Home Mchanganyiko MHE.MSIGWA AWAONGOZA WAANDISHI WA HABARI KUPATA CHANJO YA UVIKO-19 LEO JIJINI DAR...

MHE.MSIGWA AWAONGOZA WAANDISHI WA HABARI KUPATA CHANJO YA UVIKO-19 LEO JIJINI DAR ES SALAAM

0

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali,Mhe. Gerson Msigwa akipata chanjo ya Uviko -19    leo Jijini Dar es Salaam.

Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali hapa nchini wakipata chanjo ya Uviko -19    leo Jijini Dar es Salaam.

**************************

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali,Mhe. Gerson Msigwa, amewaongoza wanahabari kupata Chanjo ya Uviko -19, Baada ya Mkutano wake na wanahabari hao uliofanyika Leo Agosti 1, 2021, Idara ya Habari-Maelezo, Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya zozi hilo lililofanyika leo jijini Da es Salaam Mhe.Msigwa amesema zoezi la chanjo litaanza kutolewa hapo kesho ambapo kuna Vituo kama 550 vilivyoandaliwa.

“Chanjo hizi hazijaleta madhara kwa waliotumia kama tulivyokuwa tunasikia na chanjo hizi zitaendelea kuletwa baada ya zile dozi milioni 1 kuna nyingine zitaendelea kuletwa”. Amesema Mhe.Msigwa 

Aidha Mhe.Msigwa amesema kuna upotoshaji unaoenezwa mitandaoni hivyo amewataka Waandishi kuonesha weledi na kutokujiingiiza kwenye huo upotoshaji wa kuwatisha Watanzania.

“Serikali imeamua chanjo iwe hiari sasa tusiwashinikize Watanzania wakahiari kutokuchanja tuwaache wenyewe waamue”. Amesema.