Home Mchanganyiko TUTAZINDUA MIRADI 281 WIKI YA MAJI-MHANDISI SANGA

TUTAZINDUA MIRADI 281 WIKI YA MAJI-MHANDISI SANGA

0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji  Mhandisi Antony Sanga,akizungumza na waandishi wa habari Leo March 12,2021 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Maji yanayotarajia kuanza March 16-22,2021.

……………………………………………………….

Na.Alex Sonna,Dodoma

Katika kuelekea Maadhimisho ya Wiki ya Maji yanayotarajia kuanzia March 16,2021 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji  Mhandisi Antony Sanga,amesema kuwa Jumla ya miradi 281 ya Maji yenye thamani ya sh Trion 1.014 inatarajiwa kuzinduliwa pamoja na kuwekewa  mawe ya Msingi.

Mhandisi Sanga ameyasema hayo leo March 12,2021 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habri kuhusu wiki ya Maji inayotarajiwa kuanza March 16-22,2021.

Mhandisi Sanga amesema kuwa wataadhimisha wiki ya Maji kwa kupanda miti katika vyanzo vya maji,kuhabarisha na kuhamasisha Wananchi juu ya utunzaji wa vyanzo vya Maji pamoja na kutembelea maeneo mbalimbali ya Miradi.
” Lengo Kuu la maadhimisho hayo, ni kuungana na mataifa mengine Duniani katika kutathmini utekelezaji,mafanikio na Changamoto zinazojitokeza katika Sekta ya Maji”amesema Mhandisi Sanga 
Hata hivyo Mhandisi Sanga kuwa maadhimisho hayo yenye kauli  mbiu thamani ya Maji kwa uhai na maendeleo watatumia fursa hiyo kuboresha kwa vitendo mafanikio katika Sekta ya Maji.
Sanga amesema kuwa katika kipindi cha miaka.mitano Sekta ya Maji imeendelea kukua kwa Kasi kwa kuboreshwa kwa miundombinu ya Maji  inayopelekea kuwafikia wananchi katika maeneo mbalimbali hapa nchini. 
” Tumeweza kuwafikishia Maji mijini kwa asilimia 86, wakati kwa vijijini tumewafikia kwa asilimia 53, kwa hiyo inaonesha huduma inahitajika zaidi Vijijini”‘amesisitiza
Aidha amesema kuwa jamii kwa ujumla inatakiwa kulinda vyanzo vya maji kwa sababu maji ni uhai hakuna sababu ya kuyapoteza.
Mhandisi Sanga amesema kuwa katika kuendelea kuboresha mazingira ya upatikanaji Maji hapa nchini, mradi mwingine wenye thamani ya Sh Trion moja inatarajia kuanza April mwaka huu.