Home Uncategorized TANGA PRESS CLUB KUFANYA BONANZA NA WADAU FEBRUARY 13 MWAKA HUU JIJINI...

TANGA PRESS CLUB KUFANYA BONANZA NA WADAU FEBRUARY 13 MWAKA HUU JIJINI TANGA

0

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani
Tanga (Tanga Press Club) Lulu George akizungumza na waandishi wa habari

KLABU ya
Waandishi wa Habari Mkoa wa Tanga imeandaa Bonanza ambalo litafanyika Jumamosi
wiki hii kwenye uwanja wa shule ya Msingi Bombo Jijini Tanga.

Akizungumza
na waandishi wa habari leo Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani
Tanga (Tanga Press Club) Lulu George amesema kwamba bonanza hilo linalenga
kuimarisha mahusiano baina ya waandishi wa habari na wadau.

Lulu alisema
mbali na kuimarisha mahusiano kati ya waandishi na wadau pia linalenga
kuwajenga waandisha wa habari kiafya pamoja na wadau kuiwezesha miili yao kuwa
na kinga imara inayoweza kukabiliana na magonjwa mbalimbali.

“Hili ni
bonanza la kwanza kwa mwaka huu tumeandaa na tutaendelea kuhakikisha
tunayaandaa mara kwa mara kwa lengo la kuimarisha mahusiano mazuri na hii
itasaidia kuweza kutekeleza vema shughuli zetu za kila siku na wadau”Alisema Lulu
George

Mwenyekiti
huyo aliwataka wadau mbalimbali wakiwemo wanahabari kushiriki kwa wingi ili
kufanikisha zoezi hilo lenye manufaa ya kimahusiano na kiafya.

Awali akizungumza
katika mkutano huo,Katibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Tanga Mbonea
Herman alisema bonanza hilo litahusisha michezo mbalimbali ikiwemo Joging,Kuvuta
kamba,Mpira wa miguu,kukimbiza kuku na kukimbia kwa kutumia gunia.

Mbonea alisema
bonanza hilo litaanza kwa staili ya matembezi asubuhi yatakayoanzia kwenye
viwanja vya Klabu wa Waandishi wa Habari iliyopo karibu na Polisi Mess na
kuelekea katika viwanja vya shule ya Msingi Bombo mahali ambapo shughuli hiyo
zitafanyika.

Tukio hilo ni
la kwanza kufanyika katika kipindi cha mwaka huu 2021 lakini mpango katika
mwaka huu ni kuwa na matukio mbalimbali ya kijamii ikiwemo kuendesha zoezi la
uchangiaji wa damu baada ya kuonekana jambo hilo ni muhimu kwa jamii.