Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof.Florence Luoga akizungumza na wandishi wa habari Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna akizungumza na waandishi wa habari katika Benki kuu ya Tanzania (BoT) leo Jijini Dar es Salaam Wadau mbalimbali wakifuatilia mkutano wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof.Florence Luaga na wandishi wa habari katika Benki Kuu ya Tanzania leo Jijini Dar es Salaam. Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof.Florence Luaga na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna wakionesha mikataba ya kuhamisha mali na madeni ya benki ya Biashara ya China na kuchukuliwa na Benki ya Taifa ya NMB.
(Picha na Emmanuel Mbatilo)
********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Benki kuu ya Tanzania (BOT) rasmi imehamisha mali na madeni ya benki ya Biashara ya China na kuchukuliwa na Benki ya Taifa ya NMB, hatua Hiyo imechukuliwa Baada ya Benki hiyo kuwa na Mtaji Mdogo ambao usingeiwezesha benki kujiendesha vizuri katika kuhudumia wateja wake.
Akitoa Taarifa hiyo leo jijini Dar es salaam, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof.Florence Luoga amesema Kabla ya kuiweka Benki ya biasahara ya china, chini ya Usimamizi wake, BOT ilifanya jitihada Mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwataka kuongeza mtaji kufikia kiwango kilichoitajika kisheria na kushindwa kufikia Kiwango hicho.
“Kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha 58(2)(h) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, Benki Kuu imeamua kuhamisha kwa mujibu wa sheria (acquisition by operation of the law) mali na madeni ya China Commercial Bank kwenda NMB Bank Plc”. Amesema Prof.Luoga.
Prof. Luoga ameongeza kuwa BOT,NMB Pamoja na Wadau wengine wanaendelea kuandaa taratibu za kisheria za kukamilisha mchakato wa uhamishaji wa mali na madeni ya Benki ya biashara ya China.
Hata hivyo, Prof.Luoga amesema Benki kuu ya Tanzania itaendela kulinda maslahi ya wateja wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta utulivu katika sekta ya Fedha.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna amewahakikishia wateja wa benki ya china kupata huduma zinazokidhi viwango vya kimataifa hivyo amewatka kuondokqna na wasisi wa kukosa stahiki zao zozote kwakuwa mali na fedha zao zipo katika mikono salama.
Benki ya Biashara ya China iliyo na Tawi Moja Jijini Dar es salaam, ilipewa leseni na kuanza kufanya shughuli za kibenki hapa Nchini Mwaka 2015 na kuwa miongoni mwa Benki zenye ukuaji wa chini uliosababisha hasara kwenye biashara kwa kipindi chote toka kuanza kwake, na hadi kuchukuliwa na benki kuu ya Tanzania, Beni hiyo ilikuwa na mali zisizozidi Shilingi Bilioni 5.
Aidha, Sheria ya mabaenki na Taasisi za fedha yam waka 2006, imeipa Benki kuu ya Tanzania Mamlaka ya kusimamia shughuli zote za benki na Taasisi za fedha nchini kwa lengo la kuhakikisha uimara naa uhimilivu wa sekta ya kibenki na fedha kwa ujumla.