Home Mchanganyiko MABONDIA WA NGUMI ZA KULIPWA WANAWAKE ZULFA MACHO NA HALIMA VUNJA BEI...

MABONDIA WA NGUMI ZA KULIPWA WANAWAKE ZULFA MACHO NA HALIMA VUNJA BEI WAMLILIA MAGUFULI.

0
…………………………………………………………………………

WAKIZUNGUMZA KWA NYAKATI TOFAUTI JIJINI DAR ES SALAAM MARA BAADA YA KUAHIRISHWA PAMBANO LAO LILILOKUWA LIFANYIKE MACHI 27 WALISEMA MSIBA HUO NI PIGO KWA WATANZANIA.

BONDIA ZULFA MACHO ALISEMA ALIPANGALO MUNGU BINADAMU HATOLIWEZA LAKINI KIBINADAMU BADO TULIMUHITAJI.

“WATANZANIA KILA KONA WANALIA KIKUBWA NI MAZURI ALIYOLIFANYIA TAIFA” ALISEMA ZULFA.

KUHUSU KUAHIRISHWA PAMBANO LA UBINGWA KATI YAKE NA HALIMA VUNJA BEI ALISEMA LICHA YA MAOMBOLEZO LAKINI MAZOEZI ATAENDELEA ILI KUHAKIKISHA KIPIGO ALICHOKIANDAA KIKAMILIKE NA WATANZANIA WAONE BURUDANI.

“BURUDANI YA RAUNDI KUMI LAZIMA IPATIKANE NA KIPIGO KINAMUHUSU HALIMA ACHA TUMALIZE MSIBA, ALISEMA ZULFA.

KWA UPANDE WAKE HALIMA VUNJA BEI ALISEMA MAOMBOLEZO YAKE YATAAMBATANA NA MAZOEZI NA KUMUENZI NAGUFULI NI KUMPIGA ZULFS.

” MIMI BINAFSI KUMUENZI MAGUFULI BABA NA JEMEDARI NI KUHAKIKISHA MECHI NINASHINDA SIO VINGINEVYO.” ALISEMA HALIMA.

AIDHA ALIMPONGEZA MAMA SAMIA SULUH HASSAN KWA KUAPISHWA KUWA RAIS WA KWANZA MWANAMKE NA PAMBANO MAALUM LA WANAWAKE LINAFANYIKA.

MABONDIA WATAKAOWANIA MKANDA WA DUNIA SIKU YA PAMBANO LA WANAWAKE  NI HALIMA VUNJA BEI ATAKAYEPIGANA NA ZULFA MACHO KATIKA MCHEZO WA ROUNDI 10.

MABONDIA WENGINE NI FATUMA YAZIDU  ATAKAYEPIGANA NA DOROTHEA MUHOZA, HAPPY DAUDI DHIDI YA LEILA YAZIDU NA LULU KAYAGE DHIDI YA JESCA MFINANGA.

WENGINE NI MWAMNE HAJI  DHIDI YA SARAFINA JULIUS,AGNES KAYANGE DHIDI YA MWAJUMA PENGO,GRACE MWKAMELE DHIDI YA ASHA GOTA WAKATI  SALMA KIHOMBWA DHIDI YA MARIAM MUNGI NA ZAWADI KUTAKA  DHIDI YA MARTHA KIMARO.