Home Mchanganyiko RIANS WOMEN EMPOWERMENT CENTER YAJA NA MKAKATI WA KUSAIDIA MABINTI WA KIKE

RIANS WOMEN EMPOWERMENT CENTER YAJA NA MKAKATI WA KUSAIDIA MABINTI WA KIKE

0

Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Ilemela Sitta Singibala akipokea maelekezo juu ya shughuli za mikono zinazofanywa na wanafunzi wanaonufaika na mafunzo kutoka kituo cha kata ya Bugogwa kutoka kwa Mkurugenzi wa Asasi ya Rians Bi Esther Adhiambo 

Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa Manispaa ya Ilemela Ndugu Sitta Singibala akikata utepe kuashiria ufunguzi wa mradi wa kuwawezesha mabinti kiuchumi kata ya Bugogwa wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza 

Mkurugenzi wa asasi ya Rians akisoma taarifa ya mradi kwa mgeni rasmi ambae ni afisa maendeleo wa manispaa ya Ilemela Ndugu Sitta Singibala (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuwawezesha mabinti kujikwamua kiuchumi

Mabinti walionufaika na mafunzo kutoka kwa asasi ya Rians wakiwa na vitendea kazi vyao Picha Na.4161 Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa Manispaa ya Ilemela Ndugu Sitta Singibala akikata utepe kuashiria ufunguzi wa mradi wa kuwawezesha mabinti kiuchumi kata ya Bugogwa wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza

…………………………………………………………………………

Asasi ya kijamii ya Rians Women Empowerment center inayojishughulisha na harakati za kumwezesha mtoto wa kike aliyeachwa na mfumo rasmi wa elimu na kubaki mtaani bila kufahamu afanye nini ili aweze kujikwamua kimaisha imezindua mpango wa kusaidia mabinti katika wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza kwa kuwapa ujuzi na stadi mbalimbali zitakazowasaidia kujikwamua kiuchumi na kujiajiri.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa mafunzo ya kuwawezesha mabinti wilaya ya Ilemela, kata ya Bugogwa, Bi Esther Adhiambo amesema kuwa mradi huo ulianza rasmi Mei 05, 2021 ukiwa na wanafunzi 43 na kauli mbiu yake ikiwa ni Tembea Nami, Nionyeshe Njia, Niache Nipae ukihusisha kata tatu za Kirumba, Ilemela na Bugogwa huku ukitegemewa kuzifikia kata zote 19 za manispaa ya Ilemela

‘.. Tumeanza na kata tatu, Lakini baadae tutazifikia kata zote kumi na tisa kuhakikisha mabinti walioachwa na mfumo rasmi wanapata mafunzo yatakayowasaidia kimaendeleo …’ Alisema

Aidha ameongeza kuwa mafunzo yanayotolewa na asasi hiyo ni ya ushonaji,upakaji wa rangi za nyumba, uandishi wa mabango,  ususi na urembo, upambaji wa kumbi za sherehe, mapishi ya keki, uchoraji wa kucha, rangi, umeme, ujasiriamali, usafi wa miguu na mikono yenye lengo la kuchochea kujiajiri ili kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana

Kwa upande wake afisa maendeleo ya jamii wa manispaa ya Ilemela Ndugu Sitta Singibala mbali na kuishukuru taasisi hiyo kwa uamuzi wake wa kuanzisha mradi huo utakaosaidia vijana walio ndani ya manispaa yake, Amewaasa vijana kujitokeza kwa wingi na kuitumia vizuri fursa hiyo huku akiahidi kushirikiana na vijana wote watakopata mafunzo kwa kuhakikisha wanajiunga katika vikundi na kuomba mitaji kupitia mikopo inayotolewa na halmashauri

Nae mratibu wa mafunzo hayo kwa kata ya Bugogwa Bi Dorice Asheri Isaya akafafanua kuwa mpaka sasa wanafunzi 68 wameshanufaika na mafunzo huku akitaja changamoto ya kuongezeka kwa idadi ya wahitaji wakiwemo wenye jinsia ya kiume tofauti na lengo lililokuwa limewekwa hapo awali la kuwawezesha wasichana pekee na kwa idadi kusudiwa, Sambamba na kuwashukuru viongozi wa mitaa, kata na wilaya hiyo kwa ushirikiano wanaoutoa katika kufanikisha mradi huo.

Nae moja ya mwanafunzi aliyenufaika na mafunzo hayo, Sarifa James Chamba ameshukuru kwa mafunzo aliyoyapata huku akiahidi kutumia vyema fursa hiyo katika kujikwamua kiuchumi na kujiendeleza kimaisha.