Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella alipofika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa kupata taarifa ya hali ya upatikanaji wa maji katika mkoa wa Mwanza kabla ya kuanza ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maji katika mkoa wa Mwanza.
Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi. Maryprisca Mahundi (Mb) akimtua ndoo mama kichwani katika kijiji cha Mwabaratulu katika Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba wakati alipotembelea kuona mradi wa maji wa Mwabaratulu. Naibu Waziri amesisitiza kwamba wananchi watunze miundombinu ya miradi ya maji ili iwe endelevu kwa vizazi vijavyo. Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi. Maryprisca Mahundi (Mb) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Kwimba Mhe. Mansoor Hiran mwenye furaha baada ya wananchi wake katika kijiji cha Mahiga kupata majisafi na salama.
………………………………………………………………………………………..
Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) ameridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maji wilayani Kwimba na kuahidi kupeleka milioni 150 kwa ajili ya kuendelea na utekelezaji wa mradi wa maji wa Izizimba A.
Ahadi hiyo ameitoa alipofika kijijini hapo kukagua mradi huo na kukuta bado haujakamilika huku wananchi wakihangaika kupata huduma ya majisafi na salama.
“Serikali italeta shilingi milioni 150 ili kazi ziendelee na nimefika hapa kutembelea miradi na kuona changamoto ili tuweze kuzitatua na kuweka msukumo ili miradi ikamilike na wananchi wapate huduma ya majisafi na salama na yenye kutosheleza”, amesema Naibu Waziri.
Akisoma taarifa ya hali ya upatikanaji wa huduma ya maji vijijini katika Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Meneja wa Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilayani Kwimba Mhandisi Godliver Gwambasa amesema upatikanaji wa majisafi na salama kwa Kwimba vijijini ni asilimia 56.1 na mjini ni asilimia 67.
Amesema kwa ujumla hali ya upatikanaji wa huduma ya maji unaridhisha ambapo jumla ya wakazi 269,926 kati ya wakazi 480,920 sawa na asilimia 56.1 waishio vijijini wanapata huduma ya majisafi na salama na wakazi 23,916 kati ya 35,691 wa mjini wanapata huduma ya majisafi na salama sawa na asilimia 76.
Aidha, Naibu Waziri amewataka Mameneja wa RUWASA Mikoa, Wilaya na Watendaji wote wa Wizara ya Maji kuhakikisha wanafanya kazi kwa kushirikiana ili kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji nchini.
“Mameneja wote mlioteuliwa na Mhe. Waziri wa Maji hivi karibuni hakikisheni mnakwenda kufanya kazi na kushirikiana na viongozi wa maeneo husika ili kuleta ufanisi katika kutekeleza miradi ya maji nchini”, amesema Naibu Waziri Mhandisi Maryprisca Mahundi.
Kwa upande wake Mbunge wa Kwimba Mhe. Mansoor Hiran ameishukuru serikali kwa kutekeleza miradi ya maji katika jimbo lake na kuiomba serikali kukamilisha miradi ambayo haijakamilika ili wananchi wengi wa Kwimba waweze kupata majisafi na salama.
“Miradi inatekelezwa kwa fedha za Mfuko wa Maji wa Taifa, Programu za Payment by Results (PbR) na Payment for Results (PfR)”, Mhandisi Mapambano amesema na kuongeza lengo walilojiwekea ni kufikia malengo makubwa zaidi kwa wananchi kupata maji bombani.
Pamoja na hayo, Meneja wa RUWASA katika Halmashauri ya Wilaya ya Uyui Mhandisi Godfrey Shibiti amesema kupitia Programu ya Payment by Results (PbR) Serikali imekamilisha upanuzi wa mtandao wa maji wa kilomita 5.3 kutoka katika kijiji cha Mabama hadi kijiji cha Ideka ambapo wananchi wanapata huduma ya maji tangu Mwezi Machi, 2020.
Kazi hiyo ya kuwafikishia wananchi huduma ya maji imefanywa kwa ushirikiano wa watendaji wa Wizara ya Maji kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tabora (TUWASA), Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), na Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Tanganyika.
Aidha, Bw. Teddy amewataka TUWASA kuongeza mtandao wa mradi wa maji kutoka ziwa Victoria ili kumaliza kabisa tatizo la maji katika baadhi ya maeneo yenye upungufu wa huduma hiyo muhimu.
Mradi wa maji wa dharura wa mjini Kaliua umetekelezwa kupitia Mkandarasi kampuni ya Monimar & Sons Co Ltd na Serikali kwa gharama ya shilingi milioni 571.6, ambapo wananchi zaidi ya elfu 17 hivi sasa wanafaidika na huduma ya majisafi, salama na yenye kutosheleza.