Home Mchanganyiko SERIKALI YAWASILISHA MAKADIRIO YA BAJETI KUU YA SERIKALI YA MWAKA 2021/2022

SERIKALI YAWASILISHA MAKADIRIO YA BAJETI KUU YA SERIKALI YA MWAKA 2021/2022

0

 

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba, akionesha Mkoba wenye Hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022,  Bungeni jijini Dodoma, Juni 10, 2021.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba, akitoa Hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 kwenye mkoba kabla ya kusoma hotuba hiyo,  Bungeni jijini Dodoma, Juni 10, 2021. 

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba, akisoma Hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022,  Bungeni jijini Dodoma, Juni 10, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

…………………………………………………………………………………….

Na.Alex Sonna,Dodoma

SERIKALI imewasilisha Bungeni Makadirio ya Bajeti kuu ya Serikali ya mwaka 2021/2022 huku ikianisha Maeneo ya vipaumbele kwa Mwaka huo wa Fedha.

Akiwasilisha Makadirio hay oleo June10 Mwaka2021 Waziri wa Fedha na Mipango,Dk.Mwigulu Nchemba amesema kuwa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2021/22  ni ya kwanza katika utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26 wenye dhima ya  “Kujenga Uchumi Shindani na Viwanda kwa Maendeleo ya  Watu”. Bajeti hii itajielekeza katika utekelezaji wa vipaumbele  mbalimbali.

“Vipaumbele vilivyoainishwa katika maeneo matano  ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22,Maeneo hayo ni  Kuchochea uchumi shindani na shirikishi; kuimarisha uwezo wa  uzalishaji viwandani na utoaji huduma ili kuongeza thamani ya  mazao ya kilimo; kukuza uwekezaji na biashara; kuchochea  maendeleo ya watu; na kuendeleza rasilimali watu. 

Waziri Mwigulu ameeleza kuwa  ili kuwa na uchumi shindani na  shirikishi, Serikali itajielekeza katika kugharamia miradi ambayo  itajikita katika: Kujenga jamii yenye uwezo wa kushindana kikanda  na kimataifa; kusimamia utulivu wa viashiria vya uchumi  kwa ujumla. 

Amefafanua kuwa kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji,kuchochea uvumbuzi na uhawilishaji wa teknolojia kutoka nje  na kuendeleza  miundombinu na huduma za reli, barabara za kufungua fursa za  kiuchumi, kuunganisha nchi jirani, kupunguza msongamano mijini  na barabara za vijijini, madaraja, usafiri wa majini na angani,  mageuzi ya TEHAMA pamoja na kutekeleza mradi wa Tanzania ya  Kidijitali, nishati, bandari na viwanja vya ndege. Eneo hili  limetengewa jumla ya shilingi trilioni 7.44 ikijumuisha shilingi trilioni  3.13 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kielelezo. 

Pamoja na mambo mengine ameitaja  miradi mingine ya kielelezo  itakayotekelezwa ni: Kuboresha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL);  Makaa ya Mawe – Mchuchuma na Chuma – Liganga ikijumuisha  ujenzi wa reli ya kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge Railway)  kutoka Mtwara hadi Mbamba Bay na matawi ya Mchuchuma na  Liganga; Bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga  (Tanzania); Mradi wa Kuchakata Gesi Asilia kuwa Kimiminika (LNG)  – Lindi; Mradi wa Kufua Umeme wa Maji – Ruhudji MW 358.

“ Mradi wa Kufua Umeme wa Maji – Rumakali MW 222; Uchimbaji wa  madini ya Nickel; Ujenzi wa Madaraja Makubwa na Barabara za Juu  za Daraja la Kigongo – Busisi (Mwanza), Tanzanite (Dar es Salaam)  na Interchange ya Kamata (Dar es Salaam); Bandari ya Uvuvi  (Mbegani) na Ununuzi wa Meli za Uvuvi; Kiwanda cha Sukari  Mkulazi; Utafutaji wa mafuta katika vitalu vya Eyasi Wembere na 

Mnazi Bay North; Mradi wa Magadi Soda – Engaruka; Kuongeza Rasilimali Watu yenye Ujuzi Adimu na Maalumu (Ujuzi wa Kati na  Wabobezi) kwa Maendeleo ya Viwanda na Ustawi wa Jamii; na  kuendeleza Kanda Maalumu za Kiuchumi. “,Amesema

Amesema kuwa  katika eneo la kuimarisha uwezo wa  uzalishaji viwandani na utoaji huduma, msukumo utawekwa kwenye  miradi ya viwanda inayolenga kuongeza thamani ya mazao ya  kilimo, mifugo na uvuvi. Katika eneo hili, kipaumbele ni pamoja na:  Kujenga na kukarabati miundombinu ya umwagiliaji na uhifadhi wa  mazao ya kilimo; kuimarisha vituo vya utafiti na huduma za ugani; 

kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi;  kuhakikisha upatikanaji wa masoko ya ndani na nje ya nchi;  kuboresha huduma za uhimilishaji mifugo; na kujenga machinjio ya  kisasa na minada ya mifugo. 

Mheshimiwa Spika, Serikali itaweka mkazo kwenye ujenzi  wa viwanda vya kuongeza thamani ya madini pamoja na kuzalisha  bidhaa zitakazotumia malighafi na rasilimali zinazopatikana nchini. Aidha, Bajeti hii itajielekeza katika kugharamia miradi na programu inayolenga kuboresha huduma za utalii, fedha na bima pamoja na kuendeleza viwanda vya uzalishaji wa dawa muhimu na vifaa tiba. Jumla ya shilingi trilioni 1.38 zimetengwa kugharamia utekelezaji wa  miradi katika eneo hili. 

Mheshimiwa Spika, katika eneo la kukuza uwekezaji na  biashara, Serikali itagharamia programu zitakazoimarisha masoko ya  ndani na kutumia fursa za masoko ya kikanda na kimataifa katika  kukuza biashara. Masoko yanayolengwa ni yale yatakayotoa fursa  kwa bidhaa zinazozalishwa nchini, ikiwemo bidhaa zitokanazo na  mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na misitu. Vilevile, Serikali 

itaendelea kuboresha mazingira ya kufanya biashara na uwekezaji  ikiwemo kuendelea kutekeleza Mpango wa Kuboresha Biashara na  Uwekezaji (Blueprint). Eneo hili limetengewa jumla ya shilingi bilioni  31.6.

Dk. Nchemba amebainisha kuwa katika  kuchochea maendeleo ya watu, miradi itakayotekelezwa italenga kuboresha maisha ya watu kwa kuimarisha upatikanaji wa huduma za jamii ikiwemo elimu na  mafunzo kwa ujumla, afya na ustawi wa jamii, huduma za maji na  usafi wa mazingira na kinga ya jamii ikijumuisha Mpango wa  Kunusuru Kaya Maskini kupitia TASAF. Aidha, Serikali itaendelea kupanga, kupima na kumilikisha ardhi mijini na vijijini, kusimamia  na kuendeleza rasilimali za maji; na kuendelea na utekelezaji wa  programu za kulinda mazingira na kuhimili mabadiliko ya tabianchi.  Jumla ya shilingi trilioni 4.43 zimetengwa. 

 katika jitihada za kuendeleza rasilimali  watu, Serikali itagharamia programu inayolenga kuendeleza maarifa  na ujuzi wa rasimali watu katika ngazi zote za elimu ikiwemo  kuweka mazingira wezeshi kwa vijana kujiajiri.

Pia amesema Serikali itaendelea kuboresha viwango vya utoaji wa elimu ya ufundi na  mafunzo ya ufundi stadi pamoja na ujuzi adimu kwa lengo la  kuongeza tija na ushindani wa wananchi katika kutumia rasimali  zilizopo nchini ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii ambapo Jumla ya shilingi bilioni 50.5 zimetengwa. 

Amesema  Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22 imeainisha kwa kina  maeneo ya kipaumbele ambayo Serikali itayatekeleza kupitia Bajeti  ya mwaka 2021/22. 

pamoja na miradi ya kielelezo, Serikali  itatekeleza miradi mingine ya uboreshaji wa miundombinu ambayo  itagharamiwa na mikopo yenye masharti nafuu kutoka Benki ya  Dunia. Miradi hiyo ni Mradi wa Kuendeleza Jiji la Dar es Salaam  Awamu ya Pili (DMDP II) wa kukabiliana na mafuriko kwenye Bonde  la Mto Msimbazi utakaogharimu dola za Marekani milioni 120.

 Mradi  huu utahusisha ujenzi wa daraja katika eneo la Jangwani, na upanuzi na ujenzi wa kingo za mto Msimbazi. Mradi wa pili  unahusisha uboreshaji wa barabara za kukuza fursa shirikishi za  kijamii na kiuchumi ambapo Benki ya Dunia itatoa dola za Marekani  milioni 300 na mchango wa Serikali ni dola za Marekani milioni 50.  Mradi huu unalenga kuboresha barabara za vijijini katika maeneo  yenye tija kubwa ya uzalishaji wa mazao ya kilimo.  

katika hatua nyingine, Serikali imeanza  mazungumzo na Benki ya Dunia kupitia dirisha la International Development Association (IDA) kwa ajili ya mradi wa uboreshaji  miundombinu katika Majiji na Miji 45. Utekelezaji wa mradi huu  utaanza katika mzunguko wa 20 (IDA 20) unaotegemewa kuanza  Julai 2022 na utagharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 500. Mradi utahusisha ujenzi wa miundombinu ya msingi ili kuboresha  mazingira ya biashara na uwekezaji kwa lengo la kukuza uchumi wa  miji husika. 

Amesema maeneo mengine muhimu ni pamoja na Maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi Mwaka 2022ambapo  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania inajiandaa kufanya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka  2022 kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu SURA 351.

“Kama  mojawapo ya maandalizi ya utekelezaji wa Sensa ya Mwaka 2022  Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa upande wa Tanzania Bara na Ofisi ya  Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Zanzibar imekamilisha kuandaa Kitabu  cha Mkakati wa Usimamizi na Utekelezaji wa Sensa ya Watu na  Makazi ya Mwaka, 2022. Kitabu hiki kinaainisha namna ya usimamizi  na utekelezaji wa zoezi zima la Sensa, gharama ya kufanya Sensa  pamoja na muundo wa Sensa utakavyokuwa katika ngazi zote za  kiutawala.”,amesema  

Amesema jumla ya shilingi bilioni 328.2  zinatarajiwa kutumika kugharamia sensa ya mwaka 2022 na kwa mara ya kwanza katika historia ya Sensa nchini, Sensa ya Mwaka 2022  itatumia teknolojia ya vishikwambi (tablets) katika utengaji wa  maeneo ya kijiografia na ukusanyaji wa takwimu uwandani.  Matumizi ya teknolojia hii yana manufaa makubwa, hasa katika  kupunguza gharama na muda wa kukusanya na kuchakata takwimu,  hali inayowezesha kutoa matokeo ya Sensa ndani ya muda mfupi. 

Amesema zoezi la Sensa ya Watu na  Makazi ni jukumu la kila mtu, natoa wito kwa kamati zote za Sensa,  Wakuu wa Mikoa na Wilaya zote, Waheshimiwa Wabunge pamoja  na wananchi wote kwa ujumla kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa  kutosha katika maandalizi ya Sensa na wajitokeze wote siku ya  kuhesabu watu. Lengo ni kuhakikisha Watu waliolala nchini usiku  wa kuamkia siku ya Sensa (usiku wa sensa) wanahesabiwa na  kuchukuliwa taarifa zao za kiuchumi, kijamii, mazingira na makazi  wanayoishi na mengine mengi kwa ajili ya kupanga mipango  endelevu ya maendeleo ya wananchi.  

Kuhusu maslahi ya Wafanyakazi Waziri huyo amesema  Serikali inatambua na kuthamini  mchango wa watumishi wa umma na wa sekta binafsi katika kukuza  Pato la Taifa Kwa kutambua hilo, Serikali itachukua hatua  mbalimbali za kuboresha maslahi ya wafanyakazi  kwa Kupunguza kiwango cha chini cha kutoza kodi ya mapato ya ajira (PAYE) kutoka asilimia 9 hadi asilimia 8.

Hatua hii ni  mwendelezo wa juhudi za Serikali za kupunguza mzigo wa  kodi kwa wafanyakazi, ambapo kiwango hicho kimepunguzwa  kutoka asilimia 11 mwaka 2015/16 hadi asilimia 8 itakayoanza  kutekezwa mwaka 2021/22 kwa  Kufuta tozo ya silimia 6 iliyokuwa ikitozwa kwa ajili ya  kulinda thamani ya mkopo wa elimu ya juu (Value Retention  Fee) kwa wanufaika; na Kutenga jumla ya shilingi bilioni 449 kwa ajili ya kuwapandisha  vyeo watumishi 92,619. 

Akielezea kuhusu Maslahi ya Madiwani, Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata amesema kuwsa Madiwani  wanafanya kazi nzuri   za kusimamia shughuli za maendeleo kwenye Kata mbalimbali nchini ambapo wao  ni wabunge wakaazi wa kwenye kata hizo ambao kila siku wako na wananchi  katika kusimamia shughuli za maendeleo.

Hata  hivyo, katika baadhi ya halmashauri madiwani wamekuwa  wakikopwa posho zao, na wengine hufikia hatua ya kupiga magoti  kwa wakurugenzi watendaji ili walipwe, hali hiyo imekuwa ikipunguza  ufanisi katika halmashauri zetu kwa madiwani wengi kufanya  maamuzi yanayopendekezwa na wakurugenzi watendaji hata kama  hayana maslahi kwa Taifa ili waweze kulipwa posho zao.

“ Jambo hili  limeongelewa kwa hisia kali sana na Waheshimiwa Wabunge hapa  bungeni. Waheshimiwa Wabunge na Waheshimiwa Madiwani,  napenda niwaeleze kuwa MAMA YETU amesikia kilio chenu na  alinielekeza mimi pamoja na Waziri wa TAMISEMI kulitafutia ufumbuzi suala hili.”, 

Waziri huyo amependekeza kuanzia mwaka 2021/22, Serikali Kuu ianze kulipa posho za kila mwezi za Waheshimiwa  Madiwani moja kwa moja tena kwenye akaunti zao kwa  Halmashauri zote zenye uwezo mdogo kimapato. Halmashauri 16 zenye uwezo mkubwa wa kimapato (Daraja A) zitaendelea kutumia mapato yake ya ndani kulipa posho za Madiwani kupitia kwenye  akaunti zao. 

Kwa upande wa Maafisa Tarafa ambao  ni viunganishi muhimu wa ngazi za kata na Wilaya zetu ambapo wengi wao hufanya kazi nzuri sana ya kusimamia utekelezaji wa maelekezo ya Serikali katika  maeneo yao. Kwa kutambua umuhimu wao, Serikali ya CCM  iliwapatia pikipiki viongozi hawa ili waweze kufanya kazi zao vizuri. 

Hata hivyo, wengi wao wanashindwa kugharamia ununuzi wa mafuta na matengenezo ya vitendea kazi hivi na kulazimika  kuwachangisha wananchi na hata wengine kuomba msaada kwa  wadau mbalimbali. Hali hii inapunguza sana ufanisi katika Tarafa zetu. Kupitia hotuba hii, napenda niwajulishe Maafisa Tarafa wote  nchini kuwa MAMA YETU amesikia kilio chenu. Hivyo, napendekeza kuanzia mwaka 2021/22, Serikali Kuu ianze kulipa posho ya shilingi 100,000/= kwa mwezi kwa kila Afisa Tarafa ili waweze kumudu  gharama za mafuta na matengenezo ya pikipiki. 

Waziri Nchemba amesema  Watendaji Kata ndio wasimamizi wa  kazi za sekta zote na ni watendaji wakuu kwenye kata. Wengi wao  wanafanya kazi katika mazingira magumu ili kufanikisha shughuli za  maendeleo katika kata zetu ikiwemo kusimamia ukusanyaji wa  mapato na masuala ya usalama. Idadi kubwa ya watendaji hawa  hutumia mishahara yao kufanya kazi mbalimbali ikiwemo ufutiliaji  wa mapato ya Serikali kwa kukodi pikipiki ili kufanikisha shughuli zilizopo.

“ Kwa ujumla wanafanya kazi nzuri sana ya kusimamia  shughuli za maendeleo kwenye kata zetu. Jambo hili limeongelewa  kwa hisia kali sana na Mheshimiwa Rose Busiga, Mbunge wa Viti  Maalum (Geita), ambaye ni mtendaji wa kata mstaafu na kuungwa  mkono na wabunge wengi hapa bungeni. Waheshimiwa wabunge,  MAMA YETU amesikia kilio hiki na kutuelekeza kulitafutia ufumbuzi  suala hili. Hivyo, napendekeza kuanzia mwaka 2021/22, Serikali  kuanza kulipa posho ya shilingi 100,000/= kwa mwezi kwa kila  Mtendaji Kata kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri yaliyokuwa  yakitumika kulipa madiwani.”amesema 

Kuhusu Madeni ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii amesema  wastaafu walilitumikia Taifa kwa uzalendo, uadilifu na bidii kubwa hivyo hawawezi kuhesabu mafanikio ya nchi  bila kutaja mchango wa wazee hao.

Amefafanua kuwa   Kumekuwepo na changamoto za muda mrefu za ulipaji wa mafao  yao kutokana na ufanisi mdogo wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii katika  kuhudumia wastaafu  ambapo hali hiyo kwenye mifuko imechangia uwepo wa madeni  ambayo mifuko inaidai Serikali na hivyo kusababisha wastaafu wetu  kukosa au kusubiri kwa muda mrefu ili kulipwa mafao yao.

“Jambo  hili pia limejadiliwa kwa hisia kali na Waheshimiwa Wabunge hapa  bungeni. Wazee wetu hawa hupata shida sana, ambapo baadhi yao  hufadhiliwa malazi kwa kulala misikitini na makanisani na wengine  hutegemea wahisani kuhudumia familia zao kinyume na mchango  walioutoa katika ujenzi wa nchi hii. MAMA YETU amesikia kilio cha  wazee hawa na kutuelekeza Wizara ya Fedha na Mipango  kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu kukamilisha zoezi la kitaalamu ili kujua hali halisi ya madeni na namna bora ya kulipa madeni hayo.”, 

Aidha amependekeza kulipa madeni  yanayodaiwa na mifuko kwa kutenga fedha kwenye bajeti na kutumia utaratibu wa kutoa hatifungani maalum isiyo taslimu (Non cash Special Bond) zitakazoiva kwa nyakati tofauti kuanzia miaka  miwili hadi 25.

Amesema Utaratibu wa hatifungani una faida mbalimbali  zikiwemo: kuipa Serikali nafasi ya kibajeti ya kuendelea kutekeleza  miradi mingine ya maendeleo; kuiwezesha Serikali kuyatambua  madeni hayo kwenye kanzidata ya madeni; na kuzuia madeni hayo  kuendelea kuongezeka kulingana na tathmini ya thamani ya madai  (actuarial valuation).

 Aidha, utaratibu huo utaboresha mizania ya  hesabu na mtiririko wa mapato yanayotokana na riba ya hatifungani  hizo kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Hatua hii inakwenda kumaliza  kabisa tatizo hilo la wazee wetu kudai haki yao kwa damu na  machozi yaliyodumu kwa muda mrefu. 

Amesema Serikali imepokea malalamiko kuhusu  kucheleweshwa kwa michango ya watumishi kupelekwa kwenye  mifuko ya hifadhi ya jamii na baadhi ya ofisi za Serikali kutopeleka  kabisa michango hiyo na  Jambo hilo llimekuwa likisababisha usumbufu kwa watumishi punde wanapostaafu.

 Sambamba na hilo amependekeza kulipa  michango hiyo moja kwa moja kutokea Hazina kwa taasisi zote  ambazo watumishi wanalipwa na Hazina. Taasisi ambazo zinalipa  watumishi kutokana na vyanzo vyao vya mapato zitaendelea kupeleka michango ya watumishi wao kwa ufuatiliaji wa karibu wa  Serikali. Serikali itafanya uhakiki na kulipa madeni ya michango  ambayo haijawasilishwa kwenye mifuko hadi sasa. 

Kuhusu jeshi la polisi askari  wapiganaji, kuna utaratibu wa wapiganaji kufanya kazi kwa  mikataba ya muda mfupi kwa miaka 12 kabla hawajapata ajira za  kudumu. Jambo hili huwasababishia wapatapo mkataba wa kudumu  wawe wamechelewa kwa miaka 12 ikilinganishwa na mtumishi  mwingine aliyeingia pamoja kazini katika idara nyingine. Jambo hili  linamadhara hasi katika itifaki ya utumishi na mafao ya mpiganaji 

anapostaafu.

“ Hiki kimekuwa kilio cha muda mrefu cha askari wa  Jeshi la Polisi. Kutokana na changamoto hiyo, MAMA YETU amesikia  kilio cha askari hao na alituelekeza tukae na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ili kutafuta suluhisho la jambo hili. Napendekeza  kuanzia mwaka 2021/22 askari wa Jeshi la Polisi wataingia mkataba wa kipindi cha miaka 6 na kuingia katika ajira ya kudumu.  

Aidha amesema Kurahisisha Kasi ya Utekelezaji wa Miradi katika kuimarisha usimamizi na ufanisi  katika utekelezaji wa bajeti ya Serikali, Wizara ya Fedha na Mipango  itafanya mabadiliko katika Kanuni ya 21 ya Sheria ya Bajeti, SURA 439 ili kuondoa changamoto iliyopo ya fedha ambazo hazijatumika  hadi tarehe 30 Juni kila mwaka kurejeshwa Mfuko Mkuu wa Hazina  ya Serikali.

Amesema Mabadiliko hayo yatatoa fursa kwa Maafisa Masuuli  kuwasilisha taarifa ya fedha kuvuka mwaka hadi tarehe 30 Juni kwa Mlipaji Mkuu wa Serikali badala ya siku 15 kabla ya mwaka wa fedha kumalizika. Fedha hizo zitawekwa kwenye Akaunti ya Amana  kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli ambazo hazijakamilika wakati  wa utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha husika.

Kwa  msingi huo, kuanzia sasa hakutakuwa na fedha zenye miadi  zitakazorejeshwa Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali ifikapo tarehe 30 Juni ya kila mwaka wa fedha isipokuwa pale ambapo Maafisa  Masuuli wamekiuka masharti ya Sheria ya Bajeti, SURA 439 na Sheria ya Fedha za Umma, SURA 348. 

Kuhusu kodi ya Majengo amesema kumekuwa na changamoto kubwa katika  ukusanyaji wa kodi ya majengo, hali iliyosababisha Serikali kubadili  njia za ukusanyaji mara kwa mara. Kabla ya mwaka 2017/18, Serikali za Mitaa zilikuwa na jukumu la kukusanya mapato hayo  lakini hazikufanya vizuri.

Ameeleza kuwa Kuanzia mwaka 2017/18, Serikali ilitumia  Mamlaka ya Mapato kukusanya kodi hiyo, ambapo pia haikufanya  vizuri. Ukusanyaji wa kodi hii kwa kutumia Serikali za Mitaa au TRA umekuwa ukitumia njia za kizamani ambazo zinahusisha watu kusafiri, kupanga foleni na kukusanya fedha taslimu (cash).

 Utaratibu huu unatumia gharama kubwa, muda na ni hatarishi kwa  mapato. Katika kuhakikisha kodi hii inafikia malengo, Serikali  imeandaa utaratibu mzuri wa kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa  kodi ya majengo. 

Kwa upande wa Kodi ya Wajasiliamali,Waziri huyo amesema wafanyabiashara na watoa huduma  wadogo nchini wameendelea kutambulika kupitia vitambulisho vya  wajasiriamali. Tangu kuanza kwa zoezi la utoaji wa vitambulisho vya  wafanyabiashara na watoa huduma wadogo nchini, jumla ya  vitambulisho 2,335,711 vimegawiwa ambavyo vimewezesha  kukusanya jumla ya shilingi bilioni 46.71.

“ Lengo ni kuendelea  kuwatambua wafanyabiashara wadogo na kuwawekea mazingira  rafiki ya ufanyaji biashara. Katika mwaka 2020/21, Serikali imefanya  maboresho ya vitambulisho hivyo kwa kuweka picha na jina la  mjasiriamali ili kuongeza udhibiti na kufungua fursa kwa  wajasiriamali kuweza kutumia vitambulisho hivyo kupata huduma za  kibenki na bima ya afya. Ofisi ya Rais TAMISEMI itaendelea na  uratibu wa kugawa vitambulisho hivi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania ambayo ndiyo yenye mfumo wa kusajili  wafanyabiashara hao, kuchapisha vitambulisho na kuwapatia  Halmashauri husika kwa ajili ya kugawa. “,

Kuhusu Maboresho  ya mfumo wa kodi, ada na tozo mbalimbali amewasilisha  mapendekezo ya kufanya marekebisho ya  mfumo wa kodi, ikiwemo baadhi ya viwango vya kodi, tozo na  ada zinazotozwa chini ya Sheria mbalimbali na kurekebisha taratibu za ukusanyaji na usimamiaji wa mapato ya  Serikali.

 Marekebisho haya yamezingatia dhamira ya Serikali ya  kurejesha ukuaji wa uchumi katika hali ya kawaida baada ya athari  zilizotokana na UVIKO-19 sambamba na kuendelea kuwa na mfumo  wa kodi ambao ni tulivu na wa kutabirika ili kuvutia uwekezaji  kutoka ndani na nje. Vile vile, marekebisho yanalenga kuchochea  kasi ya ukuaji wa uchumi hususan katika sekta ya kilimo na  viwanda, kuongeza kipato kwa waajiriwa na kuongeza  mapato ya Serikali.

 Aidha, Serikali inaendelea kutekeleza Mpango  wa Kuboresha Mazingira ya Kufanya Biashara (BluePrint) kwa  kuwianisha tozo na ada mbalimbali zinazotozwa na Wizara na  Mamlaka za Udhibiti kwa lengo la kupunguza na kurahisisha ulipaji  wake au kuzifuta baadhi ya tozo na ada hizi. Marekebisho  yanayopendekezwa yanahusu Sheria zifuatazo: 

(a) Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, SURA 148; (b) Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 3

(c) Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147(d) Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004; (e) Sheria ya Usimamizi wa Kodi, SURA 438;

(f) Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, SURA 290; (g) Sheria ya Kodi ya Majengo, SURA 289; 

(h) Sheria ya Ardhi, SURA 113; 

(i) Sheria ya Ushuru wa Stempu, SURA 189; 

(j) Sheria ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, SURA 82; (k) Sheria ya Michezo ya Kubahatisha, SURA 41; 

(l) Sheria ya Ukaguzi wa Umma, SURA 418;  

(m) Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada, SURA 134 (n) Sheria ya Usajili wa Magari, SURA 124; 

(o) Sheria ya Usalama Barabarani, SURA 168; 

(p) Sheria ya Raia wa Kigeni (Uratibu wa Ajira) Na. 1 ya mwaka  2015; 

(q) Marekebisho ya Ada na Tozo mbalimbali zinazotozwa na  Wizara, Mikoa Wakala, Mamlaka za Udhibiti na Idara  zinazojitegemea; 

(r) Marekebisho madogo madogo katika baadhi ya Sheria za Kodi na Sheria nyingine mbalimbali; 

(s) Kuendelea na utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha Mazingira  ya Kufanya Biashara (Blueprint) kwa kurekebisha Ada na Tozo  mbalimbali; 

(t) Sheria ya Ushuru wa Barabara na Mafuta, SURA 220; (u) Sheria ya Petroli, SURA 392; na 

(v) Sheria ya Posta na Mawasiliano ya Kielektroniki, SURA 306.

27 

Kwa upande wa Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, SURA 148 amependekeza kufanya marekebisho  kwenye Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, SURA 148 kama  ifuatavyo(i) Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye vyumba vya ubaridi (cold rooms) vinavyotambuliwa kwa H.S Code  9406.10.10 na 9406.9010. Lengo la msamaha huu ni  kuwapunguzia gharama wazalishaji wa mbogamboga na maua  nchini ili kuchochea kilimo cha kisasa,Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye madini  (precious metals) na makinikia yatakayoingizwa nchini kwa ajili  ya kuchenjuliwa, kuongezewa thamani na kuuzwa kwenye  masoko ya madini yanayotambulika nchini. Lengo la pendekezo  hili ni kuviwezesha viwanda vya uchenjuaji vilivyoanzishwa  nchini kupata malighafi ya kutosha kwa ajili ya uchakataji na  hatimaye kuongeza ajira na mapato ya Serikali; 

Mapendekezo mengine ni Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye huduma za  bima ya mifugo ambapo Lengo la marekebisho haya ni kuchochea  shughuli za ufugaji nchini ikiwemo Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye bidhaa na  huduma zitakazoingizwa au kununuliwa hapa nchini kwa ajili ya  kutekeleza mradi wa mafuta ghafi (EACOP).

 Lengo la  marekebisho haya ni kutoa unafuu wa kodi katika utekelezaji  wa miradi tajwa;  

(v) Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye mafuta ghafi  yanayotambulika kwa H.S Code 2709.00.00 kwa lengo la kutoa  unafuu kwa mlaji ikiwemo Kampuni ya uendeshaji wa bomba la  mafuta (EACOP)Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye Nyasi Bandia  zinazotambulika kwa HS Code 5703.30.00 na 5703.20.00 kwa  ajili ya Viwanja vya Mpira vilivyoko kwenye Majiji. Msamaha  huo utahusisha ridhaa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu  Tanzania. Lengo la hatua hii ni kuendeleza michezo na kukuza  vipaji nchini. 

 Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye kadi za  kutengeneza vitambulisho vya taifa zinazotambulika kwa H.S  Code 3921.11.90.00 na malighafi nyingine za kutengeneza kadi  hizo zinazotambulika kwa H.S Code 3921.11.90.00  zitakazoingizwa nchini na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa  (NIDA). Lengo la pendekezo hili ni kupunguza gharama za  kutengeneza Vitambulisho vya Taifa na kuharakisha upatikanaji wake. 

Amesema Kumekwepo na ukiritimba katika kupokea fedha za misaada  kwenye miradi ya maendeleo kwa hitaji la kisheria la kusubiri  idhini ya Baraza la Mawaziri likae ili kuidhinisha misamaha.  Napendekeza Kutoa msamaha wa Kodi ya Ongezeko la  Thamani kwa Taasisi zisizo za kiserikali (NGO’s), kwenye  bidhaa na huduma zitakazotumika kwenye miradi  inayotekelezwa na taasisi husika. Aidha, taasisi zitakazonufaika na msamaha huo ni zile ambazo zina mikataba na Serikali  yenye kipengele kinachotoa msamaha wa Kodi ya Ongezeko la  Thamani.

Pia amesema  Sekta ya mawasiliano imekuwa ikikua vizuri na kuwa kiungo  muhimu cha kuongeza wigo wa wananchi ambao wako kwenye ulimwengu wa kidijitali na kwenye sekta ya fedha (Financial  Inclusion). Napendekeza kusamehe Kodi ya Ongezeko la  Thamani kwenye simu janja za mkononi (smart phones) HS  Code 8517.12.00, vishikwambi (Tablets) HS Code 8471.30.00  au 8517.12.00 na modemu (modems) HS Code 8517.62.00 au  8517.69.00. Lengo la hatua hii ni kuhamasisha matumizi ya huduma za mawasiliano ili kufikia lengo la asilimia 80 ya  watumiaji wa intaneti ifikapo mwaka 2025 kutoka asilimia 46  iliyopo sasa.

Amesema mapendekezo mengine ni Kufuta msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye  mikebe inayotumika kuhifadhia maziwa inayotambuliwa kwa  H.S Code 7310.29.20 ambayo kwa sasa haitumiki kwa ajili ya kazi hiyo na badala yake napendekeza kutoa msamaha wa kodi  ya Ongezeko la Thamani kwenye mikebe ya kubebea maziwa  inayotambulika kwa H.S Code 7310.29.90, 7310.10.00 na 7612.90.90. Lengo la Pendekezo hili ni kuwapunguzia gharama  wazalishaji na kuchochea ukuaji wa sekta ya maziwa nchini; 

‘’Kufuta msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye taa  zinazotumia umeme wa jua zinazotambulika kwa H.S. Code  85.13 na 94.05. Lengo la pendekezo hili ni kuwianisha  msamaha huu sambamba na msamaha unaotolewa chini ya  Sheria ya Ushuru wa Forodha ambayo inasamehe Kodi kwenye vifaa vinavyotumika kuzalisha nishati ya umeme wa jua pekee  na kurahisisha usimamizi wake. Aidha, pendekezo hili linalenga kuweka usawa katika ulipaji kodi kwa watumiaji wa taa zinazotumia nishati za aina zote’’  

Amesema kuwa Kutoza Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa kiwango cha asilimia  sifuri kwenye huduma ya usafirishaji na huduma zinazohusiana  na usafirishaji wa mafuta ghafi kupitia bomba linalojengwa kwa  pamoja baina ya Serikali ya Tanzania na Uganda (EACOP). 

Amesema kuwa Lengo la pendekezo hilo ni kuwezesha huduma tajwa kutekelezwa bila kodi sanjari na uzoefu wa kimataifa kwa  bidhaa zilizopita hapa kwenda nchi jirani au ng’ambo kwa

kuzitambua bidhaa za mtaji zilizomo kwenye Sura ya 84, 85 na  90 ya Kitabu cha Ushuru wa Pamoja wa Forodha wa Afrika  Mashariki kuwa bidhaa za mtaji zitakazostahili kupata kivutio  cha ahirisho la malipo ya VAT.

Amesema kuwa Lengo la pendekezo hilo ni kuwianisha maana ya bidhaa za mtaji kwenye Sheria za kodi na  kuziba mianya ya upotevu wa mapato ya Serikali kwenye Kubadilisha utaratibu wa kutoa msamaha kwenye miradi ya  Serikali inayogharamiwa na fedha za serikali na fedha za  wafadhili ambapo mnufaika wa msamaha huo atawasilisha  maombi kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania  badala ya utaratibu wa kuwasilisha kwa Waziri wa Fedha kwa  ajili ya kupata ridhaa na kutoa Tangazo la Serikali (GN) kwa  kila mradi.

‘’Utaratibu huu utarahisisha na kuharakisha utoaji wa  misamaha badala ya utaratibu wa sasa kutokana na TRA kuwa  na ofisi kwa kila mkoa nchini kote ambazo zinaweza kupokea,  kuchambua na kusimamia matumizi sahihi ya misamaha’’amesema

(Kuhusu Zanzibar, Waziri huyu amependekeza kufanya marekebisho ya Sheria  ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ili kurudisha utaratibu wa  kurejesha VAT kwa bidhaa zinazonunuliwa Tanzania Bara na  kutumika Tanzania Zanzibar. Hii inatokana na mfumo wa  kutoza VAT kwa kiwango cha asilimia sifuri kwa bidhaa za  viwandani pekee kutowanufaisha wafanyabiashara wa Zanzibar  wanaonunua bidhaa na kutozwa VAT Tanzania Bara na  kutozwa tena VAT bidhaa hizo zinapopelekwa Zanzibar.

 Aidha, amependekeza marejesho ya VAT yatakayofanyika kwa bidhaa  zinazotoka Tanzania Bara kwenda Zanzibar yafanyike pia kwa  bidhaa zitakazotoka Zanzibar kwenda Tanzania Bara  sambamba na marekebisho ya vifungu husika vya Sheria za  VAT kwa pande zote mbili za muungano. Ili kuwa na ufanisi wa  marejesho, maboresho ya mifumo yatafanyika ili isomane baina  ya Tanzania Bara na Zanzibar. Kutokana na utaratibu huu,  kiwango cha asilimia sifuri ya Kodi ya Ongezeko la Thamani  kilichokuwa kinatozwa bidhaa hizo kitasitishwa. 

Amesema kuwa kutokana na hatua zote za Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa ujumla  zinatarajiwa kupunguza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 55,499.97.

Kuhusu Sheria ya Kodi ya Mapato,Waziri amependekeza kufanya marekebisho  kwenye Sheria ya Kodi ya Mapato, Kupunguza kiwango cha chini cha kutoza Kodi ya Mapato  yanayohusiana na ajira kutoka asilimia 9 hadi asilimia 8. 

Waziri huyu amesema kuwa jumla ya Mapato Kiwango cha Kodi sasa  

Mapato ya jumla yasiyozidi shilingi  3,240,000/= 

Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi  3,240,000/= lakini hayazidi  

shilingi.6,240,000/=  

Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi  6,240,000/= lakini hayazidi shilingi  9,120,000/=  

Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi  9,120,000/= lakini hayazidi shilingi  12,000,000/= 

Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi  12,000,000/= 

Jedwali Na. 1B Viwango vinavyopendezwa

Mapato ya jumla yasiyozidi shilingi  3,240,000/= 

Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi  3,240,000/= lakini hayazidi shilingi  6,240,000/=  

Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi  6,240,000/= lakini hayazidi shilingi  9,120,000/=  

Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi  9,120,000/= lakini hayazidi shilingi  12,000,000/= 

Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi  12,000,000/= 

Hakuna kodi 

9% ya kiasi kinachozidi shilingi  3,240,000/= 

Shilingi 270,000/= jumlisha 20% ya  kiasi kinachozidi shilingi 6,240,000/= 

Shilingi 846,000/= jumlisha 25% ya  kiasi kinachozidi shilingi 9,120,000/= 

Shilingi 1,566,000/= jumlisha 30% ya  kiasi kinachozidi shilingi  

12,000,000/= 

Hakuna kodi 

8% ya kiasi kinachozidi shilingi  3,240,000/= 

Shilingi 240,000/= jumlisha 20% ya  kiasi kinachozidi shilingi 6,240,000/= 

Shilingi 816,000/= plus 25% ya kiasi  kinachozidi shilingi 9,120,000/= 

Shilingi.1,536,000/= plus 30% ya  kiasi kinachozidi shilingi  

12,000,000/= 

Pia amesema kuwa hatua hiyo inachukuliwa ikiwa ni dhamira ya Serikali ya muda  mrefu kuwapunguzia mzigo wa Kodi wafanyakazi. Hatua hii  inatarajiwa kupunguza mapato kwa shilingi milioni  14,178.06,kwa Kutoa msamaha wa Kodi ya Mapato kwenye hatifungani za  Serikali. Sheria ya Kodi ya Mapato ilisamehe Kodi ya Mapato  kwenye hatifungani kwa mwaka 2002/03 pekee. Lengo la  hatua hii ni kuhakikisha soko la ndani la hatifungani linaendelea kusaidia kugharamia miradi ya Serikali.

Amesema kuwa kumekuwepo na ukiritimba katika kupokea fedha za kutoka  kwa nchi wahisani zinazokwenda kutekeleza Miradi ya  maendeleo. Napendekeza Kurejesha utaratibu wa Mamlaka ya  Waziri mwenye dhamana ya Fedha kutoa msamaha kwa kutoa  tangazo la Serikali (GN) bila sharti la kupata ridhaa ya Baraza  la Mawaziri kwa miradi inayotekelezwa kwa fedha za wafadhili  kupitia mikataba iliyoingiwa baina ya nchi hizo na Serikali yenye kifungu kinachoruhusu msamaha wa kodi ya mapato. 

‘’ Lengo la marekebisho haya ni kuharakisha utekelezaji wa  madi inayofadhiliwa kwa misaada na mikopo yenye gharama  nafuu ambayo utekelezaji wake umekuwa ukichelewa kusubiri  ridhaa ya Baraza la Mawaziri’’

Amesema kuwa Kutoza Kodi ya Zuio kwa kiwango cha asilimia mbili kwenye  malipo yanayohusisha mauzo ya mazao ya kilimo, mifugo na  uvuvi yanapouzwa kwenye kampuni na mashirika yote yanayojihusisha na usindikaji na ununuzi wa mazao,Kwa sasa, Taasisi za Serikali pekee kama vile (Wakala wa Taifa wa Hifadhi  ya Chakula (NFRA) ndizo zinakata kodi hiyo kwa kiwango cha  asilimia mbili.

 Aidha,amesema kuwa pendekezo hilo halitahusisha wakulima  wadogo na wale wanaouza mazao yao kwenye masoko ya  msingi (AMCOS) na kwenye magulio. Lengo la pendekezo hili ni  kuweka usawa katika utozaji wa kodi kwa Kampuni zote zinazojishughulisha na mazao ya Kilimo, mifugo na uvuvi.Pendekezo hilo linatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa  kiasi cha shilingi milioni 43,954.2; 

(v) Kufanya maboresho ya Sheria ya Kodi ya Mapato ili kuwezesha  ukokotoaji wa gharama za uchakavu kwa kiwango maalum cha  asimilia tano (5) kwenye gharama za mali za ujenzi wa bomba  la mafuta (EACOP). Lengo la pendekezo hili ni kuwianisha  gharama za uchakavu na muda wa matumizi wa bomba husika  kwa kuzingatia masharti ya mkataba uliosainiwa baina ya  Serikali za Uganda na Tanzania; 

(vi) Kuweka utaratibu maalum wa utozaji kodi kwa wachimbaji  wadogo wa madini wenye mauzo ghafi yasiyozidi shilingi  milioni 100 kwa mwaka kama ifuatavyo: – 

(a) Kutoza kodi wachimbaji wadogo wa madini kwa kiwango  mfuto cha asilimia 3 kwenye thamani ya mauzo ya madini  pindi yanapopatikana; 

(b) Kuweka muda wa ulipaji kodi kuwa ni wakati wanapouza  madini na kulipa mrabaha kwenye Tume ya Madini au maeneo maalum yaliyoanzishwa chini ya sheria ya madini; 

(c) Kuweka wajibu kwa mchimbaji mdogo wa madini kama  mwajiri wa kukata kodi ya mapato ya ajira kutoka kwa  wafanyakazi wake pale tu madini yatakapokuwa  yamepatikana na kuuzwa katika masoko ya madini; 

(d) Kuweka muda maalum wa kulipa kodi ya zuio ya ajira  kuwa ni wakati mchimbaji mdogo anapouza madini na  kulipa mrabaha katika masoko ya madini au vituo vingine  vya uuzaji na ununuzi wa madini vinayotambuliwa na  Tume ya Madini.

(e) Kuweka kiwango cha kodi cha mapato ya ajira (PAYE) cha  asilimia 0.6 ya thamani ya mauzo ya madini ambayo  italipwa na mwajiri (mchimbaji mdogo wa madini) kwa  niaba ya wafanyakazi wake. 

Amesema kuwa Lengo la mapendekezo hayo ni kurahisisha utozaji na ulipaji wa kodi  kutoka kwa wachimbaji wadogo wa sekta ya madini ili kuongeza  mchango wa kodi ya mapato kutoka kwenye sekta hiyo. Hatua hizi  kwa pamoja zinatarajia kuongeza mapato ya Serikali shillingi 

milioni 29,776.14 

Kwa upande wa Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, amesema kuwa Kwa mujibu wa kifungu cha 124(2) cha  Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, marekebisho ya viwango maalumu vya  ushuru wa bidhaa (specific duty rates) kwa bidhaa zote zisizo za  petroli yanaweza kufanyika kila mwaka ili kuvihuisha na mfumuko  wa bei na viashiria vingine vya uchumi jumla.

 Hata hivyo, kutokana  na biashara za bidhaa hizi kuzorota kutokana na athari za kiuchumi  zilizosababishwa na ugonjwa wa Covid-19, amependekeza  kutofanya mabadiliko ya viwango maalumu vya ushuru wa  bidhaa kwa bidhaa zote zisizo za petroli isipokuwa vinywaji  vikali na bia zitakazotengenezwa kwa kutumia shayiri  iliyozalishwa hapa nchini. 

Amependekeza pia kufanya marekebisho  ya Ushuru wa bidhaa kwenye bidhaa kwa  Kupunguza Ushuru wa Bidhaa kwenye bia zinazotengenezwa  kwa kutumia shayiri iliyozalishwa hapa nchini kutoka shilingi  765 kwa lita za sasa hadi shilingi 620 kwa lita.

Lengo la  mapendekezo hayo ni kuchochea kilimo cha shayiri hapa nchini kwa Kuanza kutoza Ushuru wa bidhaa wa asilimia 10 kwenye nyuzi  na kamba za plastiki (synthetic fibres) zinazoingizwa kutoka nje  ya nchi au kuzalishwa hapa nchini zinazotambuliwa kwa  heading 55.11 na 56.07 isipokuwa zile zinazotumika kwenye 

Uvuvi (HS Code 5607.50.00).

Marekebisho hayo ni  kulinda mazingira na kuchochea uzalishaji na matumizi ya  bidhaa za katani. Hatua hii inatarajiwa kuongeza mapato ya  Serikali kwa shilingi milioni 2,644

(iii) Kuanzisha tozo ya ushuru wa bidhaa kwa kiwango cha asilimia  10 kwenye pikipiki zilizotumika kwa zaidi ya miaka 3  zinazoingizwa nchini zinazotambuliwa kwa HS Code 8711.  Lengo la marekebisho haya ni kudhibiti uingizaji wa pikipiki  chakavu na kulinda mazingira. Hatua hii inatarajiwa kuongeza ya mapato ya Serikali kwa shilingi milioni 263.7. 

Hatua za kutoza Ushuru wa Bidhaa kwenye bidhaa zisizo za petroli  kwa ujumla wake zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa  kiasi cha shilingi milioni 2,907.7. 

Kuhusu Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika  Mashariki ya mwaka 2004 Waziri huyu amesema katika  Kikao cha Mawaziri wa Fedha wa  Jumuiya ya Afrika Mashariki cha Maandalizi ya Bajeti kilichofanyika  tarehe 7 Mei 2021 mjini Arusha, walipendekeza kufanya marekebisho  ya Viwango vya Pamoja vya Ushuru wa Forodha na Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya  Afrika Mashariki (EAC Customs Management Act, 2004) kwa mwaka  wa fedha 2021/22.

Amesema kuwa Mapendekezo hayo yanalenga katika Kuboresha  Maisha ya Watu Kupitia Maendeleo ya Viwanda na Kutengeneza  Ajira kwa ajili ya Ustawi wa Pamoja wa Watu wa Jumuiya ya Afrika  Mashariki.

Amesema kuwa mapendekezo ya Mawaziri wa Fedha ya kufanya marekebisho kwenye Viwango vya Pamoja vya Ushuru wa  Forodha yanahusisha hatua mpya na zinazoendelea ambazo  zimekuwa zikitekelezwa katika Mwaka wa Fedha 2020/21.

 Hatua  hizo ni kama Mapendekezo ya hatua mpya za Viwango vya Ushuru wa  Forodha ni Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi  asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwenye mabasi ya abiria  yanayotambulika kwa HS Codes 8702.10.99 na 8702.20.99  yanayoingizwa nchini kwa ajili ya mradi wa mwendokasi.  Hatua hii inalenga kupunguza gharama za uingizaji wa  mabasi hayo ili kurahisisha usafiri kwa wananchi; 

(b) Kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 10 hadi  asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye nyuzi za pamba  (cotton yarn) zinazotambulika kwa Headings 52.05, 52.06  na 52.07. Lengo la hatua ni kulinda viwanda  vinavyozalisha bidhaa hiyo na kuongeza thamani ya zao la  pamba (value addition) nchini; 

(c) Kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 10 hadi  asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye matairi mapya ya  pikipiki (new pneumatic tyres of rubber) yanayotambulika  kwa HS Code 4011.40.00. Lengo la hatua ni kuongea  mapato ya Serikali kwa kuwa matairi haya ni bidhaa  zilizokamilika kwa ajili ya mtumiaji; 

(d) Kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi  asilimia 35 kwa mwaka mmoja kwenye siagi ya karanga (peanut butter) inayotambulika kwa HS Code 2008.11.00.  Lengo la hatua ni kulinda wazalishaji wa bidhaa hiyo  nchini;

(e) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 10 hadi  asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye nyaya (wire of other  alloy steel) zinazotambulika kwa HS Codes 7229.20.00 na  7229.90.00. Lengo la hatua hii ni kupunguza gharama kwa 

Kuhusu wazalishaji wanaotumia bidhaa hiyo kama malighafi ni Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi  asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye milk cans zinazotambulika kwa HS Codes 7310.10.00 na 7310.29.90.  Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwenye sekta ya  maziwa nchini; 

(g) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 10 hadi  asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye LABSA (Organic  surface-active agents – Anionic) inayotambulika kwa HS  Code 3402.11.00 kwa utaratibu wa duty remission. Lengo  la hatua hii ni kutoa unafuu kwa wazalishaji wa sabuni za  unga na maji nchini; 

(h) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 au 10  hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye malighafi za  kuchakata ngozi zinazotambulika kwa HS Code 3208.20.00  na 3210.00.10 kwa utaratibu wa duty remission. Lengo la  hatua hii ni kutoa unafuu kwa wachakataji wa ngozi  nchini; 

(i) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 au 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye malighafi za  kutengeneza mbolea zinazotambulika kwa HS Codes  2710.99.00, 2528.00.00 na 3505.20.00 kwa utaratibu wa  duty remission. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa  wazalishaji wa mbolea nchini; 

(j) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi  asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio vya 

38 

tumbaku iliyochakatwa vinavyotambulika kwa HS Code  5310.10.00 kwa utaratibu wa duty remission. Lengo la  hatua hii ni kutoa unafuu kwa wachakataji wa tumbaku  nchini; 

(k) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi  asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio vya chai  iliyochakatwa vinavyotambulika kwa HS Codes 4819.20.90,  5407.44.00 na 3923.29.00 kwa utaratibu wa duty  remission. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa  wachakataji wa chai (tea blenders) nchini; 

(l) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwenye malighafi ya  kutengeneza masufuria ya aluminium inayotambulika kwa  HS Code 7606.92.00 kwa utaratibu wa duty remission.  Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa watengenezaji wa  masufuria hayo nchini; 

(m) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi  asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwa waunganishaji wa  pikipiki za matairi matatu bila kujumuisha fremu kwa kuwa  zinatengenezwa hapa nchini (CKD for three-wheel  motorcycles excluding chassis and its components)  zinazotambulika kwa HS Code 8704.21.90 kwa utaratibu  wa duty remission. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa  waunganishaji wa pikipiki hizo nchini ili kurahisisha  usafirishaji wa mizigo; 

(n) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 au 10  hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye malighafi za  kutengeneza mabomba ya plastiki (glass reinforced plastic  pipes) zinazotambulika kwa HS Codes 3920.61.10,  7019.39.00, 7019.31.00, 6006.90.00, 7019.12.00, 

3920.10.10, 4016.93.00, na 3907.91.00 kwa utaratibu wa duty remission.

Amesema kuwa Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa  watengenezaji wa mabomba hayo nchini ili kupunguza  gharama za uzalishaji na kuwezesha ujenzi wa  miundombinu ya maji; na 

(o) Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki  zimekubaliana kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka  asilimia 10 hadi asilimia 0 kwenye mabati (Flat-rolled  products of other alloy steel, of a width of 600mm or  more, not further worked than hot-rolled, in coils)  yanayotambulika kwa HS Code 7225.30.00. Lengo la hatua  hii ni kupunguza gharama kwa wazalishaji wanaotumia  bidhaa hiyo kama malighafi. 

(ii) Mapendekezo ya kuendelea na utekelezaji wa Viwango vya  Ushuru wa Forodha vya mwaka 2020/21 ni kama ifuatavyo: 

(a) Kupunguza Ushuru wa Forodha hadi asilimia 0 kutoka  viwango vya awali vya asilimia 10 na asilimia 25 kwa  mwaka mmoja kwenye malighafi zinazotumika katika  uzalishaji wa vifaa maalum vinavyotumika katika  kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu  (UVIKO-19) vikiwemo Barakoa (Masks), kipukusi 

(sanitizer), mashine za kusaidia kupumua (ventilators),  na mavazi maalum ya kujikinga yanayotumiwa na  madaktari na wahudumu wa afya (PPE). Msamaha huu utatolewa kwa utaratibu wa “duty remission”. Hatua hii  inalenga kutoa unafuu wa uzalishaji wa vifaa hivyo hapa  nchini ili kuongeza kasi katika kupambana na ugonjwa  huo; 

(b) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 10 hadi  asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye mashine za  kielektroniki zinazotumika kukusanya mapato ya Serikali  (Cash registers, Electronic Fiscal Device (EFD) Machines and Point of Sale (POS) machines zinazotambulika katika  HS Code 8470.50.00 na 8470.90.00. Lengo la hatua hii ni  kuhamasisha matumizi ya vifaa hivi katika kuhasibu  mapato ya Serikali; 

(c) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi  asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio  vinavyotumiwa na wazalishaji wa maziwa kwa joto la juu  yanayodumu kwa muda mrefu (UHT Milk) vinavyotambulika kwa HS codes 4819.50.00. Lengo la  hatua hii ni kutoa unafuu kwa wazalishaji wa maziwa  hapa nchini. Utaratibu wa Duty Remission utakaotumika  kutoa unafuu huo; 

(d) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka kiwango cha  asilimia 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye  vifuniko vya chupa za mvinyo (corks and stoppers)  vinavyotambulika kwa HS Codes 4503.10.00 kwa kuzingatia kuwa havizalishwi hapa nchini. Hatua hii  inalenga kuwapunguzia gharama wazalishaji wa mvinyo ili  kuhamasisha na kuendeleza kilimo cha zao la zabibu  nchini pamoja na ajira. Utaratibu wa Duty Remission utakaotumika kutoa unafuu huo; 

(e) Kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi  asilimia 35 kwa mwaka mmoja kwenye bidhaa za  marumaru zinazotambulika kwa HS Code 6907.21.00; 6907.22.00; na 6907.23.00 zinazoingizwa kutoka nje.  Lengo la hatua hii ni kulinda na kukuza viwanda vya  ndani vinavyozalisha marumaru pamoja na kuongeza  ajira;  

(f) Kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi  asilimia 35 kwa mwaka mmoja kwenye chai inayotambulika kwa HS Code 09.02 inayoagizwa kutoka nje. Lengo la pendekezo hilo ni kulinda viwanda vya ndani  na kuhamasisha kilimo cha chai hapa nchini pamoja na  kuongeza ajira katika sekta ya kilimo; 

(g) Kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 35 kwa mwaka mmoja kwenye magunia ya kitani (sacks and bags of jute or other textile bast fibers of  heading 53.03) yanayotambulika kwa HS Code  6305.10.00 yanayoagizwa kutoka nje. Lengo la hatua hii  ni kulinda viwanda vya ndani vinavyotengeneza magunia ya katani, kukuza na kuendeleza kilimo cha zao la  mkonge hapa nchini pamoja na kuongeza ajira na  mapato ya Serikali; 

(h) Kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 0 hadi  asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwenye unga wa kakao  unaoingizwa kutoka nje unaotambulika kwa HS Code  1805.00.00. Lengo ni kuchochea na kuhamasisha kilimo  cha zao la kakao nchini pamoja na kuongeza mapato ya  Serikali; 

(i) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi  asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio vya  kuhifadhia kahawa vinavyotumiwa na viwanda vya  kusaga kahawa nchini. Vifungashio vitakavyohusika ni vile  vinavyotambulika katika HS codes 7310.21.00;  6305.10.00; 3923.50.10; 3923.50.90 na 3920.30.90.  Hatua hii inalenga kuongeza thamani kwenye zao la  kahawa na kuvipa unafuu wa gharama viwanda  vinavyosaga kahawa hapa nchini. Utaratibu wa “Duty  Remission” utatumika katika kuagiza vifungashio hivyo; 

(j) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi  asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio vya  kuhifadhia korosho. Vifungashio vitakavyohusika ni vile 

vinavyotambulika katika HS code 3923.21.00. Hatua hii  inalenga kuongeza thamani kwenye zao la korosho na  kuvipa unafuu wa gharama viwanda vinavyochakata  korosho hapa nchini. Aidha utaratibu wa “Duty  Remission” utatumika katika kuagiza vifungashio hivyo; 

(k) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi  asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio vya  kuhifadhia pamba. Vifungashio vitakavyohusika ni vile vinavyotambulika katika HS codes 3920.30.90;  6305.39.00 na 7217.90.00. Hatua hii inalenga kuvutia  uwekezaji ili kuongeza thamani ya zao la pamba nchini; 

(l) Kupunguza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia  0 kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha  asilimia 25 kwenye malighafi za kutengeneza taulo za  watoto (Baby Diapers) zinazotumbulika kwa HS code  3506.91.00 Hot Melt Adhesive; PE film HS Code  3920.10.90, Empty bag for Baby Diapers HS Code  6305.33.00, Plastic cask HS Code 3926.90.90; na  kiwango cha awali cha asilimia 10 kwenye Super  Absorbent Polymer HS Code 3906.90.00, Wet strength  paper HS Code 4803.00.00, Non-woven HS Code  5603.11.00, Polyethylene laminated Nonwovens HS Code  5903.90.00, Spandex HS Code 5402.44.00 na Dust free  paper HS Code 4803.00.00. Aidha, msamaha huu  utatolewa kwa utaratibu wa “Duty Remission”. Hatua hii  inatarajiwa kutoa unafuu wa gharama za uzalishaji na kuongeza ajira;  

(m) Kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 0  kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha  asilimia 25 kwenye vifaa vinavyotumika katika kukata,  kung’arisha na kuongeza thamani ya madini ya vito  vinavyotambulika kwa HS Codes 6804.10.00; 7018.90.00; 

7020.00.99; na kiwango cha awali cha asilimia 10 kwenye  HS Codes 3606.90.00; 6813.20.00; 8202.20.00;  8202.99.00; 8203.20.00; 8205.10.00; 8423.89.90;  8513.10.90; na 9002.19.00. Hatua hii inalenga kuchochea  uongezaji wa thamani kwenye madini. Utaratibu wa  “Duty Remission” utatumika katika kuagiza vifaa hivyo;  

(n) Kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 10  kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha  asilimia 25 kwenye makaratasi (HS Code 4805.24.00 na  4805.25.00) yanayotumika kama malighafi ya  kutengeneza vifungashio aina ya maboksi (corrugated  boxes). Utaratibu wa “Duty Remission” utatumika. Lengo  la hatua hii ni kuwapa unafuu wazalishaji wa vifungashio  hivyo hapa nchini ili wananchi waweze kuvipata kwa bei  nafuu; 

(o) Kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 0  kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha  asilimia 25 kwenye vifungashio vya mbegu  vinavyotambulika katika HS codes 3923.29.00;  6305.10.00; 4819.40.00; 7310.29.90; 6305.33.00;  6305.20.00; 6304.91.90 na 7607.19.90. Utaratibu  utakaotumika kutoa unafuu huo ni wa “duty remission”.  Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa wazalishaji wa  mbegu hapa nchini; 

(p) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 35 badala ya  asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye kahawa  inayotambulika kwa Heading 09.01 inayoagizwa kutoka  nje ya nchi. Lengo la pendekezo hili ni kulinda viwanda  vya ndani na kuhamasisha kilimo cha kahawa hapa nchini 

pamoja na kuongeza ajira katika sekta ya kilimo;  

(q) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 10 au dola za  kimarekani 125 kwa kila tani moja ya ujazo (Metric ton) kwenye bidhaa za chuma kwa mwaka mmoja kutegemea  kiwango kitakachokuwa kikubwa. Bidhaa hizo ni “Flat – rolled products of iron or Non-alloy steel na Flat –rolled  products of other alloy steel.” Bidhaa hizi hutambulika  katika HS Codes 7209.16.00; 7209.17.00; 7209.18.00;  7209.26.00; 7209.27.00; 7209.28.00; 7209.90.00; 

7211.23.00; 7211.90.00; 7225.50.0 na 7226.92.00.  Lengo la kuendelea kutoza viwango hivyo ni kulinda  viwanda vya hapa nchini, kukuza ajira pamoja na  kudhibiti udanganyifu wa thamani halisi ya bidhaa hizo  kutoka nje; 

(r) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 au dola za  kimarekani 250 kwa kila tani moja ya ujazo (metric ton) kwenye bidhaa za mabati zinazotambulika kwa HS codes  7210.41.00; 7210.49.00; 7210.61.00; 7210.69.00;  7210.70.00 na 7210.90.00 kutegemea kiwango  kitakachokuwa kikubwa badala ya ushuru wa asilimia 25  au dola za kimarekani 200 kwa kila tani moja ya ujazo 

(metric ton), kwa mwaka mmoja. Lengo la hatua hii ni  kuwalinda wazalishaji wa bidhaa hizo hapa nchini  kutokana na ushindani wa nje; 

(s) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 10 au dola za  kimarekani 250 kwa kila tani moja ya ujazo (Metric ton) kwa mwaka mmoja kutegemea kiwango kitakachokuwa kikubwa kwenye bidhaa za mabati zinazotambulika katika  HS Code 7212.60.00 badala ya ushuru wa asilimia 10 pekee. Lengo la hatua hii ni kulinda viwanda vya ndani  kutokana na udanganyifu wa thamani halisi ya bidhaa  hizo zinapoingizwa kutoka nje (under-invoicing and under valuation), na kulinda ajira na mapato ya Serikali;

(t) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 au dola za  kimarekani 250 kwa kila tani moja ya ujazo (Metric ton) kwenye bidhaa za mabati kwa mwaka mmoja kutegemea kiwango kitakachokuwa kikubwa. Ushuru huo unahusu  bidhaa zinazotambulika katika HS Code 7212.30.00;  7212.40.00 na 7212.50,00. Hatua hii ina lengo la kulinda  viwanda vya ndani kutokana na udanganyifu wa thamani  halisi ya bidhaa hizo zinapoingizwa kutoka nje (under invoicing and under valuation), na kulinda ajira na  mapato ya Serikali; 

(u) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 au dola za  kimarekani 250 badala ya kiwango cha asilimia 25 au  dola za kimarekani 200 kwa kila tani moja ya ujazo  (metric ton) kwenye bidhaa za chuma kwa mwaka mmoja  kutegemea kiwango kitakachokuwa kikubwa kwenye  nondo kwa mwaka mmoja. (Reinforment bars and hallow  profile). Hatua hii inahusu bidhaa zinazotambulika katika  HS codes 7213.10.00; 7213.20.00; 7213.99.00;  7214.10.00; 7214.20.00; 7214.30.00; 7214.90.00;  7214.99.00; 7215.10.00; 7215.50.00; 7215.90.00;  7225.90.00; 7225.92.00; 7225.99.00; 7306.30.00;  7306.50.00; 7306.61.00; 7306.69.00; na 7306.90.00.  Lengo la hatua hii ni kulinda viwanda vinavyozalisha  nondo hapa nchini na kuongeza ajira; 

(v) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 35 badala ya  asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye bidhaa za mboga  mboga (horticultural products) zinazotambulika kwa HS  codes 0603.11.00; 0603.12.00; 0603.13.00; 0603.14.00;  0603.15.00; 0603.19.00; 0604.20.00; 0604.90.00;  0701.90.00; 0702.00.00; 0703.10.00; 0703.20.00;  0703.90.00; 0706.10.00; 0706.90.00; 0710.10.00;  0710.21.00; 0710.22.00; 0710.30.00; 0714.10.00;  0714.20.00; 0804.30.00; 0804.40.00; 0804.50.00; 

0805.10.00; 0805.40.00; 0805.50.00; 0806.10.00;  0807.11.00; 0807.20.00; 0808.10.00; 0808.30.00;  0910.11.00 na 0910.12.00. Lengo la hatua hii ni kulinda  wakulima wa ndani ili kuendeleza kilimo cha matunda,  mbogamboga na maua hapa nchini;  

(w) Kutoza ushuru wa forodha kwa kiwango cha asilimia 10  badala ya asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye bidhaa  za fito za plastiki zijulikanazo kama PVC Profiles HS Code  3916.10.00; 3916.20.00; 3916.90.00 ambazo hutumika  kwa ajili ya kutengenezea fremu za milango, madirisha  n.k. Lengo la hatua hii ni kuongeza mapato ya Serikali; 

(x) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 badala ya  asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwenye karatasi  zinazozalishwa na viwanda vya hapa nchini ambazo  zinazotambulika kwa HS codes 4804.11.00; 4804.21.00;  4804.29.00; 4804.31.00 na 4804.41.00. Lengo la hatua  hii ni kuendelea kulinda viwanda vinavyozalisha karatasi  hizo hapa nchini; 

(y) Kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 10  kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha  asilimia 35 kwenye ngano inayotambulika kwa HS Code  1001.99.10 na HS Code 1001.99.90 kwa utaratibu wa  “Duty Remission” ambapo wanaonufaika na unafuu huu  ni wenye viwanda vya kusaga ngano. Lengo la hatua hii  ni kupunguza gharama kwa Viwanda vinavyozalisha unga  wa ngano; 

(z) Kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 0  kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha  asilimia 25 kwa utaratibu wa duty remission kwenye  bidhaa ijulikanayo kama “Printed Alluminium Barrier  Laminates” (ABL) HS Code 3920.10.90 ambayo hutumika 

kama malighafi ya kutengeneza vifungashio vya dawa ya  meno kwenye viwanda vya ndani. Lengo la hatua hii ni  kutoa unafuu wa gharama kwa viwanda vinavyozalisha  dawa ya meno nchini; 

(aa) Kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 0  kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha  asilimia 10 kwa utaratibu wa “Duty Remission” kwenye  malighafi ya kutengeneza sabuni ijulikanayo kama RBD  Palm Stearin (HS Code 1511.90.40) kwa viwanda 

vinavyotengeneza sabuni nchini. Lengo la hatua hii ni  kutoa unafuu kwa viwanda vya kuzalisha sabuni nchini; 

(bb) Kutoza kwa mwaka mmoja Ushuru wa Forodha wa  asilimia 25 au dola za kimarekani 1.35 kwa kilo moja ya  viberiti (safety match boxes) vinavyotambuliwa kwenye  HS code 3605.00.00 kutegemea kiwango kitakachokuwa  kikubwa badala ya asilimia 25 pekee. Lengo la hatua hii  ni kulinda viwanda vinavyozalisha viberiti nchini dhidi ya  bidhaa zenye ruzuku kutoka nje na hivyo kuwa na  ushindani sawa katika soko; 

(cc) Kutoza kwa mwaka mmoja Ushuru wa Forodha wa  asilimia 25 au dola za kimarekani 350 kwa kila tani moja  ya ujazo (Metric ton) kutegemea kiwango kitakachokuwa  kikubwa kwenye bidhaa za chuma za misumari 

zinazotambulika kwa HS code 7317.00.00 (nails, tacks,  drawing pins, corrugated nails, and staples other than  those of heading 83.05) badala ya asilimia 25 pekee.  Hatua hii inalenga kulinda viwanda vinavyozalisha bidhaa  hizo nchini. 

(dd) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 35 badala ya  asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye soseji (sausages) na bidhaa za aina hiyo zinazotambulika kwa HS code 

1601.00.00. Lengo ni kuendelea kulinda wajasiriamali wa  ndani wanaozalisha bidhaa hizo; 

(ee) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 35 badala ya asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye chingamu  (chewing gum HS Code 1704.10.00), biskuti (Heading  19.05) na peremende (HS code 1704.90.00) zinazoagizwa  kutoka nje. Lengo ni kuendelea kulinda viwanda vya  ndani vinavyozalisha bidhaa hizo na kukuza ajira; 

(ff) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 35 badala ya  asilimia 25 kwenye chokoleti (chocolates) Heading 18.06  kwa mwaka mmoja. Lengo ni kulinda viwanda vya ndani na kukuza ajira; 

(gg) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 35 badala ya  asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye nyanya  zilizosindikwa (tomato sauces) zinazotambulika katika HS  code 2103.20.00. Hatua hii inalenga kulinda viwanda  vinavyosindika nyanya nchini; 

(hh) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 60 badala ya  asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye maji ya kunywa  (mineral water) yanayotambulika katika HS code  2201.10.00. Hatua hii inalenga kulinda viwanda  vinavozalisha maji ya kunywa nchini; 

(ii) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 35 badala ya  asilimia 25 kwenye nyama zilizoainishwa katika SURA ya  2 katika Viwango vya pamoja vya ushuru wa forodha  (meat and edible meat offal of Chapter 2) kwa mwaka  mmoja. Lengo la hatua hii ni kuendelea kulinda na  kuchochea sekta ya ufugaji nchini;

(jj) Kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 25  kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha  asilimia 10 kwenye mafuta ghafi ya kula yanayotambulika  kwa HS codes 1507.10.00, 1580.10.00, 1511.10.00,  1512.11.00, 1513.11.00, 1514.11.00, 1514.91.00,  1515.11.00, 1515.21.00 na 1515.30.00. Hatua hii  inalenga kulinda na kuhamasisha uzalishaji wa mbegu za  mafuta ya kula nchini, kuongeza ajira mashambani,  viwandani pamoja na kulinda fedha za kigeni  zinazotumika kuagiza mafuta hayo nje ya nchi; 

(kk) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 35 badala ya  asilimia 10 au 25 kwa mwaka mmoja kwenye mafuta ya  kula yaliyochakatwa kwa kiwango cha kati na mwisho  (semi-refined and refined) yanayotambulika kwa HS  codes 1507.90.00, 1508.90.00, 1509.90.00, 1510.00.00,  1511.90.10, 1511.90.30, 1511.90.90, 1512.19.00,  1512.29.00, 1513.19.00, 1513.29.00, 1514.19.00,  1514.99.00, 1515.19.00, 1515.20.00, 1515.50.00 na  1515.90.00. Lengo la hatua hii ni kuhamasisha uchakataji  wa mbegu za mafuta ya kula nchini, kuongeza ajira  viwandani na mashambani pamoja na kulinda fedha za  kigeni zinazotumika kuagiza mafuta hayo nje ya nchi; 

(ll) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 10 badala ya  asilimia 0 kwenye Gypsum Powder HS code 2520.20.00  kwa mwaka mmoja. Lengo la hatua hii ni kulinda  wazalishaji wa Gypsum Powder nchini; 

(mm)Kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 35 kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha asilimia 100  kwenye sukari ya matumizi ya kawaida (consumption  sugar) inayoagizwa kutoka nje ya nchi kwa vibali maalum  kwa lengo la kuziba pengo (gap) la uzalishaji hapa nchini; 

(nn) Kutoza kwa mwaka mmoja Ushuru wa Forodha wa  asilimia 35 kwenye mitumba inayoingia kutoka nje badala  ya asilimia 35 au dola za marekani 0.40 kwa kilo moja  kutegemea kiwango kipi kikubwa kwa lengo la kutoa  unafuu kwa watumiaji nchini; 

(oo) Kutoa unafuu wa Ushuru wa Forodha kwenye malighafi,  vipuri na mashine vinavyotumika katika kutengeneza  viatu vya ngozi na nguo. Lengo la hatua hii ni  kuhamasisha ukuaji wa sekta ya nguo na viatu vya ngozi  nchini; na 

(pp) Kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 0  kwa utaratibu wa “Duty Remission” kwenye malighafi ya  kutengeneza leaf springs za magari inayotambulika kwa  HS Code 7228.20.00. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu  kwa viwanda vya kuzalisha bidhaa hiyo nchini. 

(iii) Mawaziri wa Fedha wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika  Mashariki walikubaliana kufanya marekebisho kwenye  Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika  Mashariki (EAC Customs Management Act, 2004) kwa  kuweka thamani ya chini ya bidhaa isiyopaswa kutozwa ushuru  wa Forodha kuwa Dola za Marekani 50. 

(iv) Serikali inapendekeza kuliachia jukumu la uthaminishaji wa  vitenge vinavyoingizwa nchini kwa Kamishna wa Mamlaka ya  Mapato Tanzania ili uthaminishaji wa bidhaa hiyo uzingatie  Kanuni zilizowekwa kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa  Forodha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (2004). Sambamba na  hatua hiyo, napendekeza utaratibu wa kuthaminisha vitenge  kuwa dola za Marekani kati ya 0.55 hadi dola za Marekani 1  kwa mita ya kitenge cha Polyester na dola za Marekani kati ya  0.60 hadi dola za Marekani 1 kwa mita ya kitenge chenye  pamba inapotokea thamani iliyowasilishwa (declared) kuwa chini ya kiwango hicho maalumu kwa kuzingatia taratibu za  uthaminishaji wa bidhaa hizo. 

(v) Kuondoa sharti la kuweka dhamana ya asilimia 15 ya ziada ya  Ushuru wa Forodha inayopaswa kurejeshwa (refundable)  kwenye sukari ya matumizi ya viwandani. Lengo la hatua hii ni kuwaongezea wazalishaji ukwasi (liquidity) kwa kutowazuilia  mtaji wa uzalishaji (working capital). Hata hivyo, wazalishaji  watakaobainika kufanya udanganyifu watarejeshewa sharti hili  pamoja na kuchukuliwa hatua nyingine zilizopo kisheria. 

Hatua hizi kwa ujumla wake zinatarajiwa kupunguza mapato ya  Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 32,626.38. 

Pia amezungumzia Sheria ya Usimamizi wa Kodi,Waziri huyu amependekeza kufanyia Marekebisho ya  Sheria ya Usimamizi wa Kodi.

(i) Kufuta kifungu cha 92A kwa lengo la kuziwezesha mahakama  kukusanya mapato yanayotokana na adhabu na faini  zinazolipwa mahakamani badala ya Mamlaka ya Mapato  Tanzania kama ilivyo kwa faini na adhabu kwa makosa  mengine ambayo mahakama huyatolea maamuzi na hivyo  kurahisisha ukusanywaji wa mapato hayo; 

(ii) Kufuta kifungu cha 70(2) ili kumpa Mamlaka Kamishna Mkuu  wa Mamlaka ya Mapato kutekeleza matakwa ya Sheria husika na kurahisisha upunguzaji au uondoaji wa riba na adhabu ya  madeni iwapo kutakuwa na sababu za msingi za kufanya hivyo; na 

(iii) Kufanya marekebisho ya Kanuni Na. 15 ya ukokotoaji wa kodi  za kimataifa (Transfer Pricing Regulations) kwa kufuta kifungu  kinachoweka adhabu ya asilimia 100 kwa kushindwa kutekeleza matakwa ya Sheria. Lengo la hatua hii ni kuwaondolea walipakodi adhabu kubwa ili kuboresha mazingira ya ufanyaji  biashara na kuvutia uwekezaji nchini. 

Kuhusu Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, amependekeza kufanya Marekebisho  kwenye Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa kama ifuatavyo: 

(i) Kubainisha mazingira ambayo Kampuni iliyolipa tozo ya  huduma haitawajibika kulipa tozo ya uzalishaji. Marekebisho  hayo yanalenga kutatua mgongano uliojitokeza kwenye  kutafsiri kifungu husika; na 

(ii) Kupunguza ada za matangazo kama ifuatavyo: 

(a) Mabango yanayowaka kutoka shilingi 18,000 hadi shilingi  13,000; 

(b) Mabango yasiyowaka kutoka shilingi 15,000 hadi shilingi  10,000; 

(c) Matangazo ya ukutani kutoka shilingi 15,000 hadi shilingi  10,000; 

(d) Matangazo ya kielectroniki kutoka shilingi 20,000 hadi  shilingi 10,000; 

(e) Matangazo kwenye magari kutoka shilingi 15,000 hadi  shillingi 10,000 kwa watangazaji wanaotangaza bidhaa za  watu wengine; 

(f) Matangazo ya muda mfupi/promosheni kwa siku kutoka  shilingi 55,000 hadi shilingi 50,000; na

53 

(g) Kila mabango 100 ya promosheni ya kwanza au sehemu  ya fungu la mabango 100 ya kwanza kutoka shilingi  100,000 hadi shilingi 50,000. 

Ada zote hizi zinatozwa kwa futi za mraba. Kushushwa kwa ada  hizi kutapunguza gharama za kutangaza biashara nchini na  hatimaye kukuza ushindani kwenye biashara. 

Kuhusu Sheria ya Kodi ya Majengo,amependekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya kodi ya majengo, ili ukusanyaji wa kodi  ya majengo ufanyike kwa kutumia mfumo wa ununuzi na utumiaji  wa umeme kupitia mashine za LUKU. Kila mita ya umeme ina uhusiano na mmiliki wa jengo au mtumiaji wa mita.

’’ kwa kuwa  Sheria ya Kodi ya Majengo inataka kodi hiyo ikusanywe kwa mmiliki  au mtumiaji wa jengo, hivyo, napendekeza kodi ya majengo ya  kiwango cha shilingi 1,000/= kwa mwezi kwenye nyumba za kawaida zenye mita moja na itakatwa kwenye ununuzi wa umeme (LUKU).’’amefafanua.

Aidha, amependekeza kuwa  kiwango cha shilingi 5,000/= kwa  mwezi kwa kila ghorofa au apartment zenye mita moja na itakatwa kwenye ununuzi wa umeme (LUKU). Serikali itaweka utaratibu  kwenye nyumba za kawaida na za ghorofa zinazochangia mita moja  na zinazotumia mita zaidi ya moja. 

Upande wa Sheria ya Ardhi, Waziri huyu amependekeza kufanya marekebisho ya  Sheria ya Ardhi,  na Kanuni zake za mwaka 2001 kwa kupunguza tozo ya mbele (premium) inayotozwa wakati wa  umilikishaji wa ardhi .

Amesema kuwa ni Kupunguza tozo kutoka asilimia 2.5 hadi asilimia 0.5 kwa  umiliki mpya wa ardhi na Kupunguza tozo kutoka asilimia 1 hadi asilimia 0.5 kwa  urasimishaji.  

Amesema kuwa Lengo la pendekezo hilo ni kuhamasisha wamiliki wa ardhi  kukamilisha taratibu za kupata hatimiliki na kufanikisha sehemu  kubwa ya ardhi kuandikishwa na kupunguza migogoro. Hatua za  kufanya marekebisho ya Sheria ya Ardhi kwa ujumla wake zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 9,000. 

Kuhusu Sheria ya Ushuru wa Stempu Waziri amependekeza kuifanyia Marekebisho  Sheria ya Ushuru wa Stempu kwa lengo la kuhuisha viwango  vilivyopo sambamba na mfumuko wa bei kwa kuwa viwango hivyo  ni vya muda mrefu tangu mwaka 2006. Marekebisho .(i) Ushuru wa Stempu kutoka shilingi 500 hadi shilingi 2,000; 

(ii) Ushuru wa Stempu kwenye Katiba za Makampuni kutoka  shilingi 5,000 hadi shilingi 10,000; 

(iii) Ushuru wa Stempu kwenye nyaraka za Ubia ambazo mtaji  wake unazidi shilingi 100,000 lakini hauzidi shilingi 1,000,000  kutoka shilingi 2,000 hadi shilingi 5,000; 

(iv) Ushuru wa Stempu kwenye nyaraka za Ubia ambazo mtaji  wake unazidi shilingi 1,000,000 kutoka shilingi 5,000 hadi  shilingi 10,000; na 

(v) Ushuru wa Stempu kwenye nyaraka za kumaliza ubia kutoka  shilingi 1,000 hadi 10,000. 

Hatua za kufanya marekebisho ya Sheria ya Ushuru wa Stempu kwa  ujumla wake zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi  cha shilingi milioni 2,500.89.

Kuhusu Sheria ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi,Waziri amependekeza kufanya marekebisho  kwenye Sheria ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi kwa Kupandisha kiwango cha chini cha idadi ya waajiriwa  wanaostahili kulipiwa kodi kutoka 4 wa sasa hadi 10. Lengo la  marekebisho haya ni kuwapunguzia mzigo wa kodi waajiri  wenye idadi ndogo ya waajiriwa na kuchochea ukuaji wa  uwekezaji nchini; 

Pamoja na Kufuta tozo ya Elimu na mafunzo ya Ufundi Stadi kwa hospitali  zinazomilikiwa na taasisi za kidini kwa kuwa taasisi hizi zimekuwa zikiisaidia sana Serikali kufikisha huduma za afya  hata kwenye maeneo ambayo Serikali haijaweza kupeleka  huduma kutokana na ufinyu wa Bajeti.

Aidha, taasisi hizo  zimekuwa na ushirikiano na Serikali kwa makubaliano maalum kwa baadhi ya maeneo ya kutoa huduma za afya. Lengo la  hatua hii ni kutoa unafuu wa utoaji huduma za afya kwa vituo  vya Afya na Kuanzisha utaratibu mahsusi wa ulipaji wa tozo kwa  wachimbaji wadogo wa madini kuwa ni asilimia 0.4 ya thamani  ya mauzo ya madini itakayolipwa na mchimbaji mdogo wa  madini pindi atakapouza madini hayo kwenye masoko na vituo  vya madini vinavyotambulika na Tume ya Taifa ya Madini. 

Kwa upande wa Sheria ya Michezo ya Kubatisha Waziri huyu amependekeza kufanya mabadiliko ya  Sheria ya Michezo ya Kubahatisha kwa  Kupunguza kiwango cha kodi kwenye zawadi ya ushindi  (Gaming tax on Winnings) kutoka asilimia 20 hadi asilimia 15kwenye Michezo ya kubahatisha ya ubashiri wa matokeo ya  michezo (Sports betting); 

Amesema kuwa Kuongeza kiwango cha Kodi katika michezo ya kubahatisha ya  ubashiri wa matokeo ya michezo (sports betting) kwa mapato  ghafi (Gross Gaming Revenue – GGR) kutoka asilimia 25 ya  mauzo ghafi hadi asilimia 30 ya mauzo ghafi. Ongezeko la  asilimia 5 litapelekwa kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Michezo  kwa ajili ya kuendeleza michezo nchini;  

Hivyo amesema kuwa Kutoza kodi ya michezo ya kubahatisha kwa asilimia 10 ya  mapato ghafi kwenye michezo ya kubahatisha inayoendeshwa kwa kompyuta (Virtual Games) na Kutoza Kodi ya michezo ya kubahatisha kwa asilimia 10 ya  mapato ghafi kwenye michezo ya kubahatisha iliyo chini ya  majaribio. 

Amesema kuwa Lengo la hatua hizi ni kuleta usawa wa utozaji kodi katika michezo  ya kubahatisha. Hatua hizi za marekebisho ya michezo ya  kubahatisha zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi  cha shilingi milioni 14,925.38. 

Sheria ya Ukaguzi wa Umma,Waziri huyu amependekeza kufanya Marekebisho  kwenye Sheria ya Ukaguzi wa Umma, kwa Kumwezesha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali  kuwa na uwezo wa kisheria wa kukagua mashirika  yaliyoanzishwa chini ya Sheria ya Makampuni ambayo Serikali  ina umiliki wa hisa ili kumwezesha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu  kukagua mashirika/makampuni hayo. Kwa sasa Mdhibiti na  Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali anakagua mashirika/makampuni hayo bila kuwa na nguvu za kisheria, hali inayoweza kuleta mgogoro wa kisheria; na 

Amesema kuwa Kumwezesha Waziri mwenye dhamana ya Fedha kuwasilisha  Bungeni majibu kuhusu taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu  wa Hesabu za Serikali kwenye kikao kinachofuata cha Bunge baada ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuwasilisha taarifa yake badala ya utaratibu wa sasa ambapo  taarifa zote huwasilishwa kwa pamoja katika kikao kimoja cha  Bunge. 

Kuhusu Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada,amependekeza kufanya marekebisho  kwenye Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada SURA 134 ili  kuruhusu Serikali kudhamini kampuni au taasisi yoyote kukopa kiasi  kisichozidi thamani ya Hisa za Serikali ya Tanzania kwenye mradi husika baada ya kupata ridhaa ya Baraza la Mawaziri.

Kwa upande  Sheria ya Usajili wa Magari, Waziri huyu amependekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Usajili wa Magari SURA 124, kwa kupunguza ada  ya usajili wa magari kwa namba binafsi kutoka shillingi 10,000,000  hadi shillingi 5,000,000 kila baada ya miaka mitatu.

Amesema kuwa Lengo hilo ni kuwezesha wamiliki wa magari kuchagua namba binafsi ya  usajili wa gari kwa gharama nafuu na hivyo kuongeza mapato ya  Serikali kwa kuwa kiwango cha sasa hakina mwitikio mzuri.  

Hatua hizo za marekebisho ya Sheria ya Usajili wa Magari  inatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi  milioni 270.

Kuhusu Sheria ya Usalama Barabarani, amesema kuwa vijana wengi wamejiajiri kwenye sekta  ndogo ya kuendesha bajaji na pikipiki zikijulikana kama bodaboda. Hata hivyo, Vijana hawo hupata usumbufu mkubwa wa kulipa faini  kutoka kwenye vipato vyao pale panapotokea uvunjaji wa Sheria ya  Usalama Barabarani umefanywa na abiria Hali hii imekuwa  ikisababisha baadhi yao kushindwa kulipa faini na hivyo kuzitelekeza  pikipiki zao kwenye vituo vya polisi.

‘’Mhe. Rais ameelekeza  jeshi la Polisi kujikita kwenye kutoa elimu kuhusu usalama  barabarani badala ya kuwekeza kwenye makosa na kugeuza faini  kuwa chanzo cha mapato. Hivyo basi, napendekeza kupunguza  adhabu zinazotolewa chini ya Sheria ya Usalama Barabarani kwa makosa ya Pikipiki na Bajaji kutoka shilingi 30,000 za sasa  hadi shilingi 10,000 kwa kosa moja.

Amesema kuwa Lengo la hatua hii ni kuweka  adhabu kwa kuzingatia uwezo wa kulipa. Aidha, adhabu kwa makosa mengine ya vyombo vya moto zinazotolewa kwa mujibu wa  Sheria zinaendelea kubaki kama ilivyo sasa.  

Kwa upande wake Sheria ya Raia wa Kigeni (Uratibu wa Ajira), Waziri amependekeza kufanya marekebisho ya  Sheria ya Raia wa Kigeni (Uratibu wa Ajira), Na. 1 ya 2015 kwa Kuweka adhabu ya kiasi cha shilingi 500,000/= kwa kila mwezi  kwa mwajiri aliyeajiri raia wa kigeni na kushindwa kuwasilisha  ritani za kila mwezi zenye taarifa za raia wa kigeni aliowaajiri  ikiwemo taarifa zao za mishahara kwa Kamishna wa Kazi. 

 Lengo la pendekezo hilo ni kuhimiza uwajibikaji wa hiari kwa Kuweka adhabu ya kifungo cha miezi 12 au faini ya shilingi  millioni kumi (10) au vyote kwa mwajiri aliyeajiri raia wa kigeni  na kushindwa kuwasilisha ritani za mwezi zenye taarifa za raia 

wa kigeni aliowaajiri ikiwemo taarifa zao za mishahara kwa  Kamisha wa kazi. Lengo la pendekezo hili ni kuhimiza  uwajibikaji wa hiari. 

Marekebisho ya Ada na Tozo mbalimbali zinazotozwa na  Wizara, Mikoa, Wakala, Mamlaka za Udhibiti na Idara  zinazojitegemea 

Waziri huyu amependekeza kufanya marekebisho ya  viwango vya ada na tozo mbalimbali zinazotozwa na Wizara, Mikoa,  Wakala, Mamlaka za Udhibiti na Idara zinazojitegemea ili kuvihuisha  kulingana na hali halisi ya ukuaji wa uchumi,marekebisho  hayo yataainishwa katika Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka  2021 na Matangazo ya Serikali (Government Notices). Marekebisho  hayo .

Amesema kuwa Wizara ya Kilimo Kuanzisha Tozo za Umwagiliaji kwa watumiaji wa miundombinu ya umwagiliaji ili kuwezesha miradi hiyo kuwa endelevu na kuwezesha ujenzi wa miundombinu mipya.

Viwango vinavyopendekezwa kama ifuatavyo: 

(a) Kutoza ada ya shillingi 60,000 kwenye usajili wa vyama vya  umwagiliaji; na 

(b) Kutoza ada ya Huduma ya umwagiliaji ya asilimia 5 ya mavuno  ya msimu kwa eneo la vyama vya umwagiliaji.