Home Mchanganyiko DC MHANDO AWASHA  UMEME KAMSANGA

DC MHANDO AWASHA  UMEME KAMSANGA

0
……………………………………………………………………………..
NAWANDISHI WETU
MKUU wa Wilaya ya Tanganyika Sahele Mhando, amewasha umeme kwa mara ya kwanza katika Kijiji cha Kamsanga, kilichopo Kata Mnyagala wilayani huko mkoani Katavi.
Katika ghafla hiyo, pia amewahimiza wananchi wengine kuchangamkia fursa hii ya umeme iliyoletwa na serikali ili kujiletea maendeleo.
Amewakumbusha kuwa tarehe ya mwisho ya mradi huu wa REA III Mzunguko wa kwanza ilikuwa 28/2/2021 lakini wananchi  wameongezewa muda wa mwezi mmoja na nusu ili wengi zaidi wakamilishe kuomba na kuunganishiwa huduma ya umeme mkandarasi akiwa eneo la mradi kwani akiondoka baadhi ya bei zitabadilika.
Akiwa katika eneo la mradi mkubwa wa zahanati inayojengwa Kijijini Kamsanga, aliuhimiza uongozi wa kijiji kuendelea na ujenzi huo kwani tayari fedha zimeletwa.
Pia amewakumbusha wateja wa umeme na wananchi kwa ujumla kuwa serikali imeleta huduma ya umeme katika maeneo ya vijijini ili huduma hii isaidie kuboresha maisha yao kwa namna mbalimbali.
Mhando alitolea mfano kuepuka gharama kubwa zinazotumika katika kupata nishati nyingine kama mishumaa, mafuta ya taa, tochi za betri na nyinginezo ambazo gharama zake ni kubwa kulinganisha na za umeme.
“Huduma ya umeme itawapatia watoto mashuleni fursa na muda mwingi zaidi wa kujisomea hivyo kuinua kiwango cha elimu na uelewa katika jamii yetu hali itakayoboresha maisha zaidi,”
Pia amesema huduma ya umeme itawezesha huduma bora zaidi za afya kutolewa maeneo ya vijijini kama mwanga wa kutosha, nishati kuhifadhi baadhi ya chanjo, kuwezesha matumizi ya vifaa vya kisasa kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa.
“Kupunguza uharibifu wa mazingira kama kukata miti kwa ajili ya mkaa. Upatikanaji umeme utasaidia kuongeza kipato katika ngazi ya kaya kwa kuwa watu wataweza kuanzisha shughuli mbalimbali za kiuchumi kama mashine za kuranda mbao, kukoboa mpunga au mahindi, na shughuli nyingine ndogondogo,” amesema.