Home Biashara WATEJA WA TECNO CAMON 17 KUZAWADIWA FRIDGE NA ELIZABETH MICHAEL.

WATEJA WA TECNO CAMON 17 KUZAWADIWA FRIDGE NA ELIZABETH MICHAEL.

0

NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.

Ule msimu wa mazawadi unaendelea Kampuni ya simu za mkononi TECNO inawataka wateja wote wa simu za TECNO kuendelea Tembelea maduka yao kwa kipindi hiki cha promosheni ya TWENDE ZETU
CAMPING KISTAA.

TECNO leo imefanya maandalizi ya kuwazawadia wateja wa TECNO Camon 17 zawadi mbalimbali kama vile ticket ya kutembelea mbuga za Wanyama Tanzania, Fridge, Kinga’amuzi cha DSTV,
Drones na zawadi hizi kukabidhiwa kesho na wasanii maarufu kutoka kiwanda cha filamu Elizabeth Michael, Tina na Kibibi wa watamthilia ya Huba.

Manager Mauzo Bi, Mariam Hussein amesema kuwa “bado tuna zawadi nyingi sana tunawakaribisha wateja wa TECNO ambao bado hawajafika madukani kwetu kufika leo na kesho mapema kabla ya utowaji wa zawadi https://user.tecno.com/tz/camon17series-activity?uid=359&type=2#/ ., TECNO kuwazawadia wateja wa TECNO Camon 17 kati ya zawadi hizi” na kuzitaja kama nilivyoziorodhesha hapo juu.

Amesema kuwa Camon 17 ni toleo jipya la series ya TECNO Camon ambayo uwekezaji wake mkubwa upo kwenye Camera. TECNO Camon 17pro inasifika kwa kupiga picha zenye rangi halisi na kurecord filamu kwa teknolojia ya black and white mode.

TECNO Camon 17 inayawezesha haya na selfie camera yenye MP48 na teknolojia ya 4k video resolution pamoja na camera ya nyuma yenye MP64 na teknolijia ya black and white mode.

TECNO Camon 17 inapatikana katika maduka yote ya simu nchini Tanzania na ofa ya GB78 za Tigo kwa
mwaka mzima.