Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kutembelea Kituo cha Kanzidata cha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Kibaha, Mkoani Pwani, leo. Amesema wananchi wote waliotambuliwa na NIDA, na kupewa namba ambao ni zaidi ya Milioni 12, ifikapo mwezi Julai Mwaka huu watakuwa wamepata vitambulisho vyao. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dk. Anorld Kihaule.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia), akiangalia kitambulisho kilichokamilika baada ya kuhakikiwa katika Kitengo cha kuhakiki ubora wa kadi zilizozalishwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Mjini Kibaha, Mkoani Pwani, leo. Simbachawene alitembelea Kituo cha Kanzidata cha NIDA na amesema kuwa, wananchi wote waliotambuliwa na kupewa namba ambao ni zaidi ya Milioni 12, ifikapo mwezi Julai Mwaka huu watakuwa wamepata vitambulisho vyao. Wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dk. Anorld Kihaule.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto), akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo, kabla ya kuanza ziara yake Mjini Kibaha leo, kutembelea Ofisi za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dk. Anorld Kihaule, na wapili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mhandisi, Martin Ntemo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto), akisalimiana na Maafisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Mjini Kibaha, Mkoani Pwani, leo, wakati alipokuwa anawasili mjini humo kwa ajili ya kutembelea ofisi za NIDA Mkoani humo. Amesema wananchi wote waliotambuliwa na NIDA, na kupewa namba ambao ni zaidi ya Milioni 12, ifikapo mwezi Julai Mwaka huu watakuwa wamepata vitambulisho vyao. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.