Home Mchanganyiko MASHAMBA YA MBEGU KUFUFULIWA ILI KULETA TIJA UZALISHAJI MBEGU

MASHAMBA YA MBEGU KUFUFULIWA ILI KULETA TIJA UZALISHAJI MBEGU

0
Waziri wa Kilimo Prof.Aldof Mkenda ,akizungumza wakati wa kikao cha Menejimenti na Bodi ya Wakala wa Mbegu (ASA) kilichofanyika leo Mei 11,2021 jijini Dodoma.
Mjumbe wa Wakala wa Mbegu (ASA) Bi.Gladness Temu,akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Kilimo Prof.Aldof Mkenda mara baada ya kikao cha Menejimenti na Bodi ya Wakala wa Mbegu (ASA) kilichofanyika leo Mei 11,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa Kikao wakifatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Prof.Aldof Mkenda (hayupo pichani)  wakati wa kikao cha Menejimenti na Bodi ya Wakala wa Mbegu (ASA) kilichofanyika leo Mei 11,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Kilimo Prof.Aldof Mkenda ,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufanya kikao cha Menejimenti na Bodi ya Wakala wa Mbegu (ASA) kilichofanyika leo Mei 11,2021 jijini Dodoma.
……………………………………………………………..
Na Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Kilimo Prof.Aldof Mkenda amesema kuwa kupitia Wakala wa Mbegu (ASA ) inatarajia kufufua mashamba 13 ya  mbegu kwa ajili ya mbegu bora zitakazowasaidia
wakulima kuzalisha mazao yao kwa tija.
Hayo amesema leo Mei 11,2021 jijini Dodoma wakati akizungumza na  Menejimenti na Bodi ya ASA amesema kuwa uzalishaji wa mbegu bora lakini pia kuangalia changamoto
katika eneo hilo na kuzitafutia ufumbuzi.

Prof.Mkenda amesema kuwa hivi sasa kipaumbele cha Wizara hiyo ni katika uzalishaji wa mbegu bora kupitia mashamba hayo ndio maana imejipanga
kuanzisha mfuko huo.

 “Tutajitahidi katika hili kwa sababu tunaanzisha mfuko wa umwagiliaji tukipata fedha tutapeleka katika miradi inayoendelea na siyo kuanzisha
vitu vipya,”amesema Prof.Mkenda.

Ameeleza kuwa itasaidia kupunguza matumizi ya fedha za kigeni kutokana na kuagiza mbegu nje ya nchi ambapo serikali itajitahidi na ASA
kusimamia suala hilo.

Pia Prof.Mkenda  amesema kuwa ipo haja ya serikali kuwa msimamo unaoakisi kauli mbiu ya kilimo ni uti wa mgongo ili wakulima walime kwa tija na kuondokana na umasikini miongoni mwao.

“Tunaweza kuwa na uchumi wa kati na hata kufikia uchumi wa juu lakini wimbi la umasikini likaendelea kwa wananchi na tukawa tegemezi wa chakula,lakini pia hatuwezi kuwa na mageuzi ya viwanda bila kufanya mageuzi ya kilimo hususani katika suala la mbegu,”amesema

Hata hivyo amesema kuwa ni lazima mashamba yote ya ASA yafufuliwe kwa kuwa utegemezi wa mbegu kutoka nje ya nchi wakati mwingine hausaidii kilimo cha hapa nchini.

Awali  Mwenyekiti wa Bodi ya ASA, Dk. Ashura Kihupi amesema kuwa zipo kero kubwa kwenye sekta ya mbegu ni uwekezaji mdogo uliofanywa na serikali, mtaji mdogo kwa ajili ya kuzalisha mbegu.

Dk.Kihupi amesema kuwa katika shamba la mbegu la Msimba lililopo wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, hasara kubwa imetokea kwa sababu hakuna kilimo cha
umwagiliaji.