Home Teknolojia WANAFUNZI WANAOPENDA KUWA NA TAALUMA YA FORODHA NA KODI WASHAURIWA KUJIUNGA NA...

WANAFUNZI WANAOPENDA KUWA NA TAALUMA YA FORODHA NA KODI WASHAURIWA KUJIUNGA NA CHUO CHA KODI

0

Maafisa wa Chuo cha Kodi (ITA) Edwin Matemanga na Sylvia Kaungamno wakizungumza na wanafunzi waliotembelea banda la Chuo cha Kodi katika maonesho ya vyuo vikuu nchini yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo vikuu Tanzania (TCU) yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Maafisa Chuo cha Kodi (ITA) Edwin Matemanga na Sylvia Kaungamno wakizungumza na waananchi waliotembelea banda la Chuo cha Kodi katika maonesho ya vyuo vikuu nchini yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo vikuu  Tanzania (TCU) yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Afisa Chuo cha Kodi (ITA) Edwin Matemanga akizungumza na Mwananchi aliyetembelea banda la Chuo Cha Kodi katika maonesho ya vyuo vikuu nchini yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo vikuu Tanzania (TCU) yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakipata maelezo kutoka kwa  Maafisa wa Chuo cha Kodi (ITA) walipotembelea banda la  Chuo cha Kodi katika maonesho ya vyuo vikuu nchini yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo vikuu Tanzania (TCU) yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
CHUO cha Kodi (ITA) kimewashauri wanafunzi wanaopenda kupata taaluma ya Forodha na Kodi kujiunga na Chuo hicho ambacho kimebobea katika kutoa taaluma hiyo.
Akizumgumza wakati wa Maonesho ya 16 ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Afisa Mkuu Uhusiano wa Umma Oliver Njunwa amesema kuwa ITA ndio Chuo pekee ndani ya Tanzania, Afrika Mashariki na Kusini ambacho kina ithbati ya kutoa Mafunzo ya Forodha na Kodi kwa takribani miaka 14.
“Tunawakaribisha vijana, wazazi na wananchi wote kutembelea Banda letu hapa Mnazi Mmoja ili kupata maelezo ya kozi ambazo Chuo cha Kodi kinatoa pamoja na kuwasaidia kutuma maombi.” Amesema Bi. Njunwa.
Taaluma ya Forodha na Kodi ni taaluma ambayo inahitajika sana wakati huu ambapo Tanzania inaendelea kukuza mapato ya ndani ili kupunguza utegemezi hivyo vijana wanaohitimu katika ITA watakuwa msaada zaidi kujakikisha hili linafanikiwa.
Tukiwa hapa Mnazi Mmoja katika kipindi cha maonesho haya tutawasaidia wote wanaotembelea Banda Letu kichagua kozi inayowafaa kutokana na sifa walizo nazo na kama hawana sifa za kujiunga na ITA tunawaelekeza katika vyuo vingine.
Kwa wale wanaodhani kwamba ukisoma ITA lazima ufanye kazi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwamba fursa nyingine za kufanya kazi ambazo mhitimu wa ITA anazipata.
Anaweza kujiari mwenyewe kwa kufungua kampuni yake ya ushauri wa masuala ya Kodi na akaajiri wengine, anaweza kuajiriwa katika taasisi za serikali, kwenye makampuni binafsi na hata katika mashirika yasiyokuwa ya serikali (NGOs).
“Kwa hiyo tukiwa hapa tunawaelezea wanafunzi fursa zilizopo baada ya kuhitmu kwani kwa kuwa ITA ni sehemu ya TRA wengi wanaodhani lazima ufanye kazi TRA baada ya kuhitmu.
Kwa sasa Chuo cha Kodi kinatoa masomo Usimamizi wa Forodha na Kodi ngazi ya Astashahada, Stashahada na Shahada.
Pia kinatoa Stashada ya Uzamili katika Kodi na kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo cha Muenster cha Ujerumani wanatoa Shahada ya Uzamili katika Sheria ya Kodi na Usimamizi.