Home Mchanganyiko FEDHA ZA TASAF ZAMSAIDIA MLENGWA WILAYANI IGUNGA AANZISHA MRADI WA UFUGAJI NGURUWE

FEDHA ZA TASAF ZAMSAIDIA MLENGWA WILAYANI IGUNGA AANZISHA MRADI WA UFUGAJI NGURUWE

0
Nguruwe wa Mlengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora,Hoka Leta wakiwa katika banda lao.
Mlengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora,Hoka Leta akiwaonyesha jana waandishi wa habari banda la nguruwe alizozipata kutoka na fedha za TASAF.
Mlengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora,Hoka Leta (kulia) akiwaonyesha jana Afisa Habari wa TASAF Estomu Sanga (kushoto) banda la nguruwe alizozipata kutoka na fedha za TASAF.
Mlengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora,Hoka Leta akiwaonyesha jana waandishi wa habari nyumba yake aliyoijenga  kutokana na miradi aliibua kutokana na fedha za TASAF.
Picha na Tiganya Vincent
……………………………………………………………………………..

NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA

FEDHA zinazotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) zimemwezesha mlengwa wa mpango wa kunusuru kaya masikini Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora,Hoka Leta  kuanzisha mradi wa ufugaji wa nguruwe  wapatao 23 na kumwezesha kuw na fedha za ukopeshaji wanachi wengine.
Mlengwa huyo alitoa ushuhuda huo jana wakati viongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na waandishi wa habari walipokuwa katika ziara ya kujifunga mafanikio ya walengwa.
Hoka alisema baada ya kupata fedha za TASAF alianza kwa ununuzi watoto wa nguruwe mawili  na ndipo walizaana na kufikia 23.
Alisema kupitia mradi huo ameweza kujengwa nyumba ya kisasa na kukodi mashamba na kulima mpunga ambapo amezalisha magunia 100 kwa kipindi cha mwaka jana.
Mlengwa huyo aliongeza kuwa ufugaji wa nguruwe  umemwezesha kupata kiasi cha shilingi 300,000/= hadi 500,000/= kulingana na soko wakati husika na kuongeza kuwa wateja wake wakubwa wanatoa katika mikoa ya Arusha na Dar es salaam.
Alisema pia kupitia ufugaji  wake amekuwa akikodisha madume ya ngurume kwa wafugaji wengine wanaohitaji mbegu kwa gharama ya shilingi 15,000/= kwa mmoja ambapo mradi huo nao umemsaidia kumudu maisha yake.
Aidha Leta alisema kupitia kilimo hicho cha mpunga katika mavuno ya mwaka huu anatarajia kuvuna zaidi ya gunia 100 za mpunga na mazao mengine.
Alisema kupitia fedha za TASAF aliweza kuanzia kilimo cha zao la alizeti na kupata dumu 20 za mafuta ya alizeti ambapo fedha alizopata zilimsaidia kununua vifaa vya ujenzi ikiwemo saruji , mchanga , mbao na mabati.
Leta alisema kabla ya kupata fedha za TASAF alikuwa akiishi maisha ya dhiki ambao alikuwa akisubiri watu watupe ndala zilizochoka na ndipo yeye alizichukua kwa ajili ya kuvaa.
Aliongeza kuwa dhiki nyingine aliyokuwa akikabiliana nayo kabla ya kupata fedha za TASAF ni pamoja na kutokuwa na uhakika wa chakula kwa kuwa alitegemea zaidi biashara ya kutembeza viazi mitamu na ndipo alizalishe shilingi 500/= kwa ajili ya familia yake.
Leta alisema kupitia miradi yake iliyotokana na fedha za TASAF hivi anao uwezo wa kukopesha watu mbalimbali fedha ambapo hadi hivi sasakuna watu anawadai zaidi shilingi milioni 1.5.
Mlengwa huyo alisema ni vema kwa walengwa wanaopata ruzuku kupitia mpango huo, kuzitumia  katika shughuli za uzalishaji mali kwa  lengo la kujiua kiuchumi na  kuachana na umasikini na wasirudi nyuma .
Aliishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kuwawezesha fedha za mpango huo na kufanikiwa kujitegemea na kuilea familia yake ya watoto 7 .
Mlengwa huyo alisema hata akitolewa katika Mpango huo hivi sasa hawezi kushindwa kujimudu yeye na familia yake katika  mahitaji mbalimbali.