Home Mchanganyiko Waziri Ndugulile akabithi hati ya upanuzi wa kiwanja makao makuu ya PAPU.

Waziri Ndugulile akabithi hati ya upanuzi wa kiwanja makao makuu ya PAPU.

0

Waziri wa Teknolojia na mawasiliano ya habari,Dokta Faustine Ndugulile akizungumza wakati alipotembelea mradi wa jengo la makao makuu ya PAPU lililopo mkoani Arusha Happy Lazaro).

Waziri wa mawasiliano na Teknolojia ya habari,Dokta Faustine Ndugulile akikabithi hati hiyo kwa Katibu Mkuu wa PAPU, Djibrine Younouss wakati alipotembelea makao makuu ya ofisi hizo zilizopo mkoani hapa.(Happy Lazaro)

*************************************
Happy Lazaro, Arusha

Arusha.Waziri wa mawasiliano na Teknolojia ya habari,Dokta Faustine Ndugulile amekabithi hati ya upanuzi wa kiwanja katika makao makuu ya Umoja wa Posta Afrika uliopo mjini hapa.

Akizungumza katika  hafla hiyo ya kukabithi hati hiyo kwa umoja huo,Dokta Ndugulile amesema kuwa, kitendo hicho cha kukabithi hati hiyo kimeleta manufaa makubwa Sana kwani kukamilika kwa mradi huo kutaleta tija kubwa Sana kwa umoja huo.
Amesema kuwa, kukamilika kwa mradi huo kutaongeza ufanisi mkubwa katika utendaji kazi wao huku ikitoa fursa mbalimbali za ajira pindi jengo hilo litakapokamilika.
Amesema kuwa ,mradi huo hadi kukamilika utagharimu kiasi cha shs 33.6 bilioni , ambapo aliipongeza wizara ya ardhi kwa kufanya kazi nzuri ya kukabithi hati  hiyo kwani kwa muda mrefu walikuwa hawana hati ya kiwanja hicho.
Aidha alilitaka shirika hilo kuwa kielelezo pekee cha maendeleo ambacho kitakuwa mfano bora wa kuigwa huku akiwataka kwenda na kasi mpya ,na kuhakikisha makao makuu ya posta yanafafana huduma wanazotoa katika kuhakikisha inaendeshwa kidigitali zaidi.
“Tunawaomba Sana wakandarasi mnaosimamia huu mradi mhakikishe unamalizika kwa wakati kama ilivyopangwa mwezi wa sita ,2022 hivyo mhakikishe mnafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha mnamaliza mradi huu kwa wakati na hakikisheni mnaongeza spidi zaidi .”amesema Waziri.
Naye Mwenyekiti wa bodi kutoka TCRA,Dokta Jones Killimbe amesema kuwa,ujenzi wa jengo hilo ambao ndio utakuwa makao makuu ya posta Afrika na ofisi za Kanda ya kaskazini za PAPU ni ushindi  mkubwa Sana kwao kwani unaongeza ajira kwa watanzania walio wengi pia.
Dokta Killimbe amesema kuwa,uwepo wa jengo hilo utaongeza tija kubwa kwa mapato ya  fedha za kigeni pamoja na kuwepo kwa mikutano yote ya kimataifa ambapo  ukumbi utakuwa na uwezo wa kubeba zaidi ya watu Mia tano .
“Tunashukuru sana kuongezewa eneo kwani lililokuwepo lilikuwa dogo Sana ila kwa Sasa hivi eneo limepanuliwa  na kuwa kubwa ,hivyo tunashukuru Sana kwa serikali kwa ushirikiano mkubwa katika kukamilika swala hilo.”amesema.
Naye Katibu Mkuu wa umoja wa Posta Afrika (PAPU),Djibrine Younouss amesema kuwa,anashukuru Sana serikali kwa kuwapatia hati hiyo baada ya kuwepo kwa mgogoro kwa takribani miaka 25 Sasa na hivyo hivi Sasa umeweza kufikia mwisho na kuweza kupatiwa hati hiyo.