Home Mchanganyiko MATUKIO KATIKA PICHA :WAJUMBE WA BARAZA LA WADHAMINI CCM WATEMBELEA CHUO CHA...

MATUKIO KATIKA PICHA :WAJUMBE WA BARAZA LA WADHAMINI CCM WATEMBELEA CHUO CHA CCM CHA MWALIMU NYERERE KIBAHA

0

Mwenyekiti wa baraza la wadhamini la Chama Cha Mapinduzi (CCM)  ,ANNA ABDALLAH  aliyesimama akizungumza jambo ,wakati alipoambatana na wajumbe wa baraza hilo ,kwenda kutembelea na kujionea maendeleo ya ukamilishaji wa ujenzi wa Chuo cha uongozi na Itikadi cha Mwalimu Nyerere ,kilichopo Kwamfipa,Kibaha,mkoani Pwani, wa kwanza kulia aliyekaa ni Msimamizi wa mradi huo ,Emmanuela Kaganda

Naibu katibu mkuu wa CCM Bara ,Rodrick Mpogolo aliyesimama akitoa maelekezo  ,wakati wajumbe wa baraza la wadhamini la CCM walipokwenda kutembelea na kujionea maendeleo ya ukamilishaji wa ujenzi wa Chuo cha uongozi na Itikadi cha Mwalimu Nyerere ,kilichopo Kwamfipa,Kibaha,mkoani Pwani.

Msimamizi wa mradi wa ujenzi wa chuo cha uongozi na itikadi cha Mwalimu Nyerere ,Kibaha ,Emmanuela Kaganda  ,akitoa taarifa ya mradi kwa mwenyekiti wa baraza la wadhamini la Chama Cha Mapinduzi (CCM)  ,ANNA ABDALLAH  (kulia) pamoja na wajumbe wa baraza hilo ,walipotembelea kujionea ujenzi wa chuo hicho.  (picha na Mwamvua Mwinyi).