Home Mchanganyiko WAJUMBE KAMATI YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA WATEMBELEA MIRADI...

WAJUMBE KAMATI YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA WATEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO JIJINI DAR ES SALAAM

0

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakimsiliza Meneja wa TARURA Kinondoni, Mhandisi Alberto Kindole Kabla ya kutembelea na kukagua Mradi wa uendelezaji wa Miundombinu Dar es Salaa – DMDP (Ujenzi wa Barabara ya Afrikasana – Shekilango) leo Jijini Dar es Salaam.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakitembelea na kukagua Ujenzi wa Barabara ya Afrikasana – Shekilango chini ya Mradi wa uendelezaji wa Miundombinu Dar es Salaam – DMDP  leo Jijini Dar es Salaam. Watatu kushoto mbele ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Humphrey Polepole na katikati mbele ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Aboubakar Kunenge

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Humphrey Polepole akizungumza jambo pale kamati hiyo ilipotembelea na kukagua ukarabati wa Shule ya Sekondari ya Azania leo Jijini Dar es Salaam. Watatu kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. David Silinde.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Humphrey Polepole akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo, viongozi wa Serikali, Watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma mara baada ya Kamati hiyo kutembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo katika Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) leo Jijini Dar es Salaam.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Humphrey Polepole (hayupo kwenye picha) mara baada ya kutembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo katika Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) leo Jijini Dar es Salaam.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)