Home Uncategorized WAZIRI AWESO AUPATIA UFUMBUZI MRADI WA MAJI JIJINI TANGA ULIOKWAMA TOKEA 2013

WAZIRI AWESO AUPATIA UFUMBUZI MRADI WA MAJI JIJINI TANGA ULIOKWAMA TOKEA 2013

0

WAZIRI
wa Maji Jumaa Aweso akizungumza leo Jijini Tanga wakati wa ziara yake
ya siku moja kulia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye
pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira
kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa

 

MBUNGE
wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira akizungumza wakati wa ziara
hiyo kushoto ni Waziri wa Maji Jumaa Aweso na kulia ni Mkuu wa wilaya ya
Tanga Thobias Mwilapwa
MKUU
wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa ziara hiyo
kushoto ni MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira akifuatiwa
na Waziri wa Maji Jumaa Aweso na kulia ni Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga
Mhandisi Upendo Lugongo akifuatiwa na Mkurugenzi wa Tanga Uwasa
Mhandisi Geofrey Hilly

MSTAHIKI Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shillow akizungumza wakati wa ziata hiyo

WAZIRI
wa Maji Jumaa Aweso akimsikiliza Mhandisi kutoka Tanga Uwasa Mhandisi
Salum Ngumbi wakati wa ziara yake kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Tanga
(CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira

WAZIRI wa Maji Jumaa
Aweso akichimba Mtaro wa Maji Mtaa wa Kiruku Kata ya Mabokweni Jijini Tanga wakati wa ziara yake ya siku moja

WAZIRI wa Maji Jumaa
Aweso leo amefanya ziara ya siku moja ya kukagua mradi wa Maji Mabokweni Jijini
Tanga huku akiagiza Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoani
Tanga kutoa kiasi cha fedha Sh 818 milioni ili kukamilisha mradi wa maji
Mabokweni ambao utekelezaji wake umekwama tangu mwaka 2013.

Mradi huo kwa sasa unatekelezwa
na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) huku akiagiza
pia Mamlaka ya Huduma za Nishati na Maji(EWURA) kuja jijiji Tanga kupitia
gharama za ankara za maji.

Ambapo gharama yake
ya utekelezaji ni Sh 918 milioni  na  unaohudumia kata mbili za Mabokweni na
Chongoleani ulikwama kwa muda mrefu hivyo Wizara ya Maji imetoa kiasi cha
Sh.100 milioni na kuitaka RUWASA kutoa kiasi kilichobaki. 

Kuhusu EWURA kuja
jijini Tanga baada ya mbunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu  kumueleza
Waziri Aweso kuwa baadhi ya malalamiko ya wananchi wa Tanga  kukatiwa
huduma kutokana na bei kuwa kubwa.

” Wananchi Tanga
wameunganishwa na huduma ya maji lakini hawana maji kutokana na bili
kubwa,”alisema Ummy Mwalimu.

 Kuhusu gharama za
usanifu wa utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa miradi ya maji amesema kuwa
wizara hiyo imeandaa mwongozo wa usanifu wa ujenzi ambao unaonesha gharama za
ujenzi nchini

Amesema kuwa wamekuja
na mfumo huo baada ya kubaini katika miradi ya ujenzi wa miundombinu ya maji ya
aina moja katika maeneo tofauti ilikuwa inapishana kwa gharama,hivyo kwa
kuliona hilo wizara imeaandaa mwongozo huo.

Kuhusu mradi wa
Mabokweni  ambao utekelezaji wake ulianza mwaka 2013 chini ya Mpango wa
Mradi wa Maji Vijiji 10 awamu ya kwanza(WSDP I) ambao haujakamilika amesema
kuwa miradi hiyo ya maji vijijini ilikuwa ya kihuni kutokana na kwamba ilikosa usanifu
na mengine wataalamu walikuwa wananakili na kudurufu na haikuwa na uhalisia.

“Hii michakato
isiyokuwa ya lazima katika wizara ya maji sitaki,nataka wataalam wa wizara ya
maji mkae kama jopo miradi ikamilike kwa wakati,”alisema. 

“Lakini pia hii
miradi  ya maji katika vijiji 10 ilikuwa ya kihuni ukitizama miradi hiyo
ilianzishwa haikuwa na chanzo”Alisema Waziri Aweso

Katika hatua nyingine
ameagiza bei za maji pembezoni mwa mji kwa ndoo kwenye vilula (vioski)ishuke kutoka Sh.100 mpakaSh 50.

Awali akizungumza Mbunge
wa Jimbo  la Tanga,Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) alisema kuwa mradi huo ambao unahudumia
vijiji  vya kata mbili za Mabokweni na Chongoleani umekuwa ni changamoto
kwa vijiji vya Kibafuta, Chongoleani, Mabokweni,Mzizima,Mleni na Kiruku. 

Naye kwa upande wake,Mkurugenzi
Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mhandisi Geofrey Hilly
amesema kuwa mradi huo awali ulikuwa unatekelezwa na mkandarasi Ms NCL-Abbeys
Joint Venture kwa gharama ya Sh.2,412,997,490/- lakini mkandarasi alishindwa
kutekeleza kwa wakati hivyo baada ya mabadiliko ya Sheria ya Maji ya 2019 mradi
huo ulikabidhiwa Tanga UWASA Januari 2020 kuukamilisha. 

Alisema kuwa usanifu
wa mradi ulipitiwa upya na kuanzisha mahitaji ya vifaa na gharama za mradi kwa
utekelezaji kupitia ‘Force Account ‘