Home Biashara CRDB YAPONGEZA KASI YA USHIRIKISHWAJI MABORESHO YA MITAALA YA ELIMU

CRDB YAPONGEZA KASI YA USHIRIKISHWAJI MABORESHO YA MITAALA YA ELIMU

0

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza na Wanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida,Wanachuo wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Singida na VETA wakati akifungua Kongamano la “Career Fair Day” lililofanyika katika Ukumbi wa Msonge TIA  Singida lililoandaliwa na Benki la CRDB. 

 

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Benki ya CRDB, Siaophoro Kishimbo   akizungumza kwenye kongamano hilo.

 

Meneja wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania  (TIA) Kampasi ya Singida Dkt.James Mrema akizungumza kwenye kongamano hilo.

Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Rasilimali Watu wa benki hiyo Godfrey Rutasingwa akitoa mada kwenye kongamano hilo.

Meneja Mafunzo na Uendelezaji wa benki hiyo, Edith Mwiyombela akizungumza na wanafunzi hao.

 

Wimbo wa Taifa ukiimbwa.

 

 

Wimbo wa Taifa ukiimbwa.

 

 

Wimbo wa Taifa ukiimbwa.

 

 

Wimbo wa Taifa ukiimbwa.

 

 

Kongamano likiendelea.

 

 

Kongamano likiendelea.

 

 

Afisa Masoko wa benki hiyo Oscar Zangira (katikati) akiwa kwenye kongamano hilo.

 

 

Kongamano likiendelea.

 

Rais wa Serikali ya Wanafunzi (TIASO) wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania  (TIA) Kampasi ya Singida, Hamisi Ibrahim akizungumza kwenye kongamano hilo.

Wafanyakazi wa Benki ya CRDB  wakipiga makofi kwenye kongamano hilo.

Meneja wa Kanda ya Kati wa benki hiyo Chabu Mishwaro akitoa salamu kwa kuwapungia mikono wanafunzi hao kwenye kongamano hilo.

Meneja wa benki hiyo Mkoa wa Singida Innocent Arbogast akizungumza kwenye kongamano hilo.

 

Kongamano likiendelea.

 

Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Singida Ally Mwendo akizungumza kwenye kongamano hilo.

 

Picha zikipigwa kwenye kongamano hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge akizungumza na viongozi wa Benki ya CRDB baada ya kufungua kongamano hilo.

 

Burudani zikifanyika katika Kongamano hilo.
Wanafunzi wakiwa kwenye kongamano hilo.

 

 

 

Meneja Rasilimali Watu wa benki hiyo Kanda ya Kati, Kevin James (kushoto) 

 

  akiongoza kucheza kwaito kwenye kongamano hilo.

 

 

 

 

Wanafunzi wakiwa kwenye kongamano hilo.

 

Kongamano likiendelea.

 

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Benki ya CRDB, Siaophoro Kishimbo akizungumza na wanafunzi hao.

 

Kongamano likiendelea.

Kongamano likiendelea.

 

 

Na Dotto Mwaibale, Singida

 

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Binilith Mahenge ameomba Taasisi za Fedha ikiwemo Benki ya CRDB mbali ya kuwasaidia waajiriwa watarajiwa namna ya kulipokea soko la ajira ameomba vijana waliopo vyuo mbalimbali hapa nchini wasiachwe kupewa mafunzo ya namna ya kushiriki kikamilifu kwenye ajenda ya kujenga uchumi wa Tanzania.

Dk. Mahenge alitoa kauli hiyo leo kwenye Kongamano la ‘CRDB Carrier Fair Day’  lililofanyika  kwenye ukumbi wa Taasisi ya Uhasibu nchini TIA Kampasi ya Singida kwa kushirikisha Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) na VETA.

Alisema dhana ya waajiri na waajiriwa katika mwelekeo chanya wa mafunzo hayo vinapaswa kufungamanishwa na Tanzania kwenye kuwezesha vijana wake kuwa na elimu ya kutosha na weledi katika kujenga uchumi imara.

“Hatima ya nchi yetu ipo mikononi mwa vijana hivyo ni lazima tufanye tathmini ya kutosha na kuongeza kasi ya kuwaandaa kabla ya kuingia kwenye soko,” alisema Mahenge.

Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Rasilimali Watu kutoka makao makuu ya benki hiyo, Godfrey Rutasingwa, alisema benki hiyo imeridhishwa na kasi ya maboresho yanayoendelea kufanywa na serikali kupitia sekta ya elimu hususani kwenye eneo la ushirikishaji waajiri katika muktadha wa maandalizi ya mitaala kwa kuzingatia mahitaji ya soko.

“Kuna maboresho makubwa kwa sasa, na hii imechangiwa na namna sekta ya elimu inavyoshirikisha waajiri ambao ndio wapo kwenye soko, tunapewa fursa ya kutoa maoni kwenye ufundishaji wao na muundo wa mitaala yao, na hii imesaidia kujikuta ikitoa mafunzo yanayohusiana na ajira zilizopo kwenye soko” alisema Rutasingwa.

Alisema CRDB inapokea wanafunzi waliopo masomoni takribani 500 kila mwaka kwa nafasi za mafunzo ya vitendo hatua ambayo imechagiza ubora wa kipekee katika kuwawezesha kukidhi haja ya soko la ajira kulingana na dunia ya sasa.

Mkurugenzi Rasilimali Watu CRDB, Siaophoro Kishimbo, alisema kwa sasa benki hiyo  imeanza rasmi kupanua wigo wake kwa kuwaelekeza wanavyuo hususani vyuo vya kati ambao ni miongoni mwa waajiriwa watarajiwa namna bora ya kujiandaa kuwa waajiriwa, wafanyabishara na wateja wa benki hiyo sasa na baadaye.

Alisema wametoa kipaumbele kikubwa kwenye kada ya vyuo vya kati kulingana na umuhimu wake katika uzalishaji wa ujuzi stahiki ambao huwasaidia wao kama waajiri kupata nguvu kazi jambo ambalo wengi hawalipi msukumo.

“Kupitia kongamano hili hapa TIA singida na vyuo vingine tutawafundisha namna gani waajiri wanategemea waajiriwa wawe, namna ya kupata fedha, kutunza fedha, kuzizoea fedha, na tutaendesha kasi ya mahojiano ya papo kwa papo ili kupima juzi zao kuwapima na kuandaa utayari kabla ya wao kuwa waajiriwa,” alisema Kishimbo.

Kwa upande wake Meneja TIA Kampasi ya Singida, Dk. James Mrema alisema kongamano hilo limewasaidia kukutana na waajiri hao, kubadilishana uzoefu, ujuzi, mbinu na mikakati na zaidi kupata mrejesho wa mazao wanayozalisha katika soko.