Home Mchanganyiko SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA MAAFISA KAZI NCHINI WATAKAOSHINDWA KUTATUA MIGOGORO KWENYE MAENEO YA...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA MAAFISA KAZI NCHINI WATAKAOSHINDWA KUTATUA MIGOGORO KWENYE MAENEO YA KAZI

0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama,akizungumza  wakati akifungua mafunzo ya Mpango Mkakati wa Usimamizi wa Sheria za Kazi yenye lengo la kuwajengea uwezo na uelewa washiriki hao yanayofanyika leo Februari 15,2021 jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama,akisisitiza jambo kwa washiriki wa mafunzo (hawapo pichani) wakati akifungua mafunzo ya Mpango Mkakati wa Usimamizi wa Sheria za Kazi yenye lengo la kuwajengea uwezo na uelewa washiriki hao yanayofanyika leo Februari 15,2021 jijini Dodoma.

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Patrobas Katambi,akiwasisitiza washiriki wakati wa ufunguzi wa  mafunzo ya Mpango Mkakati wa Usimamizi wa Sheria za Kazi yenye lengo la kuwajengea uwezo na uelewa washiriki hao yanayofanyika leo Februari 15,2021 jijini Dodoma.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu Mhe.
Ummy Nderiananga akizungumza na washiriki wa  mafunzo ya Mpango Mkakati wa Usimamizi wa Sheria za Kazi yenye lengo la kuwajengea uwezo na uelewa washiriki hao yanayofanyika leo Februari 15,2021 jijini Dodoma.

Mwakilishi kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO) Bw. Maridadi Phanuel akizungumza wakati wa mafunzo ya Mpango Mkakati wa Usimamizi wa Sheria za Kazi yenye lengo la kuwajengea uwezo na uelewa washiriki hao yanayofanyika leo Februari 15,2021 jijini Dodoma.

Kamishna wa Kazi Brigedia Jenerali Francis Mbindi,akiwasilisha taarifa  kwa washiriki wa mafunzo ya Mpango Mkakati wa Usimamizi wa Sheria za Kazi yenye lengo la kuwajengea uwezo na uelewa washiriki hao yanayofanyika leo Februari 15,2021 jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama,wakati akifungua mafunzo ya Mpango Mkakati wa Usimamizi wa Sheria za Kazi yenye lengo la kuwajengea uwezo na uelewa yanayofanyika leo Februari 15,2021 jijini Dodoma.

Kamishna Msaidizi wa Kazi Bi.Rehema Moyo akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama,mara baada ya kufungua Mkutano wa  mafunzo ya Mpango Mkakati wa Usimamizi wa Sheria za Kazi yenye lengo la kuwajengea uwezo na uelewa yanayofanyika leo Februari 15,2021 jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mkutano mara baada ya kufungua mafunzo ya Mpango Mkakati wa Usimamizi wa Sheria za Kazi yenye lengo la kuwajengea uwezo na uelewa yanayofanyika leo Februari 15,2021 jijini Dodoma.

PICHA ZOTE NA ALEX SONNA-FULLSHANGWE BLOG

……………………………………………………………………………….

Na Alex Sonna,Dodoma.

SERIKALI imesema kuwa itawachukulia hatua za kisheria Maafisa kazi watakaoshindwa kutatua migogoro inayojitokeza katika maeneo yao ya kazi.

Kauli hiyo imetolewa leo Februari 15,2021 Jijini Dodoma na Waziri wa  Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera,Bunge,Kazi,Ajira Vijana na Wenye ulemavu Mhe.Jenista Mhagama wakati akifungua mafunzo ya mpango mkakati wa usimamizi wa sheria za kazi wenye lengo la kuwajengea uwezo na uelewa.

Mhe.Mhangama amesema kuwa azma ya serikali ni viwanda ni lazima ufumbuzi wa changamoto katika maeneo ya kazi upatikane ili wananchi kufanya kazi katika mazingira salama wakipatiwa haki zao za msingi.

“Tumieni mafunzo haya kama fursa ya kuleta mabadiliko acheni kufanya kazi kwa mazoea kuna migogoro mingi huko nje nisingependa msubiri yafike kwetu wakati nyinyi mpo”amesema Mhangama

Hata hivyo amesema kuwa ni wajibu wetu kutatua kero zao ili waweze kupatiwa stahiki zao mkumbuke wanategemewa na familia zao wanafanyishwa kazi bila mikataba , mishahara inachelewa wanaishi katika wakati mgumu.

Aidha Mhangama ameagiza kutolewa kwa taarifa ya robo ya mwaka kwa kila mkoa kuhusu utendaji wake hasa katika utatuzi wa migogoro maeneo ya kazi huku akiipongeza   mikoa iliyofanya vizuri katika kuchukua hatua za kutafuta suluhu ya masuala ya wafanyakazi.

“Kuna mikoa imefanya vizuri kushughulikia matatizo ya wafanyakazi kama Geita,Tanga,Iringa,Rukwa,Mtwara na Kilimanjaro niwaombe muongeze nguvu kwa Mbeya, Njombe,Dar es salaam,Morogo na Mara mmefanya vibaya taarifa zote ninazo sasa kupitia taarifa ya robo ya mwaka kwa mkoa utakojirudia kufanya uzembe tutachukua hatua,”amesisitiza.

Awali Mwakilishi kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO),Maridadi Phanuel amesema mafunzo hayo yamelenga katika maeneo mbalimbali ikiwemo ukuzaji wa ajira zenye staha,hifadhi ya jamii,majadiliano ya utatuzi kukuza uhusiano na haki katika sehemu za kazi,

“Mkurugenzi wetu anaishukuru Serikali kwa ushiriakiano ambao imekuwa ikitupatia  ILO, tunashirikiana na wizara yenye dhamana  kuwajengea uwezo tunatamani kuona kunakuwa  na uhusiano mzuri katika maeneo ya kazi,”amesema Bw.Phanuel.

Naye, Naibu Waziri anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi ameeleza kuwa mpango huu wa mafunzo ni mzuri na utawajengea uzoefu maafisa kazi ambapo wataweza kujiwekea utaratibu mzuri wa utendaji wa kazi zao.

Kwa upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu Mhe.Ummy Nderiananga,amesema kuwa ni lazima ushirikishwaji wa kundi hilo utasaidia kupata ajira na kuifanya jamii kutambua thamni yao kwani bado kuna changamoto ya uotaji wa ajira  katika sekta binafsi.

“Niliombe Shirika la ILO wakati mwingine kutoa mafunzo kwa kundi la watu wenye ulemavu bado kuna shida katika Nyanja ya ajira sasa ikiwa tunataka kufikia katika malengo ya maendeleo endelevu ifikapo 2030  ni lazima tusimamie kundi hili kupata kazi za staha  na wasibaguliwe kutoaka na ulemavu wao wapewe fursa kama wengine ,”amesema Mhe.Nderiananga

Kamishna wa Kazi Brigedia Jenerali Francis Mbindi,amesema  kuwa mafunzo hayo yameshirikisha maafisa kazi wasimamizi wa sheria za kazi pamoja na maafisa kazi waendeshaji wa mashtaka hivyo mafunzo hayo yataimarisha utendaji kazi katika Idara ya Kazi na hatimaye kupunguza malalamiko.