Home Mchanganyiko Waziri mkuu awataka wawekezaji kuwaita marafikizao kuja kuwekeza Tanzania

Waziri mkuu awataka wawekezaji kuwaita marafikizao kuja kuwekeza Tanzania

0

Waziri mkuu Kasimu Majaliwa akisiliza maelekezo kutoka kwa Baraka Samson ,wakati alipofanya ziara ya kutembelea Kiwanda cha kutengeneza Magari GFA-Vehicle Assembling kilichopo Kibaha mkoani  Pwani jana. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho Ally Jawad Karmali

Waziri mkuu Kasimu Majaliwa akisiliza maelekezo kutoka kwa, Elizabert Mwaya wakati alipofanya ziara ya kutembelea Kiwanda cha kutengeneza Magari GFA-Vehicle Assembling kilichopo Kibaha mkoani  Pwani jana.kulia ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho Ally Jawad Karmali.P

Waziri mkuu Kassimu Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi wa kiwanda cha kutengeneza magari cha GFA-Vehicle Assembling kilichopo Kibaha wakati wa ziara ya kukagua kiwanda hicho jana.Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo.

***********************************

Waziri  mkuu Kassim Majaliwa ame wakata wawekezaji kuwaalika marafiki zao nje ya mipaka ya Tanzania kuja kuwekeza Tanzania  kwa kuwa kuna miundombinu Raifiki katika sekta ya uwekezaji nchin

Aliyasema hayo wakati wa ziara ya kukagua kiwanda cha  Kuunganisha magari cha GF-Vehicle Assembling kilichopo Kibaha mkoni Pwani na kuwahakikishia  wawekezaji nchini kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono katika jitihada zao za uwekezaji kwa kuhakikisha hawapati changamoto.

Aidha amesema kuwa zile changamoto zitakazojitokea zinazopo ndani ya uwezo wa Serikali basi Serikali itazisimamia na kuzitatua ili waweze kuendelea kufanya vizuri .

Pia ameupongeza mkoa wa Pwani kwa kutumia kwa kutumia fursa ya maendeleo ya viwanda nchini ambapo kwanza umeweza jutenga maeneo mengi ya ardhi katika halmashauri zake zote na kuvutia wawekezaji wengi.

Awali Mkuu wa mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo ameeleza kuwa mkoa huo ni wa viwanda ambapo adi leo una vimefikia 1438 kati yake vikubwa kama hicho alichotembelea ni zaidi ya 82.

Kwa Upande wa mkurugenzi wa Kiwanda hicho Ali Jawad Karmali alisema wao kama GFA Wanajivunia kuwekeza nchini Tanzania na kuwa kiwanda cha kwanza kutengeneza magari nchini

Pia Karmali aliiomba serikali kupitia tasisisi zake ikiwemo majeshi na  kuwapa kazi ya kutengeneza magari yao badalka ya kuagiza gari kamili waagizre vipuli na jukumu la kuunganisha liwe  juu yao

Vile vile alisisitiza kuwa anamini changamoto ndogo ndogo wanazo kutana nazo zitatatuliwa kwa kushirikiana na serikali Kampuni hiyo imetoa ajira zaidi ya 100 kwa watanzania ambao zimegawanyika katika sehemu 3 za kugumu ,mikataba na za muda mfupi alimaliza Karmali