Home Mchanganyiko WAANDISHI WA HABARI WAASWA KUTUMIA NAFASI ZAO KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI

WAANDISHI WA HABARI WAASWA KUTUMIA NAFASI ZAO KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI

0

Meneja Uendeshaji Tawi la BoT Mtwara Bi.Graceana Bemeye akisoma hotuba ya kufunga kwa niaba ya Mkurugenzi wa Tawi la BoT Mtwara katika Semina ya waandishi wa habari za Uchumi,Biashara na fedha iliyofanyika katika tawi la Mtwara.

************************************

NA EMMANUEL MBATILO,MTWARA

Waandishi wa habari wametakiwa kutumia nafasi zao kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali pamoja na umuhimu wa kila mwananchi katika kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa mbalimbali ambayo siku za hivi karibuni yamekuwa yakiathiri.

Ameyasema hayo leo Meneja Uendeshaji Tawi la BoT Mtwara Bi.Graceana Bemeye akisoma hotuba ya kufunga kwa niaba ya Mkurugenzi wa Tawi la BoT Mtwara Bw.Lucas Mwimo katika Semina ya waandishi wa habari za Uchumi,Biashara na fedha iliyofanyika katika tawi la Mtwara.

Akizungumza wakati anasoma hotuba hiyo Bi.Graceana amesema uwepo wa tahadhari katika jamii inayotuzunguka dhidi ya magonjwa yanayoibuka kuna uwezekano wa kuyashinda na tukafanya mambo mengine.

“Kuchukua tahadhari mbalimbali zinazoshauriwa na wataalamu ni kujipenda, kupenda familia zetu na kulipenda taifa letu. Kutofanya hivyo ni kutojipenda na hasara kwa mtu, familia na hata taifa”. Amesema Bi.Graceana.

Aidha amesema kuwa Benki Kuu ya Tanzania inatambua na kuthamini  mchango mkubwa unaotolewa na vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini katika kuchangia maendeleo ya taifa kwa njia mbalimbali kama vile kuhabarisha, kutoa taarifa za miradi mbalimbali ya kiuchumi inayotekelezwa hapa nchini na kuibua fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo na ambazo zikitumika vizuri zinaweza kuchangia ukuaji wa uchumi na kuongeza pato la taifa.