Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvesty Koka wa kati kati aliyevaa suti akiwa ameshika mfano wa Hundi yenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni 312 ambazo zimetolewa na halmashauri ya mji kibaha kwa ajili ya kuvikopesha vikundi mbali mbali vya vijana, wakinama na walemavu ikiwa ni utekelezaji wa agizo la serikali la kutenga asilimi 10 kutoka vyanzo vya mapato yake ya ndani.
Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka wa kushoto akiwa anazungumza jambo na kumpatia maelezo ya jinsi ya kujikwamua nawimbi la umasikini na mmoja wa vijana wajasiriamali ambao wameweza kunufaika na mkopo wa pikipiki ambazo zimetolewa na halmashauri ya mji Kibaha.
Mbungewa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akizungumza katika halfa hiyo na baadhi ya vikundi mbali mbali ambavyo vimewezeshwa na halmashauri mikopo ya fedha, pikipiki, bajaji pamoja na toyo ili kuweza kujikwamua kiuchumi na kuendeshea biashara zao mbali mbali.
Mmoja wa wanawake kutoka kundi la walemavu Joyce Salumu akitoa neon lake la shukrani kwa Mgeni rasmi ambaye ni Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini hayupo pichani wakati wa halfa hiyo ya kukabidhiwa mikopo ambapo amepatiwa mkopo binafsi kwa ajili ya kuendeshea shughuli zake.
Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya mji Kibaha Selena Wilson akizungumza katika halfa hiyo ambayo ilihudhuliwa n aviongozi mbali mbali wa serikali ikiwemo madiwani mbali mbali kutoka kata 14.
Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya mji Kibaha kushoto akiwa anawatambulisha madiwani mbali mbali waliofika katika halfa hiyo ya utoaji wa mikopo kutoka kwa makundi mbali mbali ya vijana, wanawake na walemavu.
*********************************
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
HALMASHAURI ya mjini Kibaha iliyopo mkoani Pwani katika kutekeleza kwa vitendo maagizo ya serikali ya kutenga asilimia 10 kwa ajili ya kuwapatia mikopo ambayo haina liba kwa makundi mbali mbali yakiwemo ya vijana, wanawake ,pamoja na kundi la walemavu imetoa kiasi cha shilingi milioni 312 kwa ajili kuviwezesha vikundi hivyo lengo ikiwa ni kujikwamua kiuchumi na kuondokana na wimbi la umasikini.
Akikabidhi hundi ya fedha hizo ambazo zimetolewa na halmashauri hiyo kwa vikundi hivyo Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka ambaye alikuwa ndiye mgeni rasmi katika halfa hiyo ambayo pia iliambatana na ugawaji wa vifaa vinavyofanya shughuli mbali mbali za usafirishaji ikiwemo Bajaji, Pikipiki.pamoja na Toyo vyote vikiwa na tahamani ya zaidi ya milioni 66.
Koka katika hotuba yake kwa wanavikundi hao aliwataka kuhakikisha kwamba fedha hizo amabzo wamepatiwa na serikali wazitumia vizuri kwa kuweza kutumia fursa mbali mbali zilizopo katika kufanya shughuli za ujasiriamali pamoja na kuanzisha biashara ambazo zitawasaidia kujipatia kipatoikiwemo na kukuza uchumi.
Pia Mbunge huyo alivihasa vikundi hivyo kujiwekea malengo na kwamba ili waweze kutimiza ndoto zao na kufanikiwa inapaswa waahakikishe kwamba wanakuwa na nidhamu katika fedha sambamba na kubuni biashara nyingine mpya amabzo zitaweza kuzaa matunda na kuwahidi kuendelea kuwapa ushirikiano wa kutosha.
Pia alisema kwamba wananchi pamoja na viongozi wa ngazi mbali mbali kuhakikisha kuwa wanakuwa mstari wa mbele katika kumpa ushirikiano na sapoti ya kutosha Rais wa awamu ya sita Mama Samia Suluhu Hassan ili aweze kutumiza majukumu yake ipasavyo katika kulitumikia Taifa la Tanzania pamoja na kuwaletea chachu ya maendeleo wananchi katika Nyanja mbali mbali.
Aidha Koka alisema kwamba anatambua kwamb a katika jimbo lake kuna baadhi ya changamoto zilizopo hasa za miundombinu ya barabara inayokwenda katika hospitali ya Wilaya iliyopo maeno ya Lulanzi na kuwaahidi wananchi wake kulivalia njuga suala hilo kwa kushirikiana na serikali na mamala usika ili kuweka kiwango cha lami ili iweze kupitika kwa urahisi na wananchi waweze kwenda kupatiwa huduma ya matibabu bila kero yoyote.
“Kwanza kabisa mimi napenda kumshukuru sana mama yetu mpendwa Rais wa awamu ya sita Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri ambayo anaifanya ya kuiongoza nchi yetu ya Tanzania pamoja na kutupa ushirikiano wa hali na mali katika suala zima la kimaendeleo na mimi nitahakikisha kwamba zile changamoto mbali mbali zilizopo ninazifanyia kazi kwa kushirikiana na viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na baraza la madiwani nia yetu ni kuleta mapinduzi hasa katika jimbo langu la Kibaha mji,”alisema Koka.
Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya mji Kibaha George Mbogo alibainisha kuwa kwa kipindi cha mwaka 2020 /2021 kupitia idara ya maendeleo ya jamii imeweza kuhamasisha wananchi kuunda vikundi vya kijamii ambapo jumla ya vikundi 327 kutoka katika kata 14 viliweza kuundwa na kusajiliwa.
Pia aliongeza kuwa jumla ya wanawake wapatao 150 waliweza kupatiwa mafunzo ya kuendesha vikundo vyao pamoja na kupatiwa mafunzo mbali mbali kwa kushirikiana na taasisi za fedha lengo ikiwa ni kuvijengea uwezo ambao watakuwa wanautumia katika shughuli zao za biashara kutokana mikopo hiyo wanayopatiwa ambayo haina liba.
Kaimu mkurugenzi huyo alifafanua kuwa Halmashauri ya mji KIbaha imeweza kujenga kituo cha biashara kwa wanawake wajasiriamali kilichopo kwenye soko la mnarani pamoja na eneo maalumu la kuuzia kuku kwa madhumuni ya kuinua zaidi biashara zao kwa kuanzisha mitandao yao.
Naye Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya mji Kibaha Selina Wilson alisema kwamba bado kuna changamoto ya ucheleweshaji wa kurejesha mikopo hiyo hasa katika baadhi ya makundi ya vijana na kuwataka kuhakikisha kwamba wanarejesha kwa wakati bila kuvunja taratibu zote zilizowekwa ili kuwapa fursa wengine waweze kupata.
Selina aliongeza kuwa mbai na halmashauri hiyo kutoa mikopo ya fedha, pamoja na vifaa mbali mbali lakini wanatarajia kuongeza wigo zaidi ya ukopeshaji ambao wameweka mikakati kabambe katika siku za usoni kuwezo kuvipatia vikundi mbali mbali mikopo mikubwa zaidi ikiwemo kuwapatia magari ambayo yatawasaidia katika kuendeshea biashara zao.