimbali ni
Mahafali ya tisa tangu kuanzishwa mwaka 2007 ambayo imeelezea mafanikio na changamoto kadhaa huku ikisisitiza upatikanaji wa vyumba vipya vitatu vya madarasa, matundu ya vyoo na ofisi ya walimu.