Home Mchanganyiko MAGUFULI KUZIKWA MACHI 26 CHATO

MAGUFULI KUZIKWA MACHI 26 CHATO

0

…………………………………………………………………………………..

Ratiba ya mazishi ya aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli imebadilishwa na sasa atazikwa Machi 26, 2021 badala ya Machi 25 iliyopangwa awali.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya msemaji mkuu wa Serikali inaeleza kuwa viongozi wa Serikali watashiriki ibada ya kuaga leo Jumamosi Machi 20, 2021 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Kesho Jumapili  Machi 21, 2021 wananchi wa Jiji la Dar es Salaam na maeneo jirani wataaga na mwili huo utasafirishwa kwenda Dodoma ambao wananchi wa Mkoa huo watatoa heshima zao za mwisho Jumatatu Machi 22, 2021 katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Wananchi wa Zanzibar nao watapata fursa ya kuaga Jumanne Machi 23, 2021 katika uwanja wa Amani Zanzibar kisha utasafirishwa kuelekea Mwanza na utaagwa Jumatano Machi 24, 2021 uwanja wa CCM Kirumba

Alhamisi Machi 25, 2021 wanafamilia na wananchi wa Chato na mikoa ya jirani wataungana kwa pamoja kuaga mwili wa kiongozi huyo na Siku ya Ijumaa Machi 26, 2021 ndiyo siku yatakayofanyika maziko ya Magufuli nyumbani kwake Chato.