KAMANDA wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Wilboard
Mtafungwa amewataka ametoa onyo kali kwa madereva wa malori na mafuso hapa
nchini ambao wamekuwa wakiendesha magari nyakati za usiku wakiwa wamelewa waache
tabia hiyo mara la sivyo watajikuta wakiishia kwenye mikono ya sheria.
Mtafungwa aliyasema hayo akiwa mkoani Tanga wakati alipokuwa
akiongea na madereva ,sambamba na watoa huduma wa mabasi juu ya masuala ya
usalama barabarani kwenye kituo cha
Stendi ya Mabasi Kange na eneo la Mabanda ya Papa alipozungumza na madereva wa
malori.
Alisema kwamba wapo baadhi ya madereva ambao wamekuwa
wakiendesha magari hayo wakitokea Dar es Salaam wanasubiri mpaka gizo liingie
kwa kisingizio kwamba serikali,Jeshi la Polisi itakuwa imelala wanakaa sehemu
wanaanza kunywa pombe matokeo yake wanakwenda kuendesha magari wakiwa wamelewa.
“Madereva mnaoendesha Malori ,Mafuso wakiwa wamelewa ndugu
zangu niwaambie kwamba maisha yenu yana thamani kubwa sana na kuishi ni mara
moja hakuna kuishi mara mbili lazima mjali maisha yenu wewe umetoka na fuso Dare
s Salaam unasuburi mpaka giza liingie
kwa kisingizio kwamba serikali itakuwa imelala polisi sasa wewe ulali unakaa
sehemu unaanza kunywa na pombe matokeo yake unakuja kuendesha gari ukiwa
umelewa”Alisema
Alisema kwa sasa hayo
wamekwisha kuyabaini na wameweka utaratibu wa kuwakagua hata nyakati za usiku
RTO pelekeni askari wakiwa wamevaa kiraia au sare wahakikisheni wanawakagua mpaka usiku lori ambalo
linatiliwa walisimamishe wapime ulevi madereva kwa sababu wanavyo vya kutosha
wakigundua wamekunywa pombe wamelewa wamakatwe wakae ndani mpaka pombe zake
ziishe na baadae wawapeleke mahakamani.
Kamanda Mtafungwa alisema hatua hizo ni kubwa na hawataki
zichukuliwe wanataka kila mtu athamni kazi anayofanya lakini niwaambie wale
walevi kaeni chonjo hatua kali za kisheria zitaendelea kuchukuliwa dhidi yenu
kutokana na kutokufuata sheria zilizopo.