Home Biashara TBL PLC YAADHIMISHA SIKU YA WAKULIMA WA SHAHIRI KWA MIKAKATI YA...

TBL PLC YAADHIMISHA SIKU YA WAKULIMA WA SHAHIRI KWA MIKAKATI YA KUFANIKISHA KILIMO CHA KISASA NCHINI

0

Mkuu wa wilaya ya Karatu,Abbas Kayanda (katikati waliokaa) akiwa katika  picha ya pamoja na Maofisa wa kampuni ya TBL Plc wakati wa maadhimisho ya Siku ya wakulima wa Shahiri iliyofanyika wilayani humo

 Baadhi ya wakulima wa shahiri wakifuatilia matukio wakati wa maadhimisho hayo

***************************

Kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL Plc) na wadau wengine waliungana na wakulima  wa Shahiri na mazao mengine wilayani Karatu mkoani Arusha kuadhimisha siku   ya Wakulima wa Shahiri.

 TBL kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kila mwaka  huadhimisha Siku ya Wakulima inaoshirikiana nao, ambapo huweza kukutana nao kwa ajili ya kujua changamoto zinazowakabili pia huwakutanisha na wataalamu wa kilimo na  sekta nyingine ambazo zinachangia kubadilisha maisha ya wakulima kuwa bora.

Kauli mbiu ya Siku hii mwaka huu ilikuwa ‘Wakulima wapatiwe Ujuzi ,Waunganishwe na wadau wa kufanikisha kazi yao na kuwapatia uwezeshaji wa kifedha’ ambayo na malengo endelevu ya kampuni mama ya  ABInBEV ya  kuinua wakulima wanaouzia malighafi viwanda vyake vlivyopo sehemu mbalimbali duniani.

Mkurugenzi Mtendaji wa TBL,Bw.Jose Moran, alisema “Wakulima wadogo ni wadau wetu muhimu katika manunuzi yetu ya malighafi. kwani tunaamini katika kukuza mnyororo thabiti, endelevu na jumuishi”.

Alisema TBL Plc, imedhamiria kufanikisha Malengo Endelevu ifikapo 2025, lengo mojawapo likiwa kufanikisha kilimo cha kisasa. Katika kilimo kampuni imedhamiria  kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2025 asilimia 100% ya wakulima wadogo inaoshirikiana wanapatiwa ujuzi, wanaunganishwa na wadau muhimu kufanikisha kazi yao na wanawezeshwa kifedha.

Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Abas Kayanda, alisema, “Kuboresha sekta ya kilimo nchini Tanzania, na uzalishaji wa shayiri, ni kipaumbele cha serikali. Matukio maadhimisho kama Siku ya Wakulima hutoa fursa ya kujenga uhusiano muhimu, kuwapatia wakulim aujuzi kutoka kwa wataalam,kutambua fursa  na  changamoto zinazowakabili”

Wakulima waliohudhuria  siku hiyo walipata fursa ya  mbinu za kilimo cha kisasa  na kukutana na wadau mbalimbali wa tasnia ya kilimo. Maadhimisho haya ya kila mwaka yamekuwa sehemu muhimu  katika kalenda ya kilimo nchini .