Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya sanaa wa Wizara Ya Habari, Utamduni Sanaa na Michezo
***************************

Adeladius Makwega Chamwino- WHUSM

Serikali imewapongeza wadau wote wanaoandaa matamasha mbalimbali  ya sanaa na utamaduni kwani kwa kukufanya hivyo kunakuza kulinda  na kurithisha utamaduni wa Mtanzania.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamdauni , Sanaa na Michezo Mheshimiwa Innocent Bashungwa alipowakilishwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa  Bi. Leah Kihimbi  katika kufunga  Tamasha la Cigogo  Chamwino Mkoani Dodoma.

Amesema kuwa  Wizara itaweka mikakati thabiti kuhakiksha Tamasha la Cigogo linakuwa kubwa kama matamasha makubwa mengine yanayofahamika Kitaifa na Kimataifa.

Waziri Bashungwa  amewaagiza wataalamu wa wizara yake  kuhakikisha maombi ya Mkurugenzi wa Kituo cha Sanaa Chamwino na  yale ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka yanatekelezwa kwa haraka na tamasha lijalo liwe  kubwa na la mfano.

Awali kabla ya kuhitimisha tamasha hilo Mkurugenzi wa Kituo cha Sanaa Chamwino Dkt Kedmon Mapana aliomba Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo kusaidia kufanikisha Tamasha la Cigogo la 13 kwa mwaka 2022.

 Tamasha hilo lilipambwa na wasanii kuimba nyimbo zenye maudhui ya aina mbalimbali lakini kubwa  kuliko yote  ni nyimbo za Uviko 19 kutia fola.
                                                       
                                                        Korona hauna huruma,
Mbona utumaliza,
Mbona unatutesa,
Amani haipo tena,
 Korona korona ehh
        Kazi nyingi zimesimama
Uchumi umeshuka
                                                       Tatizo ni korona
Bado unatusumbua.

“Ni kweli tulijitahidi kuhakikisha ugonjwa huu wa Uviko 19 unaeleweka kwa hadhira yetu ambayo kwa muda wa siku mbili ilikuwa ikitega masikio na kukodolea macho yao  kwenye  ngoma zetu za kitamaduni kama huo wimbo ulioimbwa na Kikundi cha Nyota Njema Chamwino.” Amesisitiza Dkt Kedmon Mapana.

Tamasha hilo la Cigogo limetamatishwa kwa  wasanii kuonyesha sanaa zao za maonesho ikiwemo ngoma za makabila mbalimbali.